Katika mapenzi suala la kuchokana ni
jambo la kawaida na inapofikia wakati mwenza wako akaanza kukuchoka ni
vyema ukajua ni dalili gani ili muweze kurekebishana mapema kabla penzi
halijavunjika. Watu wengi hujisahau na kusubiri mpaka mambo
yanapoharibika ndiyo hujaribu kusuluhisha na wanakuwa wameshachelewa.
Ingawa zipo dalili nyingi lakini kwa leo nimeamua kuchambua dalili hizi
12 kwaajili yako rafiki yangu wa nguvu.
{1} Hapokei simu zako, anachelewa kujibu meseji;
Katika ulimwengu huu wa teknolojia naamini hii ndiyo dalili kubwa ya
mtu kuanza kumchoka mtu. Utakuta unampigia simu mara tatu kwa siku
lakini hapokei na jioni anakupigia huku akijifanya alikuwa bize. Kuna
ambao ni kawaida yao kufanya hivyo lakini kama zamani hakuwa hivyo,
alikuwa akipokea au kukupigia kutwa mara tatu, jua ushaanza kukuchoka.
Lakini pia unaona anachelewa sana
kujibu meseji zako kuliko kawaida yake au hajibu kabisa na ukimuuliza
anakuwa na sababu zisizoeleweka kama vile sikuiona, nilikuwa bize, au
sikuwa online wakati ulimuona online au kwenye magroup anachangia kama
kawa. Wakati mwingine anaweza kweli kuwa alikua bize au hakuziona meseji
zako lakini kama anafanya hivyo kila siku jua kuwa ameanza kukuchoka.
{2} Hataki muda wa nyie wawili tu;
Mlishazoea kutoka mara kwamara wawili, mlishazoea kufanya mambo kwa
pamoja lakini ghafla yuko bize, hataki kuwa tena karibu na wewe na kila
mara anakuwa na visingizio. Mkipata kamuda ka wawili pamoja nnje ya
kitandani atakuwa bize na simu yake na unaona kama uko peke yako,
atatafuta sababu tu ya kuondoka. Ukiona hizo dalili basi jitathimini
angalia kuna kitu hakiko sawa.
{3} Anakukatisha kila mara unapoongea na kukukosoa kidharau;
Ndiyo unakuta kila mkiwa na marafiki zenu ukiongea kabla hujamaliza
anatafuta kakitu ka kukukosoa na kukuzodoa, tena ile kwa dharau kana
kwamba hujui chochote. Atawaunga mkono wengine lakini si wewe, anajaribu
kukushusha mbele ya marafiki zake na marafiki zako na wakati mwingine
hataki uongee kabisa, anatamani usiwepo mnapokuwa na marafiki wenu.
{4} Anakosoa kila kitu unachomfanyia;
Yaani katika kila kitu unachomfanyia atajaribu kutafuta kitu kidogo tu
cha kukosoa ili tu ujisikie vibaya. Ukimfanyia kitu cha upendo
anakipokea kwa shingo upande na atakiangalia na miwsho atakitoa kasoro,
hata kama ni kitu ambacho awali alikuwa akikipenda kwa dhati na
kukifurahia hakifurahii tena. Atakosoa kitu hicho na kukosoa kwake
hakuishi, unaweza kumpa zawadi akaikosoa na kuiacha mpaka ikaharibika
bila kuitumia.
{5} Anakumbushia makosa ya zamani;
Kuna makosa ambayo alishakusamehe na mlishasahau lakini ghafla umefanya
kitu leo utamsikia. “Hii ndiyo kawaida yako, unakumbuka mwaka juzi
tukiwa chuo, ulifanya hivi hivi?” Anaweza kununa au kama mlikuwa sehemu
kuondoka kabisa kwakuwa tu amekumbuka kitu ambacho ulimfanyia miaka kumi
iliyopita.
{6} Kitandani ni kazi tu, hakuna ‘Romance’ wala baba yake kushikana;
Zamani mpaka mnaanza mechi mlikuwa maingia bafuni pamoja, sijui
manjonjo yote lakini sasa hivi ni kama adhabu au mko jeshini ni kazi tu
na mkishamaliza anaweza kukuambia ondoka niko kesho natakiw akuwahi
kazini au kama yuko kwako akaondoka bila mazungumzo wakati mwingine hata
kuoga hataki, inakuwa kama mnalazimishana.
