Kama unatabia ya kushindwa ama kupata tatizo la kuongea na wanawake
ambao wanakuvutia, basi ni wakati murua wa kwako kutafuta mbinu ambayo
itakufanya wewe kuwa na ari na kutokuwa na wasiwasi wowote wakati ambapo
unaongea nao.
Wakati mwingine, wanaume hujiskia ndivyo sivyo wakati wanapoongea na
wanawake na mara nyingi wanapalia kutoongea na wao kabisa kwa sababu ya
kujiskia ndivyo sivyo. Hii mwishowe inachangia kwa wao kutoweza
kuwafahamu wanawake vizuri ama kushindwa kuwatoa date. Kama umechoshwa
na jambo hili ambalo linakuandama siku nenda siku rudi, basi unahitaji
njia rahisi ya kukuwezesha wewe kuzungumza na wanawake na kuyafanya
maisha yako rahisi. Kama kumtoa mwanamke date sahizi ni jambo gumu
kwako, basi unafaa kujua kuwa hilo halifai kuwa tatizo lako kamwe tena.
Hii hapa ndio njia rahisi ya kuongea na mwanamke ambayo itakusaidia kupata ujuzi kadri muda unaposongea.
1. Usijaze mazungumzo yenu na kwa kumsifu saana.
Kuna makumi ya wanaume katika nyanja hii ambao wanapenda sana kutumia
maneno ya kumsifu mwanamke kama wameishiwa na maneno wakati wanapoongea
na mwanamke. Wanaume wengine hufanya hivyo ili kudhihirisha kwa mwanamke
kuwa wamevutiwa nao. Lakini makosa ni kuwa, kutumia maneno ya kumsifu
mwanamke hayaongezi sana wala hayafanyi mengi kumsaidia mwanamke. Kwa
hivyo, weka maneno ya kusifu kando, na uanze kuongea mambo mengine
ambayo yatamvutia pia. Kama hutafanya lolote kando na kumwambia kuwa
umemzimia kwa urembo wake au macho yake, utakuwa umejiweka level moja na
wanaume wengine ambao wanatumia mitindo io kwa hio.
Kumbuka: wewe unawezekana kuwa si mwanaume wa kwanza ambaye umevutiwa
naye. Mwanzo, kuna uwezekano mkubwa kuwa wanaume wote wanamuona yeye
anavutia. Hii inamaanisha kuwa kumsifu wewe kwake haitakuwa jambo geni
kwake.
2. Usijikite sana kuonyesha ya kuwa unamwona yeye anavutia
Kusistiza, ni kuwa haufai kuweka akili yako ijikite kuwa unamwona
mwanamke unayeongea naye anavutia kupindukia. Ukijisahau tu ukianza
kumfikiria vile ana urembo na kuvutia, utakuwa unajipa presha ambayo
haitakuwa na manufaa yeyote kwa mazungumzo yenu. Kuna njia rahisi ya
kuepuka jambo hili, ni kuwa unafaa kuidanganya akili yako kuwa huyo
mwanamke unayeongea naye hana urembo wowote ule. Presha ikishuka katika
mwili wako, utajiona umepata fursa rahisi ya kuweza kujieleza ukiwa
pamoja na mwanamke yeyote yule. 3. Tafuta mambo ambayo munagawa kimaisha
Ok, haitakuwa jambo gumu vile mkianza kuongea mambo ambayo mnagawa ama
intrest ambazo mnashare. Mwanzo kama mtaanza kuongea mambo ambayo
mnagawa katika maisha, itakuwa ni njia rahisi ya wewe kuweza kupata
namba yake ya simu ili kuweza kumshawishi kumtoa date.
Kumbuka: mwanamke akigundua kuwa mnashare intrest pamoja, hapo hapo
atataka kuutumia muda wake zaidi mkiwa pamoja ili mpate kuzungumza
intrest mnazoshare. Hivyo basi, fanya utafiti wa kina na ujaribu
kuvumbua jinsi na njia utakayoitumia ili muweze kujumuika pamoja
No comments:
Post a Comment