“Mpaka sasa hivi bado anaendelea
kukupiga?” Mama John alimuuliza mkwe wake.” Ndiyo mama tena amezidi,
yaani kila siku nimekuwa kama ngoma, nimechoka Mama nibora nirudi kwetu,
kwetu sijaua Mama..” Anna alaiongea huku akitokwa na machaozi. Mama
mkwe wake alimuangalia kwa huruma, kisha akamuambia.
“Usiondoke mwanangu, nitaongea naye…”
“Haitasaidia chochote Mama, mara ngapi
tumekaa vikao kuongea naye lakini habadiliki. Wanangu wameshakuwa
wakubwa naondoka, sitaki kuendelea kuteseka…”
“Hapana usiondoke mwanangu, sasa hivi
nilazima akusikilize…”. Anna alikuwa amekata tama, miaka nane ya ndoa
yake ilikuwa ya mateso sana na mara kadhaa alishamlalamikia mama mkwe
wake kuhusu tabia ya mumewe kumpiga lakini haikusaidia.
Kila mara mumewe alisema atajirekebisha
anapokuwa mbele ya wazazi wake lakini akifika nyumbani huanza upya
akimpiga hata kwa kushitaki. Anna alishafanya mamauzi ya kuachana na
mumewe, tayari alishapata chumba chake na alienda kumpa tu taarifa Mama
mkwe wake ambaye walikuwa wakipatana sana.
“Wewe nenda nyumbani nitakuja huko huko
kuongea naya, safari hii atanisikiliza, si bado mnafuga Kuku?” Mama mkwe
wake alimuuliza swali ambalo hakuelewa kuwa lilikuwa linahusiana na
nini na kupigwa kwake, lakini alijibu. “Ndiyo Mama bado tunafuga…”
Alijibu na Mama mkwe wake alimuambia
kwenda nyumbani kwake na kesho yake angeenda kuwatembelea. Anna
aliondoka akiwa na wasiwasi, wazo la kumuacha mumewe lilikuwa palepale,
hakuwaza ni kitu gani ambacho angefanya ambacho kingemfanya kubadilisha
mawazo yake.
*****
Jioni ya siku iliyofuata Mama John
alifika nyumbani kwa mwanae, John alikua bado hajatoka kazini na Anna
alikuwa akijiandaa kupika chakula cha usiku, Mama John alimuambia mkwe
wake siku hiyo anataka kupika yeye. Ingawa Anna hakutaka lakini
alilazimishia mpaka akawa hana namna, aliingia jikoni na kuanza kupika
akiwaambia watu wote kukaa sebuleni kuangalia TV.
John aliporejea alimkuta mkewe na watoto
wakiangalia TV aliambiwa Mama yake yupo na yuko jikoni anapika, alitaka
kufoka kwanini mkewe anamufanyisha kazi Mama yake ambaye alikuwa mzee
lakini Mama yake alitokea na kumuambia yeye ndiyo kaamua kupika.
John alikuwa ampole kwani pamoja na
ukali wake kwa mkewe lakini bado alimpenda na kumuogopa Mama yake kama
mtoto. Alikaa kistaarabu sebuleni kama mkewe, Mama yake alimaliza kupika
na kutenga chakula mezani, Anna na Mfanyakazi wa ndani walipotaka
kumsaidia alikataa na kusema atafanya kila kitu mwenyewe.
Alitenga chakula mezani na kumpakulia
kila mtu kwenye sahani kisha akawakaribisha. Ingawa haukua utaratibu kwa
maana kila alikuwa akipakua chakula chake mwenyewe lakini hakuna
aliyeongea, wote walifurahia chakula cha Mama.
Wakiwa wamekaa mezani baada ya sala,
John alichukua kijiko na kuchota chakula, alipandisha mkono wake
kukiweka mdomoni lakini kabla hajafika mdomoni Mama yake ambaye alikaa
pembeni yake akimuangalia alikipiga kile kijiko chakula kikamwagika.
“Acha
kula hicho chakula, chukua hiki?” Mama John aliongea huku akichukua
sahani iliyokuwa na chakula cha John na kumsogezea ile ya kwake. Watu
wote walishangaa kwa kile kitendo lakini Mama John hakujali, aliichukua
ile sahani na kijiko alichotumia John akarudi jikoni kisha baada ya muda
akarudi na sahani nyingine ambayo alikula yeye.
John aliuliza nini kinaendelea lakini
Mama yake alifoka “Kula, hakuna kuongea wakati unakula! Unakuwa kama
sikukufundisha nidhamu?” Mama yake alimjibu kwa sauti ya juu.
Waliendelea kula kimya kimya, hakuna aliyetaka kuongea.
*****
Baada ya kumaliza kula, Mama John
hakutaka mtu aguse vyombo, aliondoa vyombo mwenyewe na kuvipeleka
jikoni. Kila kitu kilikuwa chakushangaza hawakujua kwanini kaamua
kufanya hivyo. Baada ya kuondoa vyombo na watoto wenda kulala, ulikuwa
ni wakati wa wakubwa nao kulala.
