Artikel Terbaru

Responsive Ads Here

Tuesday, May 9, 2017

Njia 4 za Kuongeza uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu katika Ubongo wako

Njia 4 za Kuongeza uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu katika Ubongo wako
Yawezekana umekua ukijishtukia ukiwa katika hali ya kusahau mambo kila mara ama kupoteza kumbukumbu na muda mwingi umekua ukitafuta suluhisho sahihi juu ya tatizo hilo.
Jambo zuri ni kwamba kila mmoja anaweza kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi kumbukumbu katika ubongo wake kwa kufuata zile njia maalumu na kufanikiwa na hakuna haja ya Kubadili mifumo yetu ya maisha ili kuondokana na tatizo hilo.
Zifuatazo ni njia sita ambazo zitakusaidia kuongeza uwezo wa Ubongo wako kuhifadhi kumbu kumbu.

1.Hakikisha Unapata Usingizi wa Kutosha.

Mara nyingi watu wenye pilika nyingi(Busy) hukosa hata muda wa kulala jambo ambalo hupelekea uwezo wao wa kuhifadhi kumbukumbu kushuka kwa kiasi Fulani. Hakikisha una lala angalao masaa saba hadi tisa kwa siku, jambo hili litaongeza uwezo wako wa kuhifadhi kumbu kumbu katika ubongo wako.

2.Jiwekee tabia ya Kutembea kwa miguu mara kwa mara.

Kutembea tembea kwa miguu mara kwa mara ni njia mojawapo ya mazoezi kwani hupelekea mzunguko wa damu kufanya kazi kama inavyopaswa. Damu hubeba Oxygen ambapo oxygen hiyo itasafirishwa katika sehemu muhimu za mwili ikiwamo UBONGO wako.
Pata mapumziko baada ya kufanya kazi kwa Muda mrefu.
Unapokua unafanya kazi kwa muda mrefu, akili nayo hufikia pahala na Kuanza kupunguza uwezo kwa Kuhifadhi mambo kama inavyopaswa.

3.Changamsha ubongo wako.

Kama unapenda kupeleka ama kukuza uwezo wako wa kuhifadhi kumbu Kumbu tafuta njia mbali mbali ambazo zitaweza kuuchangamsha Ubongo wako. Cheza Games zile zinazohusiana na memory mfano Crossword puzzles games ama zile zetu tulizo zoea kucheza kama vile Draft na Bao. Kitendo hichi kitepeleke uwezo wako wa kuhifadhi kumbu kumbu kichwan kuongezeka siku baada ya siku.

4.Kula chakula bora

Vyakula tunavyokula huchukua nafasi kubwa mno katika ujenzi wa miili yetu. Vile vyakula bora hujenga miili na kuimarisha miili yetu lakini vile vyakula visivyo bora hubomoa kabisa afya zetu. Ubongo huhitaji asilimia kubwa sana ya Protein hivyo basi jitahidi kula kwa wingi vyakula vyenye protein mfano nyama, maziwa na maharagwe.

No comments:

Post a Comment