Hivyo basi yako mambo mengi ya kuzingatia kabla hujamnunulia mke wako mtarajiwa pete hiyo ya Uchumba(Engagement Ring), na hii ni kwa sababu ziko pete aina nyingi za uchumba na ni juu yako wewe kuchagua ni Pete ipi itamfaa huyo mpenzi na amani ya Moyo wako daima.
Yafuatayo ni mambo ya kuzingatia kabla ya kununa Pete ya Uchumba kwa yule wako wa Moyo.
#1.Mfumo wake wa Maisha na Namna anavyoishi(Lifestyle)
Hii ni pete ya uchumba, na itakaa katika kidole chake siku zote, na kama ndivyo ilivyo, itakua sehemu ya maisha yake tangu ile siku utakayomvisha na kuendelea. Pete nyingi za uchumba zinaendana na LifeStyle tofauti tofauti. Hivyo Basi, kabla hujanunua pete hiyo ni lazima uweke jambo hili kichwani yakwamba Je pete hii itaendana na Lifestyle yake ama La?Usimfanye ajihisi kwamba kapewa adhabu ya kuvaa kitu ambacho ni kero katika maisha yake na kazi zake. Fikiria ni namna gani anatumia mkono wake, mfano kama ni mwalimu ama daktari huwezi ukamnunulia pete yenye Urembo Ulio jiiinua kwa juu sababu tuu Mkono wake huo anautumia kushika watu na Vitu vingi zaidi.
Kama kazi zake ni za shambani na maeneo yafananayo na hayo basi Simple Ring ndio itakayomfaa kwa kua haitakua na Mbwe mbwe nyiingi na Manjonjo kibao bali Uzuri tuu.
#2.Aina yake Mwenyewe (Personal Style).
Pete ni sawa na kitu chochote kile ambacho mtu anaweza akavaa. Unapaswa kuangalia ni nini anapenda Kuvaa, material ya Nguo zake na rangi azipendazo katika nguo zake. Hii itakusaidia kutafuta pete itakayo endena nae na ni lazima ataipenda pia.#3.Bajeti yako(Kiasi cha fedha ulicho-nacho)
Tambua yakwamba pete hizo zipo nyingi na zenye thamani ya hali ya juu pia. Usijilizimishe kununua pete ya ghali sana kama wafanyavyo wengine ikiwa tuu mfuko wako hauruhusu. Tambua ya kwamba unachotafuta ni pete Simple na yenye uzuri ambayo itaendana na Mtu unaemnunulia.Usije ukajilazimisha kununua pete ambayo ni ghali ingawa huna pesa za Kutosha kununua pete hiyo maana utajikuta ukiutesa moyo wako kwa kutaka usivyo viweza.
#4.Size ya Kidole Chake.
Kama zilivyo pete za Ndoa, basi hata pete hizi za Uchumba zina size tofauti tofauti pia. Zipo za Size Kubwa na Size ndogo pia. Kabla Hujafanya maamuzi ya kununua pete fulani, hata kama ina uzuri wa aina gani, ni lazima ufahamu Size ya Kidole cha mchumba wako.Jambo hili litakufanya uepuke balaa zitakazokukuta ile siku ya kumvisha pete mpenzi wako huyo kwani kwa kushindwa kutambua size sahihi ya kidole cha mpenzi wako kutaweza kusababisha kumvalisha pete Kubwa ama ndogo Kuliko Kidole chake( Ha ha ha haaaa) jambo ambalo litakua ni aibu kubwa mno.
#5.Ubora na Utunzaji wa Pete hiyo.
Pete ni Kitu kidogo mno ambacho kinaweza kupotea ama kuibiwa ama kusahaulika mahali popote na muda wowote. Itakusikutisha sana na utaumia sana pale utakapoambiwa kwa Ile pete ya thamani uliyonivisha imepotea ama imeibiwa ikiwa tuu ni wiki moja tangu umeinunua pete hiyo na hutoweza kufanya lolote.Ni vizuri kununua pete kwa Sonara anae-aminika ambaye atakupatia warranty ambayo itakuwezesha wewe kufidia pete ile iliyopotea(Hapa nazungumzia maswala ya Bima ama kwa lugha nyingine tunaiita Insurance).
Ni hayo tuu macheche niliyo kuandalia. Ni mimi Francis Mawere, mti mkavu usochimbwa dawa,
No comments:
Post a Comment