KWA kawaida mwanaume ana korodani
mbili ambazo zimehifadhiwa katika mfuko maalum wenye tabaka tatu na ndani kuna
kiasi kidogo cha maji kinachozunguka korodani ili kuilinda. Mwanaume endapo
atakuwa na korodani moja ni tatizo na pia akiwa hana kabisa korodani ni tatizo
kubwa. Kazi ya korodani ni kuzalisha mbegu za kiume, mwanaume anaweza kuwa na
korodani zote mbili lakini akashindwa kuzalisha mbegu za uzazi kutokana na
matatizo mbalimbali.
Mwanaume mwenye korodani moja
anaweza kuzalisha mbegu au asizalishe kabisa, kitu cha msingi akapimwe
hospitali kuona
uwezo wa hiyo moja. Mwanaume ambaye
hana korodani kabisa hawezi kuzalisha mbegu za uzazi hivyo hana uwezo
wa kumpa mimba mwanamke. Tatizo la
kuwa na korodani moja au kukosa kabisa tutakuja kuliona katika makala zijazo.
JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA
Maumivu ya korodani hutokea katika
korodani au haswa moja au zote mbili endapo zitaumizwa kwa kuumia au
maambukizi. Maambukizi haya yanaweza kuwa makali na ya muda mfupi,yanakuwa
makali kwa muda fulani halafu yanapoa yenyewe au kwa dawa baadaye yanarudi tena
yakiwa makali sana kama mwanzo au pia huwa sugu yaani unakuwa na maumivu ambayo
siyo makali ila ni ya muda mrefu na yanayokunyima raha.
Maumivu ya korodani yanaweza kuwa
makali kiasi kwamba yatahitajika matibabu ya dharura mfano korodani inavimba
kama jipu kubwa, ikiambatana na maumivu makali na homa, tatizo hili kitaalam
huitwa ‘Fournier’s gangrene’ au inatamkwa ‘Fonias gangrini’.
Vilevile inaweza kutokea korodani
ikajinyonga yenyewe na kusababisha ukapata maumivu makali ya ghafla
yanayoelekea hadi tumboni, tatizo hili linaitwa ‘Testicular Torsion’. Matatizo
haya kwa ujumla wake tutakuja kuyaona katika makala zijazo.
CHANZO CHA TATIZO
Maumivu ya korodani yana vyanzo
mbalimbali, lakini maumivu sugu ni yale yanayochukua takriban zaidi ya miezi
mitatu. Maumivu makali na ya ghafla
huwa hayavumiliki na huwa na tiba ya
dharura. Maumivu haya sugu huwa kwa kipindi fulani hasa kwa wanaume ambao
wametoka kufunga uzazi ‘Vesectomy’ lakini baadaye hupoa. Vilevile husababishwa
na maambukizi katika korodani na kusababisha magonjwa kama Epididymits,
Prostatis na Orchitis ambayo yote ni maradhi ya viungo vya uzazi vya mwanaume
na husababisha ugumba.
Tutakuja kuona katika matoleo
yajayo. Vilevile korodani inaweza kuwa na vivimbe kwa ndani,pembeni au juu ya
kokwa au kuizunguka. Uvimbe au vivimbe hivi vinaweza kuwa na mishipa ya damu
iliyojikunja humo, kujaa maji isivyo kawaida, mbegu za kiume kujikusanya na
kushindwa kutoka na mengine ya kitaalam ambayo pia tutakuja kuyaona.
Yote haya humsababishia mwanaume
ugumba. Maumivu pia husababishwa na kuumia korodani au baada ya kufanyiwa
upasuaji kama tulivyokwishaona hapo awali. Maumivu yatokanayo na korodani au
kende kujinyonga huwa makali sana na korodani zikiguswa
huuma sana na kawaida huendelea
hivyo kwa masaa yasiyozidi sita.
Unapoona dalili kama hizo wahi
kamuone daktari kwa ajiri ya uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment