Haya ni mambo 8 ya kufanya na kutokufanya ili kuondoa matatizo katika
uhusiano wako na kuyapa nguvu mahusiano yako na Mwenza wako.
Kwa hali halisi na mazoea tunaweza kusema kwenye mapenzi kuna kitu kilichomo
zaidi ya sanaa ya upendo kuliko tunavyoweza fikiria. Watu ni watata,
waliojawa madhaifu na wingi wa tamaa, na wenye kutafuta kueleweka zaidi.
Ukiacha hayo, Mwanadamu pia amejawa na uwezo mkubwa sana kuonyesha upendo endapo wataonyweshwa au kupewa upendo sahihi.
Dhumuni kubwa la mahusiano linatakiwa kuwasaidia tulionao kwenye
mahusiano waachie upendo wao mwingi ili tuweze pata mahusiano
tunayoyahitaji. (Fulfilling relationship)
Tunaona kila siku kwamba watu wanaendelea kufanya makosa yale yale kila
siku kwenye mahusiano na kutegemea kupata majibu tofauti. Mbaya zaidi
kukosekana kwa usalama au kutokujiami (insecurities) na tabia mbaya
zinapelekea kukufanya mtu atende vitu vinavyopelekea kuharibu kile
tunachoweza sema mahusiano yenye afya njema. Watu tofauti tunaokua nao
kwenye mahusiano huleta hisia tofauti kwetu, nyingine unaweza hisi
hukuwahi kabisa kua nazo kabisa na kudumisha mahusiano kukawa kugumu kwa
pande zote mbili. Kwa hili tunatakiwa kuhakikisha tunafanya sehemu
yetu.
Sasa tunafanyaje kutatua yote hayo na kuboresha ubora wa upendo wetu:
Haya mambo 8 yatakusaidia na kama ukiyafanya yakawa tabia yako,
utaimarisha mapenzi yako kwa amani, fahari na furaha.
Kuza hisia za kuwa zaidi ya Rafiki
Watu wengi huishi pamoja kimwili lakini hawako pamoja kihisia. Hisia za
zaidi ya kirafiki ni kujua nini mpenzi wako anataka kabla hata ya yeye
kupata nafasi ya kukuambia au pia kuchukua hisia zao kama vile ni zako.
Unaweza kukuza hizi hisia za zaidi ya urafiki kwa kuwa mkweli kwa mpenzi
wako na kuwa mwepesi kusaidia katika analolihitaji.
Panga maisha pamoja.
Plani zetu za maisha zinaweza zisiwe jinsi tunavyozitaka, lakini kwa
kuwaza kwa kuangalia maisha yako yatakua vipi badae na mpenzi wako,
inahamasisha kuchukua hatua sahihi kudhihirisha mipango yetu ya muda
mrefu. Ongelea kuhusu miaka ijayo na pia panga mikakati ya kufikia vitu
hivyo mnavyotaka kwa pamoja: yaweza kuwa nyumba, familia, uwekezaji n.k
3. Leta pumziko au faraja.
Mpenzi wako anataka kurudi nyumbani kuliko na upendo na sio maumivu ya
kichwa. Tengeneza nyumba yako iwe sehemu inayomfanya mpenzi wako
ajisikie amani, imara na sehemu ya kulelewa. Usianze kuongelea kuhusu
matatizo yako mara baada ya kuingia mlangoni. Bili, kazi, mkwaruzano
mliokua nao asubuhi- hivi vitu vinaweza kusubiri mpaka mazingira sahihi
ya ninyi kuyaongelea hayo.
Tenda kwa wakati.
Wakati unaweza kuwa adui yako mkubwa au rafiki yako mkubwa. Katika kila
muda, wakati unaweza kuwa upande wako au badala yako. Hekima ni kutambua
tu wakati gani utende hiki na wakati gani usubiri kutenda kile.
Ukisikiliza kilicho moyoni mwako unaweza kutambua mawimbi tofauti ya
wakati. Usimlazimishe mwezi wako kufanya kitu ndani ya muda fulani,
mfano kumsukuma kuoa ndani ya mwaka mmoja, hii ni dhana yako wewe ya
wakati sio ya kwake. Chukua hatua kubwa ya kuendelea mbele endapo tu
nyote mmekubaliana kufanya hivyo hata kama itachukua muda mwingi kuliko
ulivyotaka.
Usitumie udhaifu wao.
Kila siku unauamuzi wa kuchezea udhaifu wa mwenzio au kuimarisha uwezo
wao. Kama kila mara wewe huongelea tu kile anachokifanya vibaya mwenzio,
hawataweza kupata motisha ya kufanya chochote vizuri. Hamna mahusiano
yatakayoweza kushamiri katika mazingira hasi ya namna hiyo.
Kuna njia za kiungwa nyingi tu za kumuelewesha mpenzi wako kipi anapaswa
afanye tofauti, na kuwakaripia mara kwa mara sio miongoni mwa hizo
njia.
6. Usilipizie / usilipize kisasi
Kwa chochote kile alichofanya mpenzi wako au alikukosea zamani,
usilipize kisasi. Dunia ni duara, Weka nafsi yako iwe safi kwa kumtendea
mtu kile ambacho wewe akikutendea utafurahi bila kuwaza alikuafanyia
nini. Hii ni wajibu wako kwa ajili ya nafsi yako na si kwa mwingine
yeyote. Kumbuka, unavyotendewa na mtu ni ‘karma’ yake, unavyomjibu wewe
ni ‘karma’ yako.
7. Usidhani au kuzusha vitu nje ya uwiano. (out of proportion)
Kabla hujatupa mpira, kaa chini na tafakari fikra hizo kwa umakini: hivi
hiki ni kabaya kiasi hiki? Ongea na mpenzi wako kwa wazi kuhusu
kinachokutatiza badala ya kumvamia.
Mara nyingi tunakuza ukali wa jambo kwasababu ya woga na kutokujiamini, wakati kiukweli wala haiko hivyo tunavyofikiria kabisa.
Kabla ya kudhani vitu ambavyo tunahisi vinaweza kuwa vya uongo, jiulize kama ni kweli vina uzito wa kuhatarisha mahusiano yenu.
Usifanye maamuzi kwa pupa. (out of desperation)
Fikiria kwa makini maamuzi yako hata mara elfu moja kabla hujaamua.
Maamuzi ya pupa yatazidisha tu matatizo. Kama unataka mpenzi wako
abadilike kwa hali yoyote ile, usimtishie kuachana nae wakati kiukweli
ni kitu cha mwisho kabisa ambacho ungetaka kufanya. Akikubali kuachana
na wewe utajisikia vibaya zaidi. Acha hisia zako zipoe kwanza kabla ya
kumfikishia chochote kile, jaribu kila mara kuangalia sababu
zilizojificha za kwanini wanafanya wanayofanya kwa wakati huo.
Mahusiano ya mapenzi ni wazi kwamba ni magumu sana kuyatunza kama
hatutafata njia sahihi kukubaliana na maadiliko chanya. Chukua haya
mambo nane kuondoa matatizo na kuimarisha mapenzi yako na mwezi wako.
No comments:
Post a Comment