Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujit-okeza kama
viuvimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata
mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi
vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.
Karibu asilimia
85 ya vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya
asilimia 20 ya wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi
wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na
watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.
Chunusi ni
ugonjwa unaoathiri vifuko au glandi za ngozi.Katika ngozi ya binadamu kuna
glandi ziitwazo Sebaceous ambazo zipo chini ya ngozi na kazi yake kubwa ni
kutoa mafutamafuta yaitwayo Sebum ambayo hu-saidia kuiweka ngozi kuwa nyevu na
yenye mvuto.
Wakati wa balehe mwili wa binadamu hutoa Sebum kwa
wingi na kwa sababu wakati huu vikemikali vya mwili yaani sex hormones hutolewa
kwa wingi hasa hormone ya kiume iitwayo androgen husababisha utoaji wa sebum
kuwa mwingi zaidi kuliko kawaida. Sebum inapotolewa kwa wingi huungana na seli
za ngozi zilizo-kufa na kutengeneza mchanganyiko mzito kama nta uitwao comedo
ambao huziba vishimo vya kutolea joto.
Maambukizi zaidi hutokea pale ambapo
vijidudu yaani baktaria vinaposhambulia vishimo vilivyoziba hapo kivimbe
ambacho watu wengine huita Pimple hujitokeza pale ambapo Sebum, bacteria, seli
za ngozi na seli nyeupe za damu zinapo-changanyika na kujikusanya katika
vishimo vya jasho vilivyoziba na eneo husika hupata vivimbe au vipele ambavyo
tunaviita chunusi.
Ukubwa wa
kipele hutegemea ngozi ya mtu au kiasi cha mchanganyiko nilioeleza hapo juu
katika eneo husika.Vipele vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati
mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za
ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.
Ngozi mpya
hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha
mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka.
Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni kwa sababu maeneo
hayo yana vifuko au glandi za Sebaceous nyingi.
CHANZO CHA CHUNUSI
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo
baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
1. UMRI – Kama nilivyosema hor-mone/vikemikali
hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubale-he.Kemikali hizi huongeza
utengenezaji wa nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
2. VIPODOZI –Baadhi ya vipodozi kama Make-up za kina
dada na Sprays za ny-wele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa
nyingi zaidi.
3. CHAKULA- Chunusi hazisababishwi na chakula bali
baadhi ya vyakula hufan-ya chunusi kuwa nyingi zaidi.
4. DAWA-Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na
kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,steroids
na tranquilizers.Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo
wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na ma-kusudio ili kuongeza unene
wa misuli yao.
5. MAGONJWA- Magonjwa yatokanayo na matatizo katika
vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa
wasichana.
6. MAZINGIRA- Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa
unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa
katika mazingira ya joto huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi.
7. JINSIA-Wavulana hupata sana chunusi kuliko
wasichana.
8. FAMILIA- Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana
kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
9. HOMONI- Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati
mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa
hupelekea kupata chunusi.
10.
USAFI WA MWILI-
Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au
vipele hu-sababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwi-lini
au kutooga huongeza uwezekanifu wa kupata chunusi
11. MAWAZO AU STRESS-Mtu anapokuwa na mawazo mengi
vimkemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huwe-za kuchangia au kusababisha
chunusi
DALILI ZA CHUNUSI
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine
husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza
kujitokeza kama baka dogo na wakati mwingine mtu anaweza utambuzi wa chunusi
unaweza kuwa mgumu kutokana na watu walivyomakini au wanavyojenga wasiwasi
kubwa katika mwonekano wao hasa usoni.Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa
chunusi ni rahisi sana
Daktari kuzigundua, japokuwa katika familia zetu ni
mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi
kwa sababu ya chunusi.Pale inavyotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya
zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu chakula, ngozi,
dawa unazotumia na vitu vingine vinavyowe-za.kuchangia mtu kupata chunusi
MATIBABU
Matibabu ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji
wa anta (sebamu ), kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani
bacteria.
Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingia au
ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha
chunusi kama nilivyoeleza hapo juu.
DAWA ZA KUPAKA
Kuna dawa za kupaka ambazo hupaka katika eneo la
ngozi lililoathirika kwa chunusi. Dawa hizi hupatikana kama cream,lotion,gel au
pad.
Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko
katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu. Mojawapo ya dawa
hizi ni antibi-otic kama zenye mchanganyiko wa gentamyicin na betamethasone au
dexame-thasone kama vile Gentrisone au Gentriderm cream,Erythromycin,B-Tex na
kadhalika.Pia Persol forte Gel husaidia hasa ukianza na asilimia ndogo (2.5%)
na kuen-delea kadri ngozi yako inavyohimili dawa. Gentamycin huua wadudu
wanaosababisha chunusi wakati dawa nyingine huondoa mwasho.
Dawa nyingine ni zile zinzolainisha nta au
Comedolytics na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza
kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara
mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya
kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua
wiki kadhaa.
DAWAZA KUMEZA
Wakati mwingine daktari anaweza kumshauri mgonjwa
kutumia dawa za kumeza kulingana na wingi au ukubwa wa tatizo.
Dawa kama antibiotics huua wadudu na huzuia chunusi
,dawa hizo ni kama vile Erythromycin topical, Accutane (isotret-inoin),
Benzamycin Cleocin T (clindamycin phosphate), Desquam-E (benzoyl peroxide)
Minocin (minocycline hydrochloride) na
”Si vema kujinunulia mwenyewe tu na
kuanza kutumia bila ushauri wa daktari au mtaal-amu wa magonjwa ya ngozi.”
Wanawake wenye chunusi zisizotibika wanaweza kupewa
Anti-androgens kama vile baadhi ya vidonge wa uzazi wa mpango.Chunusi sugu
hutibiwa kwa ciorticosteroids na anti-iflammatory drugs ambazo hutibu chunusi
sugu ambazo huitwa Acne fulminans na hupatikana zaidi kwa vijana.
MATIBABU MENGINE
Kwa nchi zilizoendelea matibabu yanaweza kuwa hata
upasuaji mdogo (skin grafting) au plastic surgery kama chunusi imesaba-bisha
baka kubwa na kuna njia kama vile Chemical peel ambapo kemikali hupakwa kwenye
ngozi na inapokauka kipande au gamba la juu la ngozi huondolewa na kuondoa
baka.
MATIBABU MBADALA
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni
vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika
hali ya ukavu nakuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu wenye chunusi wanashauriwa kulAa mlo kamili
wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi, matunda, mboga za
ma-jani,vitamin B complex na Chromium. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya
pombe,vyakula vya maziwa, tumbaku, sukari, vyakula vilivyoandaliwa viwandani na
vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi
MUHIMU
Chunusi haziwezi kutibika kabisa japokuwa iwapo
matibabu Yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa unatumia dawa
usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu
na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha
mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza
kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na
madhara katika ngozi.
MAMBO YA KUFANYA ILI USIPATE CHUNUSI
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya
yafuatayo;
1. Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa
maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu
,usikwaruze kwa kucha au kitu choichote kigumu.
2. Tumia make-up au vilainisha ngozi visivyo na mafuta
mgando
3. Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba
uso (kwa wenye nywele ndefu)
4. Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta
mengi.
5. Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye
ncha kali.
6. Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri
ili kupata vitamin D
7. Punguza mawazo
No comments:
Post a Comment