Kuna watu utakuta mume au mke akiweka
simu tu chini wanaanza kuchunguza, kuangalia sms, wakikosa waaangalia
simu zilizopigwa na wakiokosa huanza kuchambua majina ya jinsia tofauti
yaliyopo katika simu za wapenzi wao.
Lakini hawaishii hapo, wakimuona tu
mwenza na mtu wa jinsia tofauti hunza kupaniki na kutafuta namna ya
kumfumania. Wewe endelea tu kutafuta na kumfuatilia, utapata
unachokitaka, lakini swali linakuja ukishapata?
Unapomfumania mwenza wako unakuwa
umejithibitishia kua hauko peke yako, utataka kuombwa msamaha na kutaka
mwenza wako abadilike? Lakini hembu kabla hujaanza kumchunguza jiulize,
hivi ukamfumania, akakataa kuomba msamaha au akaomba lakini akagoma
kumuacha huyo anayechepuka naye utafanyaje?
Je upo
tayari kuondoka na kumuacha? Kama jibu ni ndiyo endelea kumfuatilia
lakini kama jibu ni hapana basi acha kabisa. Utajiumiza bure na kwakuwa
utakuwa ushamfumania na kumsamehe bila hata kuombwa msamaha basi utakuwa
umempa tiketi ya kuendelea naye.
Iko hivi mwanzoni alikuwa akichepuka
kistaarabu, akijificha kwakuwa hujui. Lakini ukishamfumania akakuambia
hayuko tayari kumuacha na wewe ukakomaa naye basi nisawa na umemruhusu,
kwani hataogopa tena kufumaniwa mara ya pili.
Kwa maana hiyo wewe utaendelea kuumia na
kila mara akitoka utajua yuko kwa fulani. Kama huna ubavu wa kumuacha
hembu acha kumfuatilia maana utajiumiza bure, mfuatilie mtu kama unataka
kumuacha zaidi utakuwa unahalalisha mke au mume mwenza tu.
No comments:
Post a Comment