Habari ndugu, mimi ni Mama wa miaka 28.
Nimeolewa na nina mtoto mmoja. Mume wangu anamiaka 40. Kabla sijaolewa
tulika kwenye mahusiano miaka 5. Kwakeli nilimpenda sana nilimheshimu
naye alinipenda sana. Alinikutu bado msijacha yani bikra alifurahi
zaidi alinipenda zaidi alinifungulia account alikuwa ananiwekea pesa za
matumizi. Alinisomesha kuanzia format 6 mpka chuo.
Nilimtambulisha nyumbani wakamkubali
alikuwa mpole mstaarabu mwenye busara na hekima zote. Maisha yalisonga,
nilikuwa naenda kwake nafanya usafi wote napika kufua nguo. So kuna siku
nilikuwa nasafisha ndani nguo ya ndani ya mwanamke ambayo si yangu.
Niliumia sana nikarudi nyumbani nikawa sina amani kabisa na yeye
hakunitafuta baade nikampigia simu nikamwambia nilichokiona.
Jibu alilonipa kwamba yeye ni mwaume
anapesa na anauwezo wa kuwa na mwanamke yoyote atakaye mtaka kisha
akatata sim . Ikapita kam wiki nikaenda kwake nikamuomba tuzungumze
alinijibu kwadharau san nikashindwa kuvumilia nikaitafuna laini yangu
ili asinitafute tena Kwa kweli maisha kwangu yalikuwa magum san.
Matatizo yakaanza kunianda nilikuwa na mawazo san ikafikia kipindi
nikagombana na ndugu yangu niliekuwa nikiishi nae .
Visa vilikuwa vingi sana hapo nyumbani,
yule Mwanaume hakunitafuta tena Matatizo juu ya Matatizo Nikamfuata Dada
yangu mkubwa nikamuadithia akaniambia nawaza nini Nikamwambia mi nataka
kupanga akasema hawezi kuniruhusu mpaka aongee na mama kweli aliongea
nae na wakaniruhusu nikapanga na kuanza maisha.
Mambo yalikuwa magum sana tena sana
lakini nikaakimya sikuwaambia nyumbani Baada miezi mitatu nikapata kazi
maisha yakawa mepesi kwangu. Siku moja nikiwa kwenye mishe mishe za
maisha nikakutana na yule mwanaume. Tulikuwa hatujawahi kuwasiliana kwa
miaka miwili tangu nikute ile nguo ya ndani.
Alinisalimia na tukaanza kuongea akataka
tuongee kuhusu yale mambo lakini nilikataa nikamwambia tutapanga siku
ya kuongelea hayo nikaondoka zangu. Nimefika kwangu nikawa na mawazo
san. Kila sik akawa ananijulia hali baada ya wiki mbili tukaonana tena
na huyo mwaume alikuwepo nikaenda na aliniomba san msamaha na akasema
ameshaachana na yule mwanamke bado ananipenda sana.
Alipiga magoti kwakeli nililia sana na
nilikuwa bado nampenda nikamsamehe nikamueleza kwamba nimepanga
akashtuka san akaniomba anichukue nikaishi nae kwake lakini nilikataa
Baada ya miezi mitano tukiwa tunawasiliana wakati huo nilikuwa na
mahusiano na mume wa mtu ikanibidi niachane nae.
Nikarudiana na huyo mchumba wangu cha
ajabu alikuwa hataki kabisa kupajua nilipopanga Nikasema fine. Akawa
ananilazimisha nikakae kwake lakini msimamo wangu ulikuwa mguu nilikataa
katakata. Alikuwa na nyumbani nzuri ya kisasa alikuwa anaishi na wadogo
zake so uwezo wa kwenda kukaa ulikuwaepo kwani yeye ndio mkubwa na
nyumba ni yake lakini niligoma.
Baada ya msimamo wangu akaniomba tufunge
ndoa nikakubali na tukaoana. Maisha ya ndoa yalikuwa matam san.
Nikapata ujauzito Baada ya miaka miwili mambo yamejirudia yaleyale Kitu
kidogo anafoka Ananituka hana time na Mimi tena kitandani tunaweza tukaa
miezi hata sita bila kugusana na nikijaribu kumuliza ni makofi tu.
Japo ananijali kwa kula kulala na kuumwa
lakini amekuwa mkali san Chochote nikitendacho endapo kimemkwaza ni
kashifa tu kwangu anauwezo kutonisemesha hata wiki tatu. Najaibu
kumuomba msamaha lakini wapi. Nikaamua kufanya uchunguzi kumbe karudiana
na yule mwanamke wake wa zamani jamani naomba ushauri nifanyeje?
Nakuomba usinitaje jina langu. Nisaidie kimawazo, ninafanya kazi hivyo
naingiza kipato changu.
No comments:
Post a Comment