Nipo tena kwa Mara nyingine katika kubadilishana uzoefu juu
ya mambo mbalimbali yanayohusu mahusiano,kuna jambo limekuwa
likiniumiza kichwa sana ni swala zima la kulogwa au kupewa limbwata na
mwanamke.
Nidhahiri kabisa mambo haya katika jamii yetu yanafanyika
kwa baadhi ya wanawake huwa wanawafanyia wanaume,na tatizo hilo limezidi
kushamiri zaidi kutokana na ongezeko kubwa la waganga wa kienyeji.
Nimefanya research kwa baadhi ya waganga wameniambia wateja
wao wakubwa ni wanawake na shida kubwa wanayokuwa wanahitaji ni kuolewa
au kuwadhibiti wanaume zao.
Nami mekuja kugundua wanaume wengi huwa wanafanyiwa madawa
ila wakati mwengine mungu huwalinda hawazuriki bila ya wao kujua na
wanaume wengi ambao wapo katika hatari hiyo ni wale wenye kipato kidogo
ambacho kinarizisha.
Sasa basi nimejaribu kutafuta prevention za ki psychology,
ambanzo hazihusiani na mambo ya kishirikina ambazo zinaweza kukusaidia
uepukane na janga hilo nimejaribu kutumia experience yangu ni kama
zifuatazo:
Kwanza kabisa kama mwanaume unapoanza mahusiano ya
kimapenzi na mwanamke unatakiwa umwambie mwanamke vitu ambavyo huvipendi
na moja katika ya vitu ambavyo utamwambia hupendi ni mambo ya
kishirikina na unatakiwa umsisitizie kwamba endapo kama wewe utagundua
yeye anapenda mambo ya kwenda kwa waganga umwambie siku hiyo ndio
itakuwa mwisho wa mapenzi yenu.
Jambo la pili ukiwa unaishi na mwanamke ndani usipende kula
chakula peke yako hata kama umechelewa kurudi umerudi labda saa sita
usiku mwambie mke wako mle wote chakula cause peke yako hujazoea kula au
kama mna mtoto wenu ama ndugu wa mwanamke kula nae chakula.
Kwa kufanya hivyo mwanamke atajua hupendi kula peke yako na
unampenda yeye na ndugu zake kumbe unalako moyoni unajilinda na
limbwata,jambo la tatu pendelea kufanya ibada ukitaka kula na ukitaka
kulala na mshirikishe mkeo katika ibada na wakati mwingine msomee
maandiko ya vitabu vya mungu ambayo yanakataza ushirikina na adhabu zake
watakazo zipata wanaofanya mambo hayo,mengine mnaweza mkaongezea.
Note:Mwanamke anaweza akawa sio mshirikina lakini
akashawishiwa na marafiki zake akufanyie hivyo,kwa hiyo kama mwanaume ni
bora ukachukua tahadhari mapema.
No comments:
Post a Comment