Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Monday, May 1, 2017

Sababu za kupoteza hamu ya kujamiiana

 
kusababisha msisimko

kupotea kati ya wenza wawili na
hatimaye mwisho ni kupungua
uwezo au hamu ya kujamiana.


Katika utafiti uliofanyika miaka ya
karibuni nchini Marekani,
imebainika kwamba kati ya ndoa
6,000 zilizovunjika, asilimia 57
zimesababishwa na mwenza
mmoja au wote kupenda kuchati
au kutumia intaneti kupita kiasi na
hivyo kusababisha msisimko
kupotea kati ya wenza wawili na
hatimaye mwisho ni kupungua
uwezo au hamu ya kujamiana.


Ni kundi gani la wanawake lililo

katika hatari ya kukumbwa na
tatizo hili?

1. Wanawake ambao wana historia
ya kupungua hamu ya kujamiana

2.  Wale ambao wamefanyiwa
upasuaji wa kuondoa mayai yao
ya uzazi kutokana na sababu
mbalimbali

3. Wanawake waliofika umri wa
kuacha kupata hedhi (miaka
42-58)) na kupata dalili
mbalimbali kama kutokwa na
jasho usiku, kukosa usingizi mzuri
na msongo wa mawazo.

Kwa wanaume, visababishi vya
tatizo la kupungua hamu au
uwezo wa kujamiana ni kama
ifuatavyo;
1. Msongo wa mawazo kama
nilivyoeleza hapo juu. Kupungua
au kukosekana upendo/mapenzi
katika uhusiano/ndoa.

2.  Unywaji pombe kupindukia
kama nilivyoeleza awali.

3. Utumiaji wa dawa za kulevya
4.  Uvutaji sigara - Hupunguza
kiwango na uzito wa mbegu za
kiume.

5 Uzito wa mbegu za kiume
hupungua kwa asilimia 22-57 kwa
wale wanaovuta sigara. Uwezo wa
mbegu za kiume kuogelea
kwenye mirija ya uzazi ya
mwanamke pia nao hupungua
kwa asilimia 20 kwa wale
wanaovuta sigara ikilinganishwa
na wale wanaume wasiovuta
sigara.

Utafiti mwingine umethibitisha
kuwa wanaume wanaovuta sigara
wana asilimia kubwa ya kutoa
mbegu ambazo hazina maumbile
mazuri au ya kawaida na hivyo
kuongeza uwezekano wa mimba
kutoka au kuzaa mtoto mwenye
maumbile ambayo siyo ya
kawaida.
Tafiti mbalimbali pia
zimethibitisha kuwa uvutaji sigara
huharibu mirija ya seminiferous
tubules ambayo hupatikana
kwenye korodani na ni sehemu
ambapo mbegu za kiume
hutengenezwa, hivyo uharibifu
wake hupunguza wingi na uzito
wa mbegu
Pia uvutaji sigara hupunguza
vichocheo aina ya testerone,
growth hormone, na vinginevyo.
Wanaume wenye kiwango kidogo
cha testerone huwa na tatizo la
kupungukiwa uwezo wa
kujamiana na kiwango kidogo cha
mbegu.

Uvutaji sigara hupunguza
mzunguko wa damu unaopita/
kwenda kwenye moyo na kwenye
uume na hivyo basi kumfanya
mwanamume kushindwa
kusimika na kupata tatizo la
kupungua uwezo wa kujamiana.

Katika tafiti zilizofanyika, asilimia
97 ya wale waliogunduliwa na
tatizo hili walikuwa wavutaji
sigara na katika tafiti nyingine
asilimia 87 ya wale wenye tatizo
hili walikuwa pia wavutaji sigara.
Katika utafiti uliowahusisha
wapenzi 290 mwaka 1999,
ilionyesha kwamba wanaume
ambao walikuwa wavutaji sigara
walifanya tendo la ndoa na wake
zao mara 6 tu kwa mwezi mzima
na wale ambao hawakuwa
wavutaji sigara walifanya tendo la
ndoa mara mbili zaidi ya wale
wavutaji sigara.

Uvutaji sigara, huhusishwa pia na
kuongezeka kwa chembechembe
nyeupe za damu kwenye mbegu
za kiume ambazo kwa kawaida
hutolewa kukiwa na ugonjwa
ndani ya mwili.

Chembechembe hizi ambazo
zinakuwapo kwa wingi kwenye
mbegu za kiume pasipo na
kuwapo kwa ugonjwa, hupunguza
uwezo wa mbegu kuingia na
kuungana na yai kutoka kwa
mwanamke na hivyo kusababisha
kutotunga kwa mimba.

1.    Ugonjwa wa kisukari
2. Uzito uliopitiliza unaotokana na
kuongezeka kwa mafuta ambayo
husababisha mishipa ya damu
inayopeleka damu kwenye moyo
na uume kuwa midogo na
kupungua uwezo wa kujamiana.
Kupungua uwezo wa kujamiana au kufanya mapenzi kwa
wanaume ni ishara mojawapo ya
ugonjwa wa moyo na kiharusi. Matatizo ya vichocheo katika
tezi la koo
* Kuwa na wasiwasi.
* Kupenda mitandao ya kijamii
kupita kiasi .
* Umri - Kuanzia miaka ya 40,
kiwango cha kichocheo aina ya
prolactin huongezeka na
kusababisha kuongezeka kwa
kichocheo kingine aina ya
dihydro-testerone ambacho
husababisha tezi dume
kuongezeka na hatimaye
kupunguza uwezo wa kusisimka
kwa mwanamume.
* Madhara katika neva
inayohusika na kusimika kwa
uume
* Kuendesha baiskeli muda mrefu
(kwa kipindi kimoja) - Hii
hugandamiza neva na mishipa ya
damu inayopeleka damu kwenye
uume na kusababisha tatizo la
kupungua kwa nguvu za uume.

manyandahealthy@gmail.com

No comments:

Post a Comment