LABDA HII ITAWASAIDIA:
Kinachowaponza Wanawake ni POOR DECISION MAKING IN CRITICAL ISSUES.
Unakuta mtu anajua kabisa ana Boyfriend Levi la Kutupwa,analala
mtaroni kila siku,anafikishwa nyumbani hajitambui kafikaje,yeye yupo tu
amekazana na Fanta yake..Unachumbiwa na kuolewa na hilihili
levi,unasota nalo miaka 2 ya ndoa inakuwa kero...Ulimvumilia kwenye
Uchumba coz hamkuwa mnalala pamoja,analewa na kutapika akiwa kwake na
wewe uko kwenu..Sasa Mzigo ni wako,mko SAME BED..Anatapika hapo..Harudi
home siku 4..Na hata akirudi yuko Njwii,hata 'kazi hawezi kupiga'
Unaenda kulalamika kwa Mchungaji kuhusu Tabia mbaya ya mmeo...YOU KNEW
IT..Ukapuuzia na ukakubali kuolewa na JANGA...Mtabaki kusumbua
Wachungaji na Wakwe kuwapatanisha wakati mlikuwa na Muda wa kujuana
kabla hamjaamua kuishi pamoja
Kipindi cha Uchumba kitumie KUMFAHAMU VIZURI..Sio ukitumie KUMCHUNA,KULA
BATA,OFA ZA KITIMOTO,TRIP ZA BAGAMOYO,KUMPIGA MIZINGA YA PERUVIAN
HAIR..Ukasahau KEY ISSUES...Mmekaa miaka 6 ana watoto 2 na Wanawake
wengine..Analewa na kulala mtaroni..Halafu analeta Posa unasema kuolewa
ni Bahati.
Yakikushinda Usitusumbue...Sio kila POSA ni bahati,Posa nyingine ni
kichaka tu cha kutua majanga yao...Your Decision TODAY will affect your
TOMORROW...Think twice before you say YES to a Problem
No comments:
Post a Comment