§ Amua kuweza kuongea na mpenzi wako mara kwa mara, mueleze alivyo wa thamani kwako.
§ Kuwa tayari kumsikiliza mpenzi wako kila wakati ikiwezekana mguse au mshike wakati unapomsikiliza.
§ Angalianeni mara kwa mara hasa nyakati mnapokuwa na furaha au hata zile nyakati furaha inapokosekana
§ Mguse na mshike hata nyakati ambazo hauna haja na tendo la ndoa. Sio kwamba kila ukimgusa ndio ajue muda wa ku “do” umewadia
§ Msilale
kama maadui, gusaneni na kumbatianeni, mbona hata wanyama wengine
wanafanya hivyo?Ingawa hawana ndoa kama uliyonayo wewe?
§ Kubali, heshimu na onyesha kupenda vile vitu vizuri anavyovifanya mpenzi wako, sio kila wakati wewe ni wakukosoa na kupinga tu.
§ Mpe
tabasamu hatakama huna sababu maalumu ya kutabasamu, kwani unapoteza
nini ukitabasamu? Au tabasamu inakugharimu kiasi gani? Mbona kwa wengine
unatabasamu?
§ Mara
nyingine chukua muda wako simama naye jikoni anapopika au anapofanya
kazi nyingine, ongea nae, au onyesha kumsaidia kile anachofanya. Kule
kusimama karibu naye hatakama haumsaidii kitu akiwa jikoni kunampa nguvu
kuliko msaada wako mwingine katika maeneo mengine.
§ Mwambie
ukimwangalia usoni kwake kwamba pamoja na madhaifu yako yote (yani
madhaifu yako wewe mwanaume) bado yeye ndiye mtu wa muhimu kabisa
maishani mwako. Usinyamaze tu ukidhani anajua hilo, sema kwa kinywa
chako, mwambie, tena sio tu kwa meseji za simu au kupitia meseji za
mitandao, mwangalie usoni na umtamkie.
No comments:
Post a Comment