Kila mwanaume anapenda kutaka kujua jinsi ya kumzuzua mwanamke mpaka
ampende. Lakini wengi hushindwa kutimiza azma hii kwa kuwa hawajui mambo
muhimu ya kufanya ili aweze kumzuzua mwanamke.
Je, uko tayari kuzijua mbinu TANO kuu za kumfanya mwanamke azuzulike kwako?
Najua labda ushawahi kuwaona mwanamke fulani wakiweza kuzuzuliwa na
mwanaume, na mwanamke kama huyu anacheka mara kwa mara huku akikiri kuwa
mwanaume flani anajua kuzuzua. Well, waonaje kama ni wewe sasa hivi
unapewa sifa kama hii?
Kupewa sifa ya kuwa mzuzuaji na mwanamke ni sifa kubwa zaidi kwa
mwanaume kutoka kwa mwanamke. Na si kwa ajili ya sura, shepu wala ujanja
wako. Yote itategemea na kipawa chako na tajriba yako wa kuzuzua.
So, utamzuzua vipi mwanamke?
Kumzuzua mwanamke kutategemea uwezo wako wa kuwasiliana na yeye na
kumfanya ajihisi kuwa na furaha wakati wote. Tumia mbinu tano ambazo
tumezihakikisha utendaji wake.
#1 Ongea na yeye mambo ambayo anataka
Unaweza kuona kuwa haina umuhimu wowote, sababu wanaume wengi hufanya
hivi. Wanaume wengi hubaki wakijiuliza kuna haja gani kwao kuongea
mambo ambayo mwanamke anataka kuongea. Mbona wanawake hawawezi kuongea
mambo ambayo mwanaume pia anataka?
Bila shaka, wanawake wanaweza. Wanawake pia wanakuwa active kutaka kujua
aina ya mwanaume ambao wanajihusisha nao. Lakini wakati mwingine, haswa
unapotaka kumfurahisha na kuteka atenshen yake kwako, ni vizuri kujua
mambo ambayo yanagonga ndani ya kichwa cha mwanamke. Na kumakinika
kuteka atenshen yake haimaanishi kuwa mwanaume anapaswa kuongea kuhusu
mambo ya vipodozi na urembo na mwanamke, La. Daraja kati ya mwanaume na
mwanamke imepungua siku hizi. Ni rahisi kuongea na mwanamke mambo ambayo
anapenda bila hata kutatizika. Bora tu uhakikishe kuwa utaweka kando
maswala ya mipira, elekroniki na hesabu katika mazungumzo yenu.
#2 Msuke
Wakati unapozungumza na mwanamke, ni rahisi kumfanya aweze kuongea na
wewe. Lakini hio haitoshi. Kama unataka kumzuzua mwanamke basi
unahitajika kumfanya ajihisi huru, na pia umuonyeshe kuwa uko interested
na yeye.
Marafiki hawawezi kuzuzuana hadi wavuane chupi. So kama utaongea na yeye
kama rafiki yako basi atakuona tu kama mwanaume anayevutia. Lakini
hatakuona kama mwanaume anayezuzua. Kutaka kuonekana kama mwanaume mweye
uwezo wa kuzuzua machoni mwa mwanamke, basi unahitajika kumfanya akuone
wewe kama mwanaume ambaye anaweza kutoka naye deti. Na kufanya hivyo
lazima umsuke.
Na unapochukua hatua ya kumsuka hakikisha kuwa hautumii maneno kama
‘unapendeza’, ‘leo umerembeka’, ama kutumia mstari wowote ambao
unaendana na hii. Inaboesha na haionekani kuwa na uhalisia wowote.
Badala yake tumia maneno ambayo yanamlenga yeye moja kwa moja. Umemuona
amepaka wanja kwa macho? Mwambie “Leo nauona utofauti kwa sura yako,
kwani umejipaka nini?” akijibu hajui, ama akikwambia ni wanja mtamkie,
“Basi unapendeza kupindukia, hata nashindwa kuacha kukuangalia.” Haya ni
baadhi ya maneno ambayo unaweza kumsifia yeye binafsi na moja kwa moja.
Kwa kumsuka utakuwa umefanya mambo matatu wakati mmoja. Kwanza ni kuwa
umemchangamsha kwa kumfanya atabasamu. Pili umemfanya atambue kuwa wewe
umemuona anapendeza. Na tatu ni kuwa umemuonyesha kuwa umevutiwa na
yeye. Yote haya ni ya kufanya ili akutizame kama mwanaume ambaye anaweza
kutoka deti na yeye.
