Ushawahi kujikuta katika hali ambayo
unashindwa kujua utaanza vipi kuongea na mwanamke? Ni mwanamke mzuri
ambaye moyo wako unamtamani lakini akili yako inashindwa kutengeneza
mawazo ya jinsi utakavyoanzisha stori na yeye. Unabakiwa ukimuangalia
akikupita mbele yako, ama mbaya zaidi anakuja kuchukuliwa na wanaume
wasiokuwa na thamani yeyote kwa maisha yake. Unabakia na majutio na
mawazo ya "kama ningeweza kujiamini mbeleni si ningem...." Well, tatizo
hilo halijawahi kutokea kwako pekee bali kwa kila mwanaume wakati flani
katika maisha yake na hatutaki lijitokeze tena mbeleni.
So chanzo cha wewe kutoweza kumtongoza
huyu mwanamke ni kuwa akili yako ilikataa kutoa mazungumzo ambayo
ungeweza kuyatumia kwa huyo mwanamke. Well, waonaje kwa mara moja
tukubaliane na akili yako na tusitumie maongezi kuapproach mwanamke, na
badala yake tutongoze kimya kimya?
Kutongoza kimya kimya ni mbinu rahisi
sana, mwanzo ni rahisi kwa kuwa unapata kujua kama mwanamke anakupenda
au la. So bila kupoteza wakati, hebu tuchambue mpango mzima.
Zama nami!
1. Kwa kutumia macho
Kila mtu anajua nishati inayotokana na
kutumia macho. Macho ni kiungo ambacho wanaume wamebarikiwa nacho na
akikitumia vizuri kinajeuka kama silaha nzito wakati ambapo unaitumia
kwa mwanamke. Ushawahi kujiuliza ni kwa nini wakati mwingine mwanamke
anashikwa na aibu/haya wakati unapomwangalia? Ama je ushawahi kumskia
mwanamke akisema kuwa usimwangalie machoni mwake? Hii ni kwa sababu
macho yanaweza kutumika kuongea maneno ambayo mdomo unaweza kushindwa
kuongea.
Wakati utajipata ukimwangalia mwanamke,
mwangalie machoni halafu utoe tabasamu. Kumuangalia kunaonyesha
unajiamini. Kutabasamu unamwonyesha kuwa wewe ni salama na anaweza
kuongea na wewe. Unaweza kusoma chapisho letu la awali ambalo
linafafanua mbinu ya kutumia macho kuapproach mwanamke kwa kina.
2. Mfanye akugundue kupitia kutangamana kwako
Njia nzuri ya kusimama ili wanawake
waweze kukutambua ni kupitia utangamano wako na wengine. Kujizunguka na
wanawake wengi (haswa wale warembo) kutaashiria ya kuwa wewe ni aina ya
mwanaume ambaye wanawake wanapenda kuwa naye. Hii itawafanya wanawake
wengine katika hio sehemu kuwa na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani
ambacho kinakufanya wanawake wapende kuwa na wewe. Hii automatically
itawafanya wanawake kuwa na umbea kukuhusu, kuvutiwa kwako, na hata
kuingiwa na wivu wa kwa nini haujawaingiza katika kundi lako.
Mbinu hii ni moja wapo ya sosholojia ya
wanawake, kimaumbile wanawake hupenda vitu ambavyo wanawake wengine
hupenda. Hivyo kama wewe unamtaka mwanamke flani na hutaki kutumia
maongezi, anza kutangamana na marafiki wake wote isipokuwa yeye,
mwishowe utamwona akijileta yeye mwenyewe, tena ujitayarishe na mapema
kwa kuwa atakuja na presha ambayo kama hukujipanga vizuri inaweza
ikakulemea.
3. Matumizi ya banta bila kuongea
Banta ni mbinu ya kuonyesha ucheshi,
mchezo na mzaha wakati wa kuongea na mtu. Mbinu hii pia inaweza
kutimizwa bila kutumia mazungumzo ili umfanye mwanamke aweze kuvutiwa
kwako.