{7} Anawasifia watu wa jinsia tofauti mbele yako kama vile haupo;
Yaani mko tu kapita mwanamke mzuri anasifia tena anasifia kitu ambacho
anajua kabisa huna na anajua itakukera, kapita mwanaume anasifia bila
kujali hisia zako. Mwanzoni hakuwa hivyo alikuwa makini kulinda hisia
zako lakini sasa wala hajali. Anaweza hata kuwaisfia marafiki zako mbele
yako na wakati mwingine kuulizia kuwa wanaendeleaje hata kabla ya
kukuuliza unaendeleaje.
{8} Anataja mtu wa ndoto zake ambaye si wewe;
Utasikia napenda nioe mwanamke mweupe wakati wewe ni mweusi au anasema
anataka mfupi wakati wewe mrefu, yaani kila anachoongea ni kinyume
nyume na wewe ulivyo. Mbaya zaidi hakuongelei kwenye mipango yake ya
baadaye, haongelei kitu anachokipenda kutoka kwako, bali anachopenda
kutoka kwa wengine.
{9} Haonyeshi kuvutiwa tena na wewe; mwanzoni
hata kabla ya kuvua nguo alikuwa shapagawa anakuvamia na mnaanza
kuvuana, ila sasa umevua nguo uko mbele yako wala hastuki ndiyo kwanza
yuko na simu anajibu meseji, mpaka umshike na kumvutia kitandani ndiyo
anastuka. Unamhitaji na uko sexy balaa lakini utamsikia subiri kwanza
nimalizie kuangalia mpira au hii tamthilia, jua kuna kitu jiongeze.
{10} Amefuta picha zako katika mitando ya kijamii;
hapa ndipo ujue unakaribia kauchwa, alikuwa ameweka picha zako, na
status za kimapenzi lakini taratibu anaanza kufuta, alikuwa anacomment
kwanye kurasa zako lakini hafanyi tena, ukimtag anaondoa tag. Wakati
mwingine anaweza kukuambia anajitoa kwenye mitandao ya kijamii lakini
baada ya muda unakuta kaanzisha akaunti nyingine. Hapo alikuwa anaogopa
kufuta picha zako hivyo kwa kuanzisha akaunti mpya hatakuwa na sababu ya
kukupost.
{11} Anazungumzia sana kuhusu kuwa single na kuachana;
Yaani utakuta hakuambii nakuacha lakini unakuta kila mara anzungumzia
kuhusu kuachana, kuwa single, anasifia watu walio single kila mara,
anaponda mapenzi, anajifanya kukata tamaa za kimapenzi na mambo kama
hayo. Ukiona hivyo jua anataka kuachana na wewe lakini hajui ni namna
gani ya kuachana.
{12} Hakung’ang’anii tena;
Awali ukimuambia uko bize msionane basi atakubembeleza mpaka utaona
poteli ya mbali ngoja nikamuone hata kama ni kuongea tu. Sasa hivi hata
kama ukisema uko bize kwa utani utasikia tu “Poa nitakucheki basi…” na
baada ya hapo ndiyo nitolee hakuna cha kukucheki wala kuku cash, mpaka
umtafute tena na yeye kujifanya yuko bize. Akikuambia nitakupigia au
nitakutafuta baadaye ujue ndiyo imetoka hiyo mpaka umtafute wewe.
Hizi ni baadhi tu ya dalili, zipo
nyingi kutegemeana na mtu, muhimu ni kumjua vizuri mwenza wako na
kuangalia kama kuna mabadiliko yoyote. Hii inatokana na ukweli kuwa
wakati mwingine mpenzi wako alikuwa hafanyi kabisa vitu nilivyo taja
hapo juu hivyo akawa hajabadilika na ikawa ndiyo alivyo, lakini kama
alikuwa akifanya na sasa amebadilika basi kuna umuhimu wa kujiangalia
mapema, kuongea naye na kujua nini tatizo.
No comments:
Post a Comment