Kama kuna sehemu moja hapa duniani ambayo unaweza kujiachilia na kuwa
wewe mwenyewe na kupata wanawake wakupende, bila shaka hio sehemu ni
mtandaoni.
Hii ndio sababu kuu ya wanaume wengi kujiingiza katika Internet ili
kujaribu mizare yao ya kuwavutia na kuwashawishi wanawake sikuhizi.
Habari njema ni kwamba wanaume wengi hufanikiwa
katika azma yao. Kuingia katika mitandao ya kijamii na kujaribu
kuwashawishi wanawake inaweza kuwa jambo gumu kiasi na wakati mwingine
likawa ni rahisi. Wengine hutumia fursa ya kutumia mitandao kama mazoezi
ya washawishi mademu huku wengine wakifanikiwa kupata wachumba ambao
wanakuwa nao katika maisha yao ya kawaida. Well, kama hujawahi kutongoza
mwanamke online, ama unapata vigumu kutongoza then hapo chini kuna
mbinu mwafaka ambayo itakuwezesha wewe kumtongoza yeyote yule katika
mitandao ya kijamii kiurahisi.
1. Mtongoze
Kama maisha ya kawaida, kumtongoza mwanamke akiwa online ni lazima kama
ibada. Itakuwa bora zaidi ukichanganya mitindo spesho ya kutongoza mara
kwa mara, Mnyeshee kwa kumsifu siku moja halafu unakuwa mfidhuli siku
nyingine. Jambo muhimu hapa ni utambue kuwa lazima unafaa kumfanya awe
ametulia wakati unapochat nayeye. Pia lazima awe anajiskie yuko huru
kabisa wakati mnapoongea. Hii itahakikisha kuwa anapenda na kufurahia
kutaka kukujua zaidi na labda siku moja atatamani muweze kukutana ana
kwa ana.
2. Tafuta maneno ya kwako
Usithubutu kutafuta mistari ya papo kwa papo kwani kawaida haifaulu
katika mitandao. Kile unachohitajika kufanya ni kuhakikisha umepanga
conversation yenu vizuri ili isiweze kukwama mbeleni. Pia hakikisha kuwa
unaingiza maneno ambayo yataleta hisia za kucheka na furaha. Hii
itamfanya amakinike zaidi na wewe.
3. Mfanye Acheke
Ok najua si kila mtu ana talanta ya kumfanya mwanamke yeyote acheke kama
vile mzee Majuto lakini unafaa angalau utumie maujanja uliozaliwa nayo
ili kumfanya mwanamke acheke. Nasema hivi kwa sababu wanawake wengi
kawaida hupenda wanaume wacheshi. Ukitumia mbinu hii utamfanya akiwa
offline ama online, fikra zake zitakuwa kwako.
4. Usimwambie kila kitu chako
Ukiwa unachat na mwanamke online, hakikisha humwambii kila kitu chako
kwa wakati mmoja. Hakikisha ya kuwa kama mnachat unamfungulia moyo wako
pole pole. Hii itamfanya yeye kuwa na shauku ya kutaka kukujua zaidi.
Ukiweka baadhi za siri zako kikapuni, lazma ataingiwa na tamaa ya
maswali hivyo kutaka kuongea na wewe zaidi na zaidi.
5. Kutana na yeye uso kwa uso.
Mwisho wa siku -baada ya kumtongoza na kumjua nje na ndani -unafaa
kumuuliza kama atatoka out na wewe. Kumbuka hii ni level nyingine kubwa
sana katika chat ya online hivyo kabla hujamuagiza mukutane uso kwa uso,
lazima ujipange vilivyo.
No comments:
Post a Comment