Nilikua mtu wa Kuichukia asubuhi yangu kila kukicha. Nilichukia
kuamka mapema, Lakini nilikua nikisikia na kusoma haya mambo na faida za
kuamka hasubuhi na mapema. Kuamka mapema kuandaa mambo yako, Kuweka
mambo sawa, kuuweka mwili wako fit nk.
Kipekee niliona faida za kuamka hasubuhi na mapema. Na zifuatazo ni
njia za kuifanya asubuhi yako na siku yako kuwa nzuri kabisa.
1.Jinyooshe kwa Muda wa Dakika 15.
Punde tuu utakapokua umeamka toka kitandani, jinyooshe na kufanya
mazoezi kama Vile Yoga kwa muda wa dakika kumi na tano. Kitendo hichi
kitaufanya mwili wako kuchangamka. Nguvu hiyo utakayo pata itakaa na
wewe siku nzima.
2.Kaa mbali na Vifaa vya Kielekroniki.
Utakapoanza kushika shika vifaa hivi mfano Sumu, computer nk utakua
unajitengenezea Stress(Msongo wa mawazo) na kukuharibia siku yako
kabisa. Unaweza kukutana na SMS ama Email ambayo kwa kweli itaweza
kukukwaza siku nzima. Hivyo basi, ni vizuri ukaachana na mambo hayo
hasubuhi na kufanya jambo jingine ambalo litakusaidia.
3.Tengeneza Plan yako ya siku nzima.
Ikiwa hukutengeneza plan yako kwa ajili ya siku inayofuata mara baada
ua kutoka kazini, basi uamkapo asubuhi fanya jambo hilo. Kufanya hivyo
kutakufanya wewe kuwekeza mawazo yako na nguvu zako zaidi katika Ufanisi
wa kazi zako na Uzalishaji.
4.Pata breakFast ya Nguvu.
Najua unafahamu juu ya swala hili la kupata breakfast ya nguvu
hasubuhi kabla ya kuanza shughuli zako. Unapokua unapata kifungua kinywa
cha kweli pindi uamkapo unapata Nguvu ya kuanza shughuli zako
kiuhakika, utaweza kulenga zidi katika shughuli zako.
5.Fanya yale mambo yanayokupa Furaha.
Furaha ni jambo Muhimu mno katika maisha ya mwanadamu awaye yeyote yule.
Unapokua umeamka asubuhi jitahidi kufanya yale mambo yote ambayo hua
yanakupa Furaha wakati wote, hii itafanya siku yako kuenda sawa sawia
kwani Utakua na amani moyoni mwako na katika fikra zako hivyo kupelekea
ufanisi katika katika kazi zako.
6.Kunywa Maji angalao glass Moja.
Ni wazi kwamba unapokua umelala usiku kwa muda wa masaa 8, mwili
hupoteza kiasi fulani cha maji, hivyo basi yakupasa kupata maji walao
glass moja ili kuongeza maji mwilini. Tia limao kidogo katika maji hayo
na hii itakusaidia katika mmeng’enyo wa chakula kukaa vyema na zaidi ya
yote utapata nguvu zaidi na mwili kuchangamka.
7.Jiweke teyari, hata kama utakua umekaa tuu nyumbani.
Labda umepanga siku yako kuwa ya Uvivu(Jambo ambalo ni poa pia kwa
wakati mwingine), lakini ni vyema kujiandaa na kukaa sawa kwa ajili ya
siku yako kwa ujumla hata kama hutotoka nyumbani siku nzima. Hii
itakufanya kuuweka mwili wako sawa na hivyo kuwa full organized, jambo
ambalo litakuweka poa siku nzima.
8.Anza Shughuli zako na Mungu wako.
Imani ni jambo la muhimu mno, Kila mmoja na imani yake, hivyo ni
vyema kabla ya kuanza shughuli zako za kila siku ukanza na Mungu wako.
Jambo hili litaluweka sawa kiroho hivyo hekima katika maisha yako itakua
na wewe.
No comments:
Post a Comment