Kama ambavyo wanaume hawapendi
kusikia kuhusu wanaume wengine ndivyo hivyo ambavyo wanawake hawataki
kusikia unasifia wanawake wengine, wawe wapiti njia, marafiki zake au
hata wale unapowaona kwenye TV. Pale utakaposifia kuwa “yule muigizaji
anakifua kizuri” itakuwa ni sawa na umemuambia mpenzi wako anakifua
kibaya na angalau kwa wanaume ni rahisi kusahau lakini kwa mwanamke kila
wakati akimuona yule mwanamke au mwanamke aliyefanana fanana na yule
hata kama ni kwenye TV atajisikia vibaya sana.
Wakati mwingine atahisi unamsaliti
na hatajiamini. Kwakifupi acha kusifia mwanamke mwingine mbele ya mpenzi
wako, acha kujifanya unasema mimi napenda wanawake wa aina flani…to
hell na wa aina flani, kama umemchagua huyo inamaanisha ndiyo aina ya
unaowataka. Unapata faida gani kumfanya mwenza wako kujisikia vibaya
kutokana na muonekano wake.
Unaweza kumuambia “Baby napenda uwe
unavaa nguo za aina flani, zinakupendeza na nazipenda… Hiyo ni sawa
kwakuwa nguo anaweza enda shona dukani na akawa kama unavyotaka, lakini
hana tako unamuambia unataka matako, chuchu saa sita unamuambi unataka
sijui makubwa ya kushika…yeye ayapate wapi, ungetaka ungewafuata wanye
hivyo vigezo.
Umemkuta na unene wake wa asli
unamuambia unataka slim, unamsumbua dada wa watu kujikondesha kumbe
ndiyo alivyo zaliwa na hapungui. Anajilazimisha kula malimau na kushinda
njaa kisa ufurahi! Kwa mwanamke muonekano wake ni kila kitu, akihisi
hufurahii muonekano wake jua kuwa hata kitandani hatafurahia,
hutamridhisha na kubwa kabisa hata wewe unaweza usiridhike na huo ukawa
mwanzo wa kuvunja uhusiano wenu, chagu cha kuongea na wakati wa
kukiongoa.
No comments:
Post a Comment