Kabla ya kwenda kulala Mama John alirudi
jikoni na kuchukua sahani ya chakula, ilikuwa ni ile ambayo alimkataza
mwanae kula. “Naomba mnisindikize nnje..” Aliwaambia na wao bila kujua
kuwa alikua anataka kufanya nini walinyanyuka na kuongozana naye, “Uje
na funguo za banda la Kuku”. Aliamrisha na Anna alienda kuchukua funguo
la banda la Kuku.
Walifika katika banda la Kuku, kulikuwa
na mabanda matatu, Mama John aliwaambia kufungua moja ambapo alimwaga
kile chakula kwenye lile banda la Kuku ambao walianza kukimbizana,
alifunga banda na kuwaambia waende wakalale. Bila kujua sababu zake za
kufanya hivyo waliingia ndani kulala kila mmoja akiwa na mawazo yake.
*****
Siku iliyofuata ilikua ni Alhamisi hivyo
Anna na Mumewe walitakiwa kwenda kazini. Waliamka mapema na kukuta Mama
mkwe kashaamka zamani na kashaandaa chai, ulikua ni mshangao kwani mara
kadhaa alikuja kukaa pale na hakuwa akifanya hivyo. Aliwaandalia chai
mezani na kwa mara nyingine John alipotaka kunywa alimzuia na
kubadilisha kikombe.
Walimuuliza kwnaini anafanya hivyo
lakini alikataa kuwajibu akiwaambia wanywe chai kwanza. Walikunywa chai
na baada ya kumaliza wakati wakitaka kuondoka, aliwaambia waende kwanza
kwenye banda la Kuku. Walifika na baada ya kuangalia, katika mabanda
mawili hakukuwa na kitu, Kuku walikuwa salama.
Lakini katika banda lile ambalo alikua
wamemwagia chakula ambalo lilikua na kuku zaidi ya kumi, wote walikuwa
wamelala chini wamekufa. John na mkewe walistuka na kushangaa nini
kimetokea, Mama yake aliwaangalia akiwa maetulia kwa muda kisha akasema.
“Unaona mwanangu, hicho ndiyo chakula
nilichokutengea mezani jana. Nilikuwa nimeweka sumu kama ambavyo
nimeweka katika chai asubuhi, kijiko kimoja tu au funda moja la chai
vilitosha kukufanya kuwa kama hao Kuku hapo!” Aliongea huku akiwaangalia
namna walivyokuwa wanashangaa midomo mizito hata kufunguka.
“Jana niliokoa maisha yako, lakini
ningeweza kukuacha ule na subuhi ukaamka kama hao Kuku nikawaambia
majirani umekufa kwa presha kama ambavyo naweza sema hawa Kuku wamekufa
na kideri…
Mkeo kila siku analalamika unampiga,
kila siku nakusihi acha kumpiga mkeo lakini husikii. Jana alikuja kwangu
na kuniambia kuwa kachoka na anataka kuondoka, huyu ni mke mwema,
wengine wanapochoka hawaondoki bali wanakuondoa wewe.
Nikuulize kitu kimoja wakati una miaka
mingapi?” John alilisikia swali lakini hakuweza hata kujibu bado alikuwa
ameshikwa na butwaa. “Huwezi kujibueee… mimi nakumbuka miaka 35, hembu
niambie wakati unakua kuna Babu yako hata mmoja ambaye ulimuona…?
“Hapana, hata siwakumbuki…” John alijibu kinyonge kabisa.
“Na Bibi zako…”
“Wote wapo mpaka sasa…”
“Nadhani
sasa umepata jibu… chezea kila kitu lakini si mwanamke anayekupikia
chakula! Usifikiri kila mwanaume anayekufa ni Mungu kapanga, wengine ni
wake zao wamechoka tu kupigwa na kunyanyasika. Mke wako anaondoka
kwakuwa ana kazi anajua anaweza kujihudumia, hembu jiulize kama
angechoka halafu hana kazi anajua ukimuacha anaenda kuwa ombaomba…
Mimi ni Mama yako nimeona mengi, acha
kujifanya mwanaume kuliko wanaume wengine, mwanaume kamili hampigi mke
wake anenda kupigana na wanaume wenzake. Mimi naondoka, sitegemei
kusikia umempiga mkeo tena…
Kama unataka kuendelea kumpiga basi anza
kupika mwenye…” Mama John alimaliza kuongea kisha akarudi ndani
akiwaacha wote wameduwaa, alichukua mfuko wake aliokuja nao na kutoka
nnje kuondoka. Alirudi na kumuona mwanaea amepiga magoti akimuomba mkewe
msamaha…”
Anna alikubalia kumsamehe mume wake
ambaye aliahidi kutokurudia tena. John aliahidi kubadilika na kweli
alibadilika, alianza kuwahi kurejea nyumbani na kurudisha mapenzi yote
kama kipindi cha uchumba, hakumpiga tena mkewe na sasa ndoa yao ina
miaka kumi na tano bila ugomvi wowote.
****MWISHO****
No comments:
Post a Comment