Ipo
tofauti kubwa kati ya neno kusikia na kusikiliza, hauhitaji kuwa na
digrii ya mawasiliano au kuwa mtaalamu wa mawasiliano ili kujua hili.
Kusikia ni kitendo cha masikio kuhisi sauti pasipo ulazima wa kuitafsiri
maana ya hiyo sauti, wakati kusikiliza ni pale masikio na akili
vinapohusika pamoja kuihisi sauti, kuielewa na kuitafsiri maana yake na
kuandaa mrejesho kwa kile kilichosikiwa (akili inaelewa kilichosemwa).
Sasa kwa kufahamu utofauti huu utagundua kabisa kwamba maranyingi kwenye
mahusiano baina yetu na wapenzi wetu tuna sikiana zaidi ya
kusikilizana. Hakuna aliyetayaru kumpa mwenzake sikio kwa nia ya
kumsikiliza na kujali kile mwenzake anachosema, kila unachojaribu kusema
kinapuuziwa na kutokueleweka. Ukosefu wa kusikilizana unaathiri sana
mawasiliano baina ya wewe na mpenzi wako na huo ni ufa mkubwa sana
katika kuongeza misuguano, tofauti, migogoro na hata kufikia kuachana.
Bahati mbaya wanaume wachache wanajua kwamba mwanamke ameumbwa na kiu ya
kusikilizwa zaidi kuliko mwanaume, na bahati mbaya kubwa ni kwamba
mwanaume ndio kilema mkubwa wa kusikiliza, sasa basi kama kweli
unampenda basi jitahidi kumsikiliza, sio tu kumsikia, na wewe mwanaume,
zawadi pekee na ya maana unayoweza kumpa huyo mpenzi wako wa kike ni
KUMSIKILIZA – Chris Mauki
Tuesday, May 16, 2017
MNASIKIANA AU MNASIKILIZANA???
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment