Kuweza kujiamini kwa mwamume ni jambo muhimu katika huu ulimwengu ambapo
kunatofautisha kati ya mwanamume thabiti na wale feki. Kila mwanamume
anajaribu kuimarisha kujiamini kwake katika huu ulimwengu. Lakini
ushawahi kujiuliza ni mbinu gani unazofaa kutumia ili
uongeze ama kuimarisha kujiamini kwako? Wengi wasiojua mbinu za kutumia
kuwa na confidence wanabakiwa na kutumia mbinu ambazo mwishowe
zinawaweka katika hali ambayo inakuwa aibu kwao.
Tukiongea kuhusu maswala ya kujiamini, wanaume wengi kujiamini kwao mara
nyingi hutumika wakati ambapo anajaribu kumtongoza mwanamke fulani ama
wakati ambapo anajaribu kumridhisha mpenzi wake ili azidi kumpenda zaidi
na zaidi.
Well, kwa wanaume, kuna wale ambao wanajiamini na kuna wale ambao bado
kujiamini ama kuwa na confidence kwa mwanamke ni tatizo.Labda kuna
mwanamke ambaye ushawahi kujaribu kumtongoza halafu baada ya siku ama
madakila ya kuongea naye anakupuuza ama anakudhalilisha mbele ya
marafiki zako. Usikate tamaa kwani bado una nafasi kubwa ya kujua kosa
lako limetokea na wapi.
1. Jikumbushe kuwa wewe ndiwe wewe
Wanaume wengi wanafanya makosa makuu ya kujidhalilisha kibinafsi. Hii
inatokea pale ambapo mwanamume anapomakinika na mambo ambayo yanamfanya
yeye duni. Maneno ya kujiona kama wewe hufai ama kujiona kuwa mwanamke
unayemfukizia hatapendezwa na tabia zako unafaa kuyatupilia mbali.
Unafaa kumakinika na mambo ambayo yana uzuri kwako. Mfano kujiamini ya
kuwa una kipawa cha kuongea, kuchekesha nk. Kujiamini huku kutamfanya
mwanamke kukudhanimi. So kazi ni kwako, aidha usijiamini mwanamke
akudharau ama ujiamini wanawake wakuandame kama vile kivuli.
2. Usimakinike sana na urembo
Kosa jingine ambalo wanaume wengi wanafanya ni kuwa wanamakinika sana na
urembo wa mwanamke. Ukweli usemwe, ukiwa umezungukwa na wanawake wengi
warembo kwa kawaida inakuwa vigumu kumakinika na yale ambayo unasema.
Hii hutokea kwa sababu ya kufikiria sana urembo wa mwanamke kiasi ya
kuwa unapunguza kujiamini kwako. Kusuluhisha hili tatizo hakikisha ya
kwamba wakati ambapo unapokuwa na mwanamke mrembo yeyote, weka kwa akili
yako kuwa mwanamke huyu ni mbovu na hana lolote na urembo, hii itakupa
wewe uwezo wa kumwona mwanamke unayeongea naye ni wa kawaida hivyo
kukupatia nafasi rahisi ya kuongea naye bila tatizo.
3. Shughulika na maswala mbadala
Wakati mwingi ambapo mwanamume anapokuwa date na mpenzi wake ama
kukutana na mwanamke kwa mara ya kwanza, kitu ambacho anakiweka mbele ni
malengo na madhumuni ya kutaka kitu kutoka kwa mwanamke. Aidha
inawezakuwa anataka namba ya simu, kupewa date nyingine ama kitu tofauti
mbali na haya.
Ok mbona usimakinike utulie uje na mtindo mpya ambao utakufanya uwe na
confidence kwa mwanamke yeyote? Jaribu kuleta maswala ambayo hayalengi
ajenda yako kwa mwanamke ili uweze kupata confidence. Njia hii
inapunguza wasiwasi wako ambao unaweza kuwa nao kwa mwanamke yeyote.
Mwishowe wakati umemzoea itakuwa rahisi kwako kuweza kumwambia chochote
ambacho umekuwa ukitaka kumwambia.
4. Rudiarudia
Wataalamu wengine wangepinga mbinu hii ya kutumia kwa mwanamke wakati wa
maongezi lakini kwa mtizamo flani hii ni njia muruwa ya kutumia wakati
wa kujenga kujiamini kwako kwa mwanamke. Kama una mistari ambayo
umeishika na kwa kawaida unaitumia wakati unapokuwa na mwanamke na
umeshuhudia kuwa inafanya kazi kila wakati, mbona usiitumie tena na tena
kwa mwanamke unayemzimia kwa sasa? Hii kando na kukupatia confidence,
itakupa nafasi ya kuonekana mtulivu na kukuona kama unajua kupanga
maneno yake vile inavyotakikana.
Kujifunza kujenga kujiamini kwako kando na kuwa kutakuwezesha kuweza
kuongea na wanawake kwa urahisi, pia kutakuwezesha wewe mbeleni kuweza
kukabiliana na mambo kadhaa na kufanikiwa maishani.
No comments:
Post a Comment