Tumia kondom mpya
kila mara unapofanya mapenzi.
Jitahidi kutokugusa sehemu za siri ya mpenzi wako (au osha
mikono yako) kabla ya kugusa sehemu zako za siri.
1. Usiguse sehemu
za siri za mpenzi wako kabla ya kuvaa kondom. Angalia kwa
makini paketi za kondom kabla ya kuifungua.
Hakikisha
haijaharibika au kupasuka.
Angalia tarehe ya mwisho ya matumizi ya kondom hii, ambayo
itakuwa imechapishwa sehemu ya nje ya paketi ya kondom kuhakikisha tarehe
haijafika. Kama tarehe imeishafika na kupita, tumia kondom nyingine.
2. Fungua paketi
kwa uangalifu kwenye sehemu iliyo na makucha makucha kama msumeno, ili
kuhakikisha hauharibu kondom.
Usitumie makucha
au meno kufungua paketi, kwa sababu kondom inaweza kuchanika.
Upapogusa kondom,
iwe na utelezi kidogo. Kama kondom haina utelezi, imeharibika, kwa hiyo
usiitumie. Sehemu ya nje ya kondom huwa na majimaji yanayorahisisha kufanya
mapenzi. Kabla ya kuvaa
kondom kwenye uume, hakikisha unafahamu sehemu gani inakaa nje unapoikunjua.
Tumia kondom mpya
kila mara unapofanya mapenzi.
Usitumie tena kondom iliyokwisha tumika.
3. Weka kondom
kwenye uume uliyosimama tu. Minya chuchu iliopo sehemu ya juu ya kondom kuhakikisha hamna
hewa ndani yake. Hii ni kuhakikisha kuna nafasi ya kutosha katika kondom wakati
mwanaume anamwaga shahawa.
4. Endelea
kuminya chuchu na kunjua kondom kwa uangalifu hadi unapofika sehemu ya chini ya
uume. Kuminya chuchu kunahakikisha kuna nafasi ya kutosha kupokea shahawa
itakayomwagika.
Kama unaweka kondom juu ya uume na unaanza kuikunjua vibaya,
usiitumie tena, kwa sababu ukiigeuza kuna uwezekano kuna tone chache za shahawa
zilizokaa nje ya kondom.
Usitumie
Vaseline, losheni au aina nyingine yeyote ya mafuta kuongeza utelezi wa kondom
zaidi. Mafuta ya aina hii huongeza uwezekano wa kondom kupasuka. Kama unahitaji
utelezi zaidi, tumia mate au majimaji maalum yaitwayo KY-Jelly, yanayopatikana
katika duka ya madawa.
5. Anza kufanya
mapenzi
6. Mara tu baada
ya kufikia mshindo, toa uume ukeni wakati unaendelea kushikilia kondom kwenye
sehemu ya chini ya uume karibu na mapumbu. Kila mara ondoa uume kabla haujalegea kuhakikisha kondom
haiachii na kubaki ndani ya uke.
7. Kwa uangalifu,
vua kondom kutoka kwenye uume.
8. Funga kondom
kwa fundo kwenye sehemu ile ya wazi kuzuia shahawa kumwagika.
9. Funga kondom
kwenye karatasi au kwenye paketi yake ya mwanzo.
10. Tupa kondom
kwenye choo cha shimo, au ichome moto. Nawa mikono yako na maji na sabuni.
TUMIA KONDOM MPYA KILA UNAPOFANYA MAPENZI.
JINSI YA KUTUMIA KONDOM YA KIKE:
Tumia kondom mpya
kila mara unapofanya mapenzi. Kondom ya kike
inaweza kuwekwa ndani ya uke mara tu kabla ya kufanya mapenzi, au hadi masaa 6
kabla ya kufanya mapenzi.
Jitahidi kutokugusa sehemu za siri za mpenzi wako (au osha
mikono yako) kabla ya kugusa sehemu zako za siri.
1. Tazama paketi
ya kondom ambayo bado haijafunguliwa.
Hakikisha
haijaharibika au kupasuka.
Angalia tarehe ya mwisho ya matumizi ya kondom hii, ambayo
itakuwa imechapishwa sehemu ya nje ya paketi ya kondom kuhakikisha tarehe
haijafika. Kama tarehe imeishafika na kupita, tumia kondom nyingine.
2. Fikicha kwa
upole paketi ili kuhakikisha majimaji yaliyomo yanasambaa kote kwenye kondom.
Fungua paketi kwa
uangalifu kwenye sehemu yenye makucha kama msumeno, ili kuhakikisha kondom
haiharibiki.
Usitumie makucha au meno kufungua paketi kwa sababu yanaweza
kuchana kondom.
Unapogusa kondom,
iwe na utelezi kidogo. Kama kondom haina utelezi, imeharibika, kwa hiyo
usiitumie. Sehemu ya nje ya kondom huwa na majimaji yanayo-rahisisha kufanya
mapenzi.
3. Ni rahisi
zaidi kuingiza kondom ukeni kama unachuchumaa, kupandisha mguu mmoja juu ya
kiti, au kulala kitandani ukiwa umekunja magoti wakati umepanua miguu yako wazi
kabisa.
4. Minya kondom
kwa nje, ukiminya sehemu mbili za mviringo mdogo wa ndani kwa pamoja kama
ilivyooneshwa kwenye picha. Muundo huu hurahisisha kuingiza kondom ukeni.
5. Wakati
umeendelea kushikilia sehemu ya nje ya kondom namna hii, pole pole ingiza
mduara mdogo wa ndani ukeni ukitumia kidole cha shahada.
6. Ili
kuhakikisha kondom imekaa vizuri, unaweza kuingiza dole lako la shahada au dole
la kati ndani ya kondom na kusukuma mduara wa ndani mpaka mwisho wa kidole
chako. Hakikisha kutokuharibu kondom na makucha yako.
7. Hakikisha
mduara wa nje wa kondom unaishia kwenye mlango wa uke: usiingie ndani ya uke.
Mduara wa nje utafunika mlango wa uke wakati wa kufanya mapenzi.
8. Usitumie
Vaseline, losheni au aina nyingine yeyote ya mafuta kuongeza utelezi wa kondom
zaidi. Mafuta ya aina hii huongeza uwezekano wa kondom kupasuka. Kama unahitaji
utelezi zaidi, tumia mate au majimaji maalum yaitwayo KY-Jelly, yanayopatikana
katika duka ya madawa.
Fanya mapenzi
ndani ya muda wa masaa 6 baada ya kuvaa kondom.
Tumia mikono yako kuongoza uume ndani ya kondom, ili kuhakikisha
kuwa uume unaingia ndani ya kondom na siyo kando.
9. Baada ya
kufanya mapenzi, viringisha mduara wa nje wa kondom mara moja ili kuzuia
shahawa kumwagika.
Kisha toa kondom ukeni polepole.
10. Funga kondom
kwenye karatasi au kwenye paketi yake ya mwanzo.
11. Tupa kondom
kwenye choo cha shimo, au ichome moto.
Nawa mikono yako na maji na sabuni.
TUMIA KONDOM MPYA KILA UNAPOFANYA MAPENZI
sayi manyanda
manyandahealthy@gmail.com
No comments:
Post a Comment