(1) Wanaume huchagua wanawake kama
vile mtu anachagua yeboyebo zilizotandazwa chini sokoni na kwa mwanaume
yeyote ataokota tu zile ambazo ziko karibu yake wakati mwingine hata
kama hazimtoshi. Lakini kwa mwanamke anayejitambua na anayejua thamani
yake atakuwa sawa na kiatu kizuri ambacho kimetundikwa dukani juu kabisa
tena kwenye duka la kioo ambacho hakipatwi hata na vumbi. Anajua
thamani yake hivyo atamfanya mwanaume amhangaikiekumfuata dukani na
kumchagua kwa heshima, hata jirahisisha na kuruhusu kutandazwa tandazwa
chini.
(2) Mwanamke anayejitambua anapaswa
kujua kuwa mahusiano yanachangamoto lakini angalau asilimia 8o ya muda
wenu muutumie mkifanya mambo yakuwapa furaha, kama mnatumia zaidi ya
asilimia ishirini ya muda wenu kugombana basi jua uhusiano wenu hauendi
popote, jitathimini kama unamhitaji huyo mtu au la?
(3) Mwanamke anayejitambua hujipenda
yeye mwenyewe kwanza kabla ya kumpenda mwanaume, hii ni kutokana na
ukweli kuwa, kama hujipendi hata kama ukipendwa vipi huwezi furahia
upendo huo.
(4) Mwanamke anayejitambua anajua
pia ni kitu gani anakitaka kwa mwanaume na anahakikisha anakipata. Kama
hujui unachokitaka kwake hata ukikipata bado utajihisi hujakamilika,
hembu jiulize sasa unataka nini kwenye mahusiano uliyonayo sasa.
(5) Mwanamke anayejitambua
halinganishi mahusiano yake ya sasa na yazamani, au mahusiano yake na
mahusiano ya rafiki yake. Huamua kuwa na furaha sasa bila kujali huko
nyuma maisha yalikuwaje, husahau yaliyopita na hahangaishwi na mambo
yanayofanywa na wengine.
(6) Mwanamke anayejitambua huchagua
aina ya mwaname anayemtaka na si kuchukua tu kila mwanaume kwakuwa tu ni
mpweke au anahisi umri umeenda.
(7)Mwanamke anayejitambua hujitoa
kimwili kwa mwanaume pale anapohisi kuwa yuko tayari kufanya hivyo na si
kwakuwa anaogopa kumpoteza mwanaume, kwani anajua thamani yake na
anajua kama mwanaume anamthamini basi hatajali sana kuhusu ngono bali
ataangalia upendo wa kweli.
(8) Mwanamke anayejitambua anafahamu
kuwa mwanaume si Baba yake, Kaka yake au Bosi wake bali ni rafiki yake,
hivyo atamheshimu lakini hatamuogopa na yuko tayari kuongea kuhusu
hisia zake. Kwakuwa anajua anachokitaka atamuambia mwenza wake na
kwakuwa ni marafiki basi kila mmoja atakuwa huru na mwenzake.
(9) Mwanamke anayejitambua anajua
kuwa mapenzi si maisha yake bali ni sehemu tu ya maisha yake, hawezi
kusumbuliwa na mwanaume kwakua tu anapenda kwani anajua yuko imara
vyakutosha kuvumilia upuuzi wa mwanaume yeyote. Ameiweka mbele furaha
yaake kuliko ya watu wengine na anapoona hapati anachokitaka basi
hujitoa mara moja kwenye aina hiyo ya mahusiano.
(10) Mwanamke anayejitambua hawezi
kupigania mwanaume kwani anafahamu kuwa mwanaume hachungwi na kama
mwanaume anampenda basi hawezi kuhangaika hangaika na wengine. Anafahamu
kuwa mwanaume anachepuka kwakuwa antaka na si sababu ya mwanamke
mwingine hivyo basi humaliza mambo yake na mwanaume wake na hapotezi
muda wake kugombana na mwanamke mwingine kwaajili ya mwanaume.
No comments:
Post a Comment