Wengi wa wasomaji wamemtumia meseji za kutaka kujua njia ya kupunguza
mafuta tumboni, wanawake kwa wanaume walituma maswali kwa wingi. Njia
iliyosalama ya kupunguza mafuta katika tumbo au kupunguza tumbo kubwa ni
ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.
Nilipata nafasi wiki hii ya kuzungumza na daktari mmoja katika hospitali
ya mkoa wa Iringa ambaye sitamtaja kwa jina na alikuwa na mengi ya
kuelezea jinsi hali hiyo inavyoanza na husababishwa ni nani.
Alisema kuwa,kama unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula
vyakula vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa
wingi.
Vyakula kama viazi mviringo, wali mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku
tatu, pia ulaji wa nyama nyekundu inasababisha kuongezeka uzito na pia
huongeza ukubwa wa tumbo,vyakulahivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi
kidogo sana.
"Kuna wakati tumbo linajitokeza na kuwa kubwa kuliko kawaida hali hiyo
inasababishwa na kula vyakula vya wanga kwa wingi, kutokunywa maji ya
kutosha na pia kula bila ya mpangilio maalum" anasema.
Anasema kuwa kama ntu anataka kupunguza mafuta au kuondoa kitambi
anatakuwa kula milo mitatu kwa siku na si kujinyima kula kwa kudhani
kuwa unaweza kupungua uzito.
"Vyakula vya wanga na mafuta ufanya mtu kunenepa, acha au kupunza kula
vyakula vyenye wanga ili kupunguza mafuta yaliyozidi mwilini, mafuta
yanaporundikana mwilini athari moja kubwa ni kuwa na tumbo kubwa."
anasema.
Anasema kuwa,tumbo kuwa kubwa ni dhahiri kuwa chakula unachokula
hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na ziada mwilini na hii ziada
inafanyika mafuta ambayo hujiwekesha akiba katika maeneo mbalimbali ya
mwili.
"Kwa kuwa Chakula hiki cha ziada huwa hakitakiwi, mwili hukibadilisha na
kuweka akiba katika mfumo wa mafuta kitaalