Hili ni swala tata sana kwa wale ambao hawajakuwa na ustadi mkuu wa
kuwaelewa wanawake na kila wakati wanashindwa kuelewa kama imetimia ule
wakati wa kumtoa date mwanamke au la. Wanaume wengi wanabakiwa na
maswali mengi wakijiuliza kama wanapendwa au la. Ok hapa umefika kwa
nesi mwenyewe. Nitakuonyesha dalili zote za haraka kukuonyesha kama
kweli yule mwanadada unayemzimia, yule ambaye unaongea naye kila wakati
anakupenda au la.
Onyo: hata kama unaconfidence kiasi gani, usiwahi kuthubutu kumuuliza
mwanamke kama anakupenda sababu utakuwa unajiingiza kwa majanga wewe
mwenyewe. Hapo chini nimeweka orodha ya dalili ya kuonyesha kuwa yule
mwanamke anakuzimia.
1. Anapenda kushika nywele zake
Dalili moja ambayo wanawake hufanya bila wao kutambua kama wamemzimia
mwanamume ni pale ambapo anakuwa anashika nywele zake ama kupitisha
mkono wake kwa nywele zake bila kwa maksudi yeyote. Hii humfanya
kuonekana mrembo zaidi na pia kumpa confidence ya kujitambua yeye
mwenyewe. So kama mwanamke unamzimia kila wakati ukiwa na yeye anapenda
kufanya huu mtindo basi fahamu kuwa hii ni dalili dhahiri.
2. Anapenda kutaka kuskiliza kila neno ambalo utaongea
Wanawake wanapenda kujiunganisha kimwili na kihisia. So ukiona kuwa
anapenda kukuuliza maswali kukuhusu halafu anakuwa makini kwa kila kitu
unachoongea, basi fahamu ya kwamba huyo mwanamke amekuzimia na angetaka
kukufahamu zaidi na zaidi. Pia kama anakupenda, ile mizaha yako yote
hata kama ni ile ya kijinga utamwona akicheka tu. Hii ni ishara ya wazi
ya kuwa umegonga ndipo. Hakikisha kuwa unaitumia nafasi hii vile
inavyotakikana.
3. Atakupa namba yake ya simu bila tatizo
Kama mwanamke anakupenda, huwa kamawaida anajipendekeza yeye mwenyewe
kwako. Atakurushia kuhusu dalili zote wakati ambapo yuko free au nafasi
ya kuongea na pia atakwambia kuwa angetamani kukutana na wewe wakati
mwingine muwe pamoja. Lakini tatizo ni kuwa kwa wanawake wengi si rahisi
kumwambia mwanamume watoke out pamoja. So ijapokuwa mwanamke angetamani
kutoka date ama out na wewe siku moja, atasalia kungojea maisha yake
yote hio siku itimie bila mafanikio. So instead ya kumfanya angojee huu
muda wote, wewe ndio unafaa uchukue hatua hio na kumwambia wazi kuwa
umemzimia na unataka kutoka naye date ama kumtoa out kiasi.
4. Anamaintain eye contact na wewe, yaani muda wake wote atakuwa akikuangalia machoni mnapoongea
Kukuangalia macho ni ishara kuu ya kuonyesha kuwa mwanamke amekuzimia.
Kama kila wakati unapoongea na mwanamke atakuwa akikuangalia macho yako
kwa umakini bila kuangalia pengine ni ishara kuwa anakupenda. Hii
inamaanisha kuwa utakuwa umeiteka hisia yake na angetamani kukujua wewe
mwenyewe binafsi zaidi.
5. Anapenda kusimama kando yako
Wanawake wanapenda kusimama karibu na wanaume wanaowapenda kwa sababu
inawafanya wao kujiskia huru na kuwa bila wasiwasi. Wakati wowote
mwanamke anaposimama kando yako hii kwa urahisi inamaanisha anajiskia
yuko salama na huru akiwa na wewe. Hii ni ishara tosha ya kuonyesha kuwa
mwanamke kama huyo amekuzimia kwani pia inatambulika ya kuwa wanawake
hawapendi kukaa karibu na wanaume ambao wanawachukia na wasiowapenda.
6. Anatafuta sababu ya kukushika
Wanawake wanapenda kuonyesha hisia zao na dhamira zao kwa jinsia ya
wanaume kwa kutumia mtindo wa kuwashika mkono na viganja vyao.
7. Anakusuka
Ukiona mwanamke anapenda sana kuongea na wewe kwa mitindo ambayo
anajaribu kwa njia zozote kukufurahisha na ujiskie kumtamani ni dalili
tosha kuwa anakuzimia. Anaweza kutumia maneno ya kukuchanganya akili ili
mradi ucheke ama ufurahie. Hii kwa kawaida huwa anajaribu
kujiunganisha na wewe na ni dalili kuonyesha kuwa amekuzimia.
KUMBUKA: Ni muhimu kufahamu kuwa si lazima mwanamke aonyeshe dalili zote
hapo juu tulizoziorodhesha ili uweze kudhihirisha kuwa yule anakupenda.
Dalili mbili ama tatu hivi ni ishara tosha. Halafu ufahamu kuwa
mwanamke yeyote anaweza kuonyesha baadhi ya dalili hizi so haimaanishi
kuwa ukiingia kwa basi la abiria halafu mwanamke akusongelee karibu yako
inamaanisha kuwa amekuzimia.
No comments:
Post a Comment