Wanawake kuchagua wanaume masharobaro aka badboys kuwaliko wanaume wa
kawaida si jambo geni na hutokea mara kwa mara. -aidha katika vyuo,
vilabuni, sinema, maktabani ama sehemu yeyote ile. Wanaume masharobaro,
kama wanaume wengine, wao pia wanamaumbo ya kila
aina, shepu na mvutio wa kijinsia. Kama wewe ni mwanamume wa kawaida
ambaye humaliza wa mwisho ama ushawahi kupoteza mpenzi wako kwa
sharobaro fulani, hapo chini kuna nadharia ambazo zitasaidia kueleza kwa
nini wanawake wanapenda sana kuvutiwa na wanaume masharobaro.
1. Hamu ya kufuata
Kufuata kitu ambacho unakipenda huwa kuna msisimko fulani mtu hupata.
Lakini msisimko zaidi hutokea wakati ambapo mtu anajaribu kufuata mtu
ambaye hataki kujulikana mienendo yake ya kimaisha, kufuatwa ama
kueleweka kimaisha. Haya ndio maisha anayoishi mwanamume sharobaro.
Wanawake wanapenda sana wanaume ambao hawaeleweki kimaisha (yaani
hawatambuliki) ama kutaka kujua maisha yao. Na wewe kama mwanamume
unataka kutumia huu udhaifu kwa manufaa yako, wakati mwingine unafaa
kumfanya mwanamke abaki na maswali chungu nzima kutaka kukujua zaidi.
Kama unampenda, jaribu kadri iwezavyo kutojaribu kumuonyesha. Badala
yake mpe pia yeye changa moto kwa kuweka ujanja wa kutoeleweka mara kwa
mara. Hii ni njia moja murua ya kuhakikisha utaingia katika akili yake.
2. Kutaka kuwafunga fundo
Kitu kingine ambacho wanawake huvutiwa kwa sharobaro ni kutaka nafasi ya
kuwafunga fundo ama kuwajeuza tabia zao. Mwanamke, amezaliwa naturally
na hisia za uzazi, yaani kutaka kujeuza mtu mwenye tabia ovyo kuwa na
tabia nzuri. Hii huibua hisia halizi za uzazi ndio maana kama mwanamume
unapaswa wakati mwingine kumsumbua mwanamke hikisia, kimawazo na
kadhalika. Unafaa kuwa mpinzani lakini usiwe mhalifu. Unafaa kuwa hatari
lakini usipitishe kiwango ambacho kitamwogopesha. Kimtazamo, unafaa
kumfanya mwanamke auonyeshe uke wake wote ili kujaribu kukubadilisha,
mpe nafasi ajaribu kuubadilisha upande wako wa kiza na mwishowe
kukufanya uwe mwanamume thabiti katika mchakato mzima.
3.Uanaume uliothabiti
Wanaume masharobaro (na si wale feki) karibu nyakati zote huwashinda
wanaume wa kawaida kwa sababu ya mambo mawili makuu. Kwanza ni kuwa ni
wanaume majasiri na pili wanaudhibiti uanaume wao kwa kuwa ngangari
kimaisha. Kutoogopa kwao kwa jambo lolote ndiko kunawafanya wanawake
kuvutiwa nao. Wanawake wengi wanavutiwa na wanaume ambao ni hatari,
ngangari na wenye nguvu kwa sababu si rahisi kuchezewa au kufanyiwa
masihara. Ukismama kumtetea mwanamke kuhusu mahitaji yake na uovu, hii
inamaana ya kuwa una uwezo wa kusimama kando yake na jambo lolote lile.
Kuweza kuonyesha level ya kuwa wewe ni mtu usiekuwa na woga wowote,
unafaa kumwonyesha mwanamke wako kuwa una uwezo wa kuwa ngangari mahali
popote pale ili mradi kumlinda yeye tu.
4. Uoga wa kujitwika majukumu
Wanaume masharobaro hupenda kuhepa majukumu yanayohusiana na mahusiano.
Kwa wanawake ambao wana uoga huo huo wa kuwa na majukumu, masharobaro
huwavutia sana na kuwaona kama hakuna wanaume wazuri kama hao. Kwa kuwa
wanawake hawatajitweka majukumu, huwa hawana haja ya kujishughulisha na
hisia za kipenzi ambazo ni stress. Pia ni habari njema kwa wanawake
ambao wako tayari kwa uhusiano wa kimapenzi wa muda mfupi pekee. Lakini
kama kawaida, mwisho wa siku lazima mwanamume sharobaro au mwanamke
mtundu lazima kuna sehemu fulani ndani ya mawazo yake anatamani kuwa na
mahusiano ya kudumu na pia kupendwa. Hivyo siri hapa ni kuipima miondoko
yake na uangalie level yake ya kujitwika majukumu katika mapenzi halafu
sasa uanze na hapo.
Upende usipende, wanaume masharobaro watakuwa na nafasi kubwa katika
moyo wa mwanamke. Kuna kitu ndani yao ambacho kinawasababisha wanawake
kuangua mwili mzima kihisia na kimapenzi kwao. Lakini hii haimaanishi
kuwa lazima kila mwanamume ajeuke na kuwa sharobaro ili aweze kuwa na
nafasi rahisi ya kutongoza mwanamke aliye kwa ndoto zako. Kile
unachotakiwa kufanya ni kucheza mchezo mzima kiwastani. Daima unafaa
kuwa vile ulivyo huku ukiingiza tabia flani za usharobaro hivi katika
miondoko yako. Kama kuna kitu nzuri kati yenu wawili, basi pia kuna
sehemu mbaya ambayo unaweza kuitumia ili ukajinufaisha nayo
No comments:
Post a Comment