#3 Kuwa mcheshi
Kufikia sasa kwa kuwa tayari ushamfanya kuwa na tabasamu kwa kumsuka, ni
wakati wa kuingia katika himaya yake binafsi. Kila mtu huwa na himaya
yake binafsi na kawaida hatujihisi huru iwapo mtu mwingine ataingia
katika himaya zetu unless mtu huyu ni mtu ambaye tunajihisi comfortable
naye. Ok, kwa kueleza juu juu ni kuwa mfano hauwezi kumuaproach mwanamke
usiyemjua halafu uende ukakae na yeye sako kwa bako na uongee na yeye
kana kwamba ni mtu unayemjua na kufahamiana naye tangu kitambo bila
kufuata taratibu zake.
Kumfanya ajihisi huru na wewe, lazima uwe na muda mrefu na yeye ili
akuzoee. Akikuzoea hapo sasa unaweza kutumia ucheshi ambao unaweza
kuutumia kwa manufaa yako. (machapisho ya awali tuliongea kuhusu jinsi
ya kuwa mcheshi)
Hapa hakikisha kuwa wakati unapomchekesha mwanamke usitumia wala
usijilazimishe kutumia hekaya ama stori za kuchekesha ulizozisikia
mahali ama kusoma kitabuni. Kinachohitajika kwako ni kuwa mhalisia tu,
mwanamke akipendezwa atacheka tu.
#4 Mtongoze
Wanaume huwatongoza wanawake kila wakati, lakini wakati mwingine
wanawake wanahisi kuwa wanaume wanaowatongoza ni mafala. So usivuke
mipaka yako wakati unapomtongoza sababu anaweza kukubeza. Mbinu rahisi
ya kuanza kutongoza ni kwa kuanza kwa wepesi. Muulize wikendi atakuwa
wapi baada ya shughli zake za wiki, muulize kuhusiana na sehemu
anayopenda kubarizi na pia mkahawaha anaoupenda, na kitu chochote kile
kinaweza kuhusiana na yeye moja kwa moja. Atajua kuwa unajaribu
kumtongoza kwa sababu hakuna mtu anaweza kuuliza maswali haya bila lengo
madhumuni.
Halafu mrushie hili swali.
“Enhe, hii inaweza kuwa personal, hivi wewe una boyfriend? Kama uko
naye, basi moyo wangu naona unaweza kuyayuka wakati wowote kuanzia
sasa!”
Hii inaweza kuoneka nzito lakini hufanya kazi wakati wote.
Atacheka, lakini mstari huu utakuwa umepitisha lengo lako kwako, na
atajua kuwa uko interested na yeye. Lakini usifanye mambo yaende
segemnege kwa kunyamaza kwa muda baada ya kukupa jibu lake. Endelea na
stori nyingine ujifanye kana kwamba swali hilo halikuwa na umuhimu
wowote kwako. Lengo lako umeliweka wazi lakini hutaki ajihisi kuwa
hayuko huru mbele yako.
#5 Mguse
Hii ni sehemu hatari, lakini unahitaji muda kujifundisha. Unataka kujua
jinsi ya kumzuza mwanamke, sawa? Basi kumgusa wakati ufaao inakupa point
tano muhimu ambazo unahitaji kujua ili umzuzue mwanamke. Kama umepata
kila kitu sawa, basi utakuwa umefanikiwa kwa kila kitu.
Lakini tena kumgusa mwanamke ni sawa na kucheza na moto. Ukiwa na haraka
ya kuuguza hautahisi lile joto. Na ukikaa muda mrefu ukiugusa,
utachomeka. Unaona venye hatari iliopo hapa?
Unaweza kutuma msisimko hadi kwa uti wake wa mgongo kwa kumgusa kiulaini
kama tayari umemchangamsha awali. Lakini kumbuka hili, mguse wakati
ambao unataka kumgusa pekee, kama vile kugusa sikio lake wakati
unapomsifia kuhusu vipuli alivyofaa, kupapasa nywele zake wakati kuna
upepo mkali, ama kuuwekeza mkono wako nyuma yake wakati mnavuka
barabara. Mguso ni njia ya kuingia katika hulka ya mwanamke, so
unahitajika kuwa makini zaidi na umsome vile ambavyo atareact kabla
umguse kwa mara ya pili.
Upo?
No comments:
Post a Comment