Wanaume wengi hubaki kujiuliza ni vitu gani ambavyo wanawake hupenda
-lakini kila wakati wanapokea majibu tofauti tofauti yasiyokuwa na
mwisho. Kadiri wakati unapobadilika, wanawake pia hubadilika. Na
kuongezea ni kuwa kila mwanamke analadha yake tofauti
na mwingine...so kiufupi wanawake huwa tofauti na wengine na hauwezi
kusema wanawake wote huwa wanatafuta kitu kimoja kutoka kwa mwanamume.
Lakini kama kawa, hatuwezi kukosa vitu ambavyo vinapatikana katika
wanawake wote. Wanawake kwa kawaida wana tabia flani ambayo hupatikana
kwa kila mmoja wao. Najua mpenzi wako labda unataka kumpenda ukiwa
naturally...yaani vile ulivyo kitabia. Lakini kuna mambo mengine ambayo
mwanamke angependa uwe nayo ambayo kwa sasa huna so ni lazima ukazani
ili uwe na baadhi ya tabia hizo. Na kama uko nazo basi wewe ni miongoni
mwa wanaume ambao wanapigiwa upato na wanawake wengi. Cheki list yenyewe
ya tabia ambazo mwanamke yeyote angependa kumwona mwanamume akiwa nazo.
1. Kuwa gentleman ama mwanamume thabiti
Wanawake siku hizi wamekuwa wa kisasa, lakini bado wangependa kuwa na
mwanamume ambaye anawafungulia milango, wanawaletea saprize mara kwa
mara nakadhalika. Pia wanapenda mwanamume ambaye ni mkarimu na ambaye ni
mpole. So kama wewe unatabia za ugentleman, basi una nafasi kubwa ya
kumridhisha mwanamke yeyote. Na kama huna hizo tabia basi kazi ni
kwako.
2. Kuwa mtu mwenye hisia na mambo ya kwake
Kama tulivyotangulia kueleza hapo juu ni kuwa mwanamke anapenda mtu
mwenye tabia za kigentleman, so kama wataka kuyeyusha moyo wa mwanamke
ni kuhakikisha kuwa unapenda kumfanyia saprize mara kwa mara huku
ukimuonyesha ukarimu wako kwake. Hii itasaidia kumfurahisha na kutimiza
ndoto zake. Kumfanya kuwa special ni dhahiri kuwa utamfanya akupende
zaidi na zaidi.
3. Kuwa na tabia za utu uzima
Kulingana na utafiti ni kuwa wanawake wengi hupenda kudate na wanaume
ambao ni wakubwa kuwaliko. So kama wewe unajiona unatabia za utuuzima na
hauna mambo ya kifala basi bila shaka utatimiza ndoto yako na kuwa na
yule umpendaye.
4. Kujiamini
Mwanamume ambaye anajiamini kuwa yeye ni yeye bila kujishuku ana nafasi
kubwa ya kuteka hisia za mwanamke yeyote. Kujiamini hakumaanishi
kutojali na mambo yeyote bali kujiamini kinafsia. Mwanamume anayejiamini
anaweza kukabiliana na matatizo yeyote ambayo yanaweza kumkumba
maishani mwake. So hio ni rahisi kwa mmoja kuiteka hisia a mwanamke
kiurahisi.
5. Kuwa na uwezo wa kumshughulikia
Wanawake wanafikiria maisha ya mbele, yaani maisha ya usoni mkiwa nyote
wawili. So mwanamume ambaye anaonyesha dalili za kuwa anajielewa na ana
uwezo wa kumtunza yeye kifedha maishani basi ana nafasi kubwa ya
kumnasua mwanamke kiurahisi. Ujue kwamba hii haimaanishi kuwa lazima uwe
tajiri kuweza kutimiza ndoto yako bali kile unachohitajika ni kumsaida
kadri unavyoweza wewe na usipitishe kiwango ambacho kinaweza kukuathiri
kisaikolojia.
6.Uwe nadhifu
Ingawa kuwa nadhifu haichangii sana kumfurahisha mwanamke kama ilivyo
kwa wanaume, bado hii ni baadhi ya vitu ambavyo mwanamke angependa
kuviona kwa mwanamume yeyote. So kufanya akupende lazima uhakikishe
umetia bidii fulani katika sekta hio.
Sasa, hata kama kuna tabia flani hapa tulizozieleza ambazo hazifanani na
wewe kabisa, haina haja ya kujistikia vibaya. Ili mradi una nia ya
kujifundisha kuwa na tabia kama hizi ama unauhakika kuwa mbeleni utakuwa
na tabia kama hizi, basi wewe una nafasi kubwa zaidi ya kukufanya
kupendwa na wanawake ambao wako wengi wanatafuta wanaume ambao wanatabia
kama hizi.
No comments:
Post a Comment