Sababu za kwako kumzimia mwanamke ambaye tayari ana boyfriend sizijui ni
zipi. Labda ulikuwa umemzimia tangu zamani lakini ulikosa mbinu za
kumtongoza akachukuliwa, labda unataka kulipiza kisasi, ama labda unaona
huyo boyfriend aliye naye sahizi hafai...ama sababu
tofauti kabisa na hizi. Well, jawabu langu ni kuwa, hakuna chochote
kisichowezekana hapa ulimwenguni. Mwanzo inaweza kuwa rahisi zaidi
kumnyakua mwanamke huyo bila wewe kutoamini. Kile unachohitajika sasa
nikufuata hizi mbinu ambazo zimehakikishwa na kufanyiwa utafiti.
1. Kuwa mwanaume ambaye anakuwa kwa ndoto ya kila mwanamke
Kuwa na tabia za kigentleman. Kuwa gentleman itamfanya mwanamke yeyote
yule akuwaze na kukutia ndotoni mwake na pia kutaka kukujua zaidi ama
atleast kuwa mnakutana mara kwa mara. Hakikisha pia kando na kuwa na
tabia za ugentleman, hakikisha ya kuwa unapenda kuwa karibu na yeye na
akianza kuonyesha dalili zozote zile, mfano kukupa busu kipajini au kwa
shavu, ama kupenda kukukumbatia, fahamu kuwa unaenda sambamba na ajenda
yako. Pia kumfanya akuweke kwa akili yake lazima uonyeshe interest zako
kwake.
2. Usiache kumuangalia
Wakati ambapo mnakuwa pamoja mnaongea, hakikisha kuwa macho yako yote
yanamuangalia yeye kila wakati. Hii ni ishara ambayo itamuonyesha yeye
kuwa una macho ambayo yanamzimia yeye pekeake. Mbinu hii itamfanya kwa
urahisi kutaka kukutia machoni akuangalie kama bado tabia ya kumuangalia
yeye uko nayo ama la.
3. Usisahau kutumia lugha za kumsifu
Ukweli usemwe. Watu wakiwa katika mahusiano kwa muda mrefu kuna vitu
mbavyo wanavichukulia kama mzaha. Mfano katika mahusiano ya mwanamke na
mwanamume, unapata mara nyingi wamezoeana kiasi cha kuwa wanajihisi
uhusiano wao umeshikana kiasi cha kuwa wanasahau mambo madogo madogo
kama vile kumsifu mpenzi wake, kumzawadi nk.
Hii ni njia wapo rahisi ambayo itakuwezesha wewe kuuteka moyo wa
mwanamke ambaye ana boyfriend kwa haraka. Maneno ya kumsifu ambayo
hajaambiwa kitambo yanaweza kumchanganya akili mwanamke yeyote na
kumfanya kuingiwa na hisia mbili mbili. Niaminiukitumia mbinu hii
utakuwa na nafasi kubwa ya kwako kufaulu kumpata mwanamke aina hii.
4. Hakikisha umemuelewa ndani na nje
Wengi wangeuliza itakuwaje kumfahamu mwanamke ndani na nje na tayari ana
boyfriend? Kama ulikuwa hujui basi ni hivi, kulingana na utafiti,
inasemekana kuwa akili ya mwanamke inafanya kazi tofauti kabisa na ya
mwanamume. So usitilie shaka kabisa hapa. Pia hakikisha umesikiliza kila
kitu ambacho atakwambia na utilie maanani yote atakayosema.
KUMBUKA: Wanawake hujiskia huyu kuongea yote ambayo yanatoka akilini
mwao kwa mwanamume ambaye anamuamini na kumkubali. Hivyo ukiona umefikia
level hii fahamu ya kuwa hauko mbali na kutimiza lengo lako kuu. Pia
usisahau kutumia maneno ya uchezi ili kupunguza tenshen ambayo inaweza
kuwa kati yenu.
ONYO: Usijaribu kumwambia moja kwa moja kuwa unamzimia na unataka
kumpokonya kutoka kwa boyfriend wake kwa sababu hio haitafanya kazi
kamwe.
No comments:
Post a Comment