Kwa mfano, kama ulishatumia mbinu ya
macho kuwasiliana na mwanamke na unataka kuendeleza shughli kwa kutumia
banta, njia rahisi ni kumuonyesha nyuso za ucheshi. Jifurahishe na uwe
mcheshi - toa ulimi wako nje - pinda macho yako - weka uso wowote ule wa
kipuzi ambao unajiskia. Hii ni njia rahisi ya kumfanya mwanamke
atabasamu akiwa mbali, na itakuwa rahisi kwako kumuapproach na kuendea
na yeye iwapo ataonyesha dalili za kupendezwa na wewe.
4. Mvutie na mwonekano wako
Ukitaka kumvutia mwanamke kiurahisi basi
ni muhimu kubadilisha mwonekano wako. Mbinu hii tuliieleza kwa kina
katika chapisho la jinsi ya kubadilisha mwonekano wako uwavutie
wanawake. Kwa kawaida, wanawake wanapenda kushufu wanaume ambao
wanavalia kinadhifu.
Lakini hapa usichukulie makosa.
Kubadilisha mwonekano hakumaanishi ya kuwa unapaswa kuvalia nguo ghali
ama za thamani ya juu. La hasha. Kubadilisha mwonekano kunamaanisha
kuvalia nguo safi, nadhifu na ambazo zinaashiria hulka yako. Usijitese
kuvalia nguo ambazo haziwiani na wewe kwani kwa mwanamke ni rahisi
kukugundua kama umejeuka mwigo.
5. Ishara ya mwili wako
Wanawake wanaweza kujua mengi kukuhusu
kwa kuangalia miondoko yako ya mwili pekee. Kama unataka kuonyesha
ujiaminifu ambao utamfanya mwanamke akutambue, basi ni lazima mwili wako
uonekana vile unapaswa kuonekana.
Kuonyesha confidence katika mwili wako unapaswa kufanya yafuatayo:
i) Simama wima - mwanaume thabiti
akisimama anakuwa hivi; masikio yako yawe nyuma ya mabega yako, mabega
yako yawe nyuma ya kiuno chako, kiuno chako kiwe nyuma ya kiwiko chako.
ii) Kaa kwa kujitanua - wakati umekaa
katika kiti, hakikisha ya kuwa unachukua nafasi yote ambayo unaweza
kuitimia. Egemea kwa kiti, itanue miguu na mikono yako, kichwa kiweke
kiangalie juu.
iii) Jinsi unavyokaa - Usisogee sogee
kama huna sababu zozote, usikunje miguu wala mikono, usiangalie chini,
usijikune kichwa ama kutafuna tafuna.
iv) Unavyotembea - Tembea na sababu, tembea kwa kujiamini, tembea na njia thabiti.
Kuweza kukontrol mwili wako inakusaidia kuonekana mtu mwenye nguvu, wa kujiamini ambaye anapendwa na wanawake.
6. Kuwa na hadhi ya juu
Mpaka sasa hili chapisho linaongea
kuhusiana na kuwasiliana na mwanamke bila kuongea naye. So iwapo unataka
mwanamke akunotice, wakati mwingine inahitajika kuwa na jitihada za
ziada. Kukaa sehemu moja kungojea mwanamke akugundue haitakuwa ya fanaka
kama vile ambavyo utaamka na kujifanya uonekane wewe mwenyewe.
So utafanyaje mpaka mwanamke akunotice?
Tangamana na marafiki, jamiiana na kila
mtu ambaye unamjua. Wakati umetoka matembezi au sehemu yako ya
kujivinjari, ongea na kila mtu - wanaume, wanawake, wateja, wafanya kazi
nk. Wanawake watauona uwezo wako wa kutangamana na kila mtu na watakuwa
na interest ya kuongea na wewe. Ziada ni kuwa utakuwa unaonyesha
ujiaminifu, urafiki, na uko na uwezo wa kujicontrol katika jamii - tabia
zote ambazo wanawake wanaziona nzuri katika mwanaume.
7. Wafanye wanawake wakufukuzie
Kufanya wanawake wakufukuzie inaweza
kuwa rahisi sana. Kile ambacho unahitajika ni kutoka nje umakinike na
kujifurahisha muda wote. Weka tabasamu katika uso wako na ujiinjoy wewe
mwenyewe. Hii itamfanya mwanamke kukunotice na kutamani kuungana na wewe
ili muinjoy pamoja.
No comments:
Post a Comment