Kutongoza ni sanaa ambayo inahitaji mmoja kufanya mazoezi ya mara kwa
mara ili aweze kuwa na ustadi ambao unaweza kumnufaisha au kumsaidia
mhusika wakati ambapo anakabiliwa na tatizo la kumshawishi mwanamke.
Ijapokuwa kuzijua sanaa hizi dhidi ya wanawake haitaonekana kuwa na
ustaarabu katika jamii, kila mwanaume ana haki ya kuzijua na kutambua
mbinu hizi.
Kitu cha kwanza ambacho unapaswa kujua ni kuwa kutongoza si matumizi ya
mistari na miondoko ya mwili pekee bali pia ni subira. Kutongoza
mwanamke kutachukua muda mwingi kutoka kwako hivyo unahitajika kuwa na
imani. Kwa mfano kabla ya kuchukua hatua ya kuapproach mwanamke lazima
upime manufaa na hasara ambazo zitakuja iwapo utaamua kutangamana na
mwanamke ambae unakusudia kuwa naye.
Ikija swala la kumtongoza mwanamke katika kikundi cha watu, haya hapa ni
baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuwa nayo wakati unapokabiliana na
windo lako.
#1 Kumsifia
Kama umetoka out hadi kwa klabu na marafiki zako halafu ukamwona
mwanamke unayemtamani akiwa katika kikundi, muapproach na umuagizie
kinywaji na uwe mkweli na mhakika wakati unapomsifia kuhusu umbo lake na
nguo alizovalia. Weka katika akili yako kuwa mwanamke anapenda kusifiwa
kwa nguo alizovaa, hairstyle yake, macho yake, ucheshi wake na pia
marashi aliyoyapaka. Pia, hakikisha kuwa unaspend muda mwingi zaidi hata
kama klabu inaenda kufungwa. Kama umeongea na mwanamke huyu usiku huo,
hakikisha kuwa unamwambia kuwa umependezwa na kuspend muda na yeye.
#2 Jiamini
Confidence ni nguzo ya kila mwanaume ambayo anapaswa kuwa nayo wakati
wowote ule. Mwanaume anayejiamini anatambulika haraka na wanawake. Hivyo
lazima uwe na confidence wakati unapotangamana na wanawake. Hii
inamaanisha kuwa lazima uonyeshe confidence mbele ya umati na pia
uonyeshe kuwa una interest na yeye hata kama umezungukwa na watu.
Confidence ni lazima kama unataka kumtongoza mwanamke. Usifikirie sana
kuhusu jinsi utakavyompendeza kwa sasa lakini. Kwa kujionyesha wewe
mwenyewe bila kujifanya mtu mwingine kutakusaidia zaidi kuliko kuwa
muigo wa mtu mwingine ili uonekane mzuri.
#3 Kujieleza
Wakati unapomtongoza mwanamke katika umati, ni bora zaidi kuweka toni ya
sauti yako chini na ambayo itavutia kadri uwezavyo. Hii haimaanishi
kuwa unapaswa kumnong’onezea, la. Kile unachopaswa ni kuweka wazi sauti
yako aisikie vizuri na mara kwa mara umuonyeshe tabasamu ambalo
utalichanganya na mvutio wa macho yako. Pia wakati unapoongea onyesha
ujuba na maneno unayoyatamka. Hii itamfanya akuone kuwa wewe una
interest kwake na unataka kuendeleza aproach yako zaidi.
Wakati utakapokuwa umeuchukua muda wako kuongea na mwanamke na
kumuonyesha kuwa uko interested na yeye, jaribu kutafuta ishara ambazo
zinaonyesha kuwa pia yeye amevutiwa ama anahisi kama vile unahisi wewe.
Ishara hizi utaziangalia kupitia miondoko ya mwili wake. Je anapinda
mwili wake upande wako? Je kifua chake amekienua ili uone ukubwa wa
matiti yake? Je anacheka mizaha yako hata kama haichekeshi? Kama umeona
kuwa amevutiwa na wewe kupitia ishara hizi, basi rudi nyuma na umngojee
yeye aanze kuchukua hatua. Hii ni njia hakika ya kumfanya amaintain
interest na wewe.
No comments:
Post a Comment