Najua ni maneno makali lakini nilazima
yasemwe, kuna idadi kubwa ya wanawake ambao wapo kwenye ndoa, si
kwasababu ya upendo bali kwasababu ya pesa. Hilo si jambo baya kwani
maisha yenyewe mafupi, umezunguka hakuna wakukuoa au yupo na haeleweki
poteli ya mbali kula hela utampenda mbeleni.
Lakini kama mwanaume uliyeko naye
anakupiga, anakunyanyasa anakusaliti kila si na huna furaha halafu
unajidanganya kuwa ndoa ni uvumilivu, wakati hata humpendi huyo mwanaume
upo naye kwasababu ya pesa zake basi hata kama una ndoa inakufanya kuw
akahaba anayeteswa
Labda ili unielewe kabla ya kutoa mapovu
na kunilaumu kuwa nimetukana nichambue maana ya neno “Kahaba” tafsiri
hii nimeitoa kutokana na neno la kizungu Prostitute ambayo humaanisha
“…a person, typically a woman, who engages in sexual activity for
payment”.
Hapa wanamaanisha kuwa ni mtu (hata
mwanaume anaweza kuwa kahaba) hasa mwanamke ambaye hujishughulisha na
masuala ya kimapenzi kwaajili ya malipo. Kwamba unafanya mapenzi
kwaajili ya pesa, hapa hawajataja idadi ya wanaume ambao unapaswa
kujishughulisha nao au kama mko kwenye ndoa au la.
Kwa manaa hiyo basi kama wewe ni
mwanamke umeolewa na mwanaume ambaye humpendi na unapenda pesa zake, kwa
maana kuwa uko kwake kwasababu anakupa hela, anakununulia chakula
mavazi na kila kitu basi wewe ni kahaba.
Hivyo hivyo kwa mwanaume kama umeoa
mwanamke kwasababu ya pesa na humpendi bali unafanya mapenzi ili upate
pesa zake basi wewe ni kahaba. Lakini kama nilivyosema sijambo baya,
nijambo baya kama unapigwa au unayanyasika hapo ndipo unageuka na kuwa
kahaba anayepigwa.
Wakati kahaba wa mtaani yeye husimama au
hukutana na mwanaume wakafanya mapenzi akalipwa na kila mtu kwenda
kivyake. Wewe unakua na mwanaume, anafanya mapenzi na wewe mnaendelea
kuwa pamoja mkiishi kwenye nyumba moja, lakini ukimuudhi anakupiga na
kwakua unahitaji hela zake unavumilia na upo tayari kuvumilia kipigo ili
uishi tu kwenye nyumba nzuri.
Kuna wanawake wanaovumilia vipigo
kwakuwa wanapenda, yaani hawajali hata kuhusu pesa, ingawa sikushauri
kuvumilia lakini wewe hauko kwenye kundi hili. Hapa nazungumzia wale
ambao wanapigwa wanakasirika lakini mume akirudi anamnunulia nguo au
mkufu anamsamehe, hasamehi kwasababu anafurahia kupigwa bali kwa sababu
ya ule mkufu au nguo.
Lakini kuna wale ambao anamfumania
mumewe kila siku na wanawake tofauti, lakini kwakuwa anapewa pesa basi
huvumilia. Huyu hana tofauti na wale wanaojiuza, kwani wanaojiuza
hutembea na wanaume tofauti tofauti na kulipwa nao, lakini yeye hutembea
na mwanaume mmoja ambaye ana wanawake tofauti tofauti na kulipwa na
huyo mwanaume mmoja huku akiwa sawa na ametembea na wanawake wote
wanaotembea na yule mwanaume.
Hapoa nikimaanisha kuwa, ingawa
unatembea na mume wako tu ambaye unajua ana vimada 20 lakini kama wale
vimada ishirini kila mmoja akiwa na gonjwa lake yatakusanywa kwa mumeo
na utapewa yote wewe. Hii ni sawa na yule kahaba wa mtaani aliyekusanya
magonjwa ya wanaume ishirini.
Najua kwamba kama uko kwenye hali hii
ushaanza kutukana na kuniona nimeandika vitu vya uongo, unajipa moyo
kuwa unavumilia ndoa kwakuwa mna watoto, lakini ukweli nikuwa kama
humpendi huyo mwanaume na hufurahii mnapofanya mapenzi acha kuwasingizia
watoto, unavumilia kwasababu ya pesa.
Kwa mwanaume kufanya mapenzi na mwanamke
ambaye hakuvutii na humpendi wala si shida kwakuwa hisia zetu si za
kuunga unga zipo tu. Lakini kwa mwanamke kufanya mapenzi na mwanaume
ambaye anakutia kichefu chefu ni kazi yaani hata hafurahii kwakuwa hisia
zao ni za kuunga unga.
Hivyo kama unavumilia kufanya mapenzi na
mwanaume kwa miaka kumi ambaye humpendi kwasababu tu ya pesa, hongera,
lakini kama umevumilia na kipigo, manyanyaso basi pole na amka. Acha
uvivu jishughulishe na tafuta cha kwako.
Vumilia ndoa kwasababu unampenda mtu,
unafurahia kuwa naye hapo hata ukimuomba Mungu atakuelewa na kukubariki,
anaweza kumbadilisha. Lakini kama unavumilia kwaajili ya pesa hata
Mungu harakusikiliza kwakuwa hata wewe si msafi.
Unapoomba ushauri kwa mwanamke mwenzako
akakuambia kuwa ndoa ni uvumilivu hata nayeye anavumilia hembu muulize
sababu za yeye kuvumilia kwake ili usije kuwa unashauriwa na mtu ambaye
amekubali mwili wake kutumika kwa mapenzi na kipigo kwaajili ya pesa!
Kwamba upo na mtu ambaye anavumilia
kupigwa ili aendelee kuendesha gari zuri na kuringishia mtaani. Mtu
ambaye anakubali kuipigwa kwasabu ya iPhone 6, mtu ambaye anakubali
kupigwa kwasababu ya Brazilian hairs. Huyo atakuwa anajipa moyo tu kuwa
ni mke wa mtu lakini ukweli ni mfanyakzi wa mtu.
Huna ulemavu wowote, una akili timamu
halafu bado unajiuliza “Sasa nitafanyaje…nitaenda wapi?”. Acha kumkufuru
Mungu aliyekupa nguvu na akili, siku huyo mwanaume akikuambukiza
magonjwa, siku akikutoboa macho, akikuvunja miguu na kuw a mlemavu ndiyo
utakosa kweli pakwenda.
Lakini pia huyo mwanaume anajua uko
kwake kwaajili ya pesa ndiyo maana anakufanyia anachotaka. Mwanaume
akijua unampenda kweli ni rahisi kubadilika kama unamvumilia lakini
akijua unapenda pesa zake hana sababu ya kubadilika kwani ashajua
unachotaka hivyo atahakikisha unakuwa nacho kila wakati.
Anajua akikupiga, ukimfumania akakuletea
mkufu wa dhahabu unasahau, anajua akikupiga na kukupa ada ya ndugu zako
unafurahi, sasa ana sababu gani ya kubadilika zaidi ya kuendelea
kutafuta pesa tu ili kukuridhisha. usidhani nayeye ni mjinga hajui nini
unapenda zaidi kwake pesa au yeye?
No comments:
Post a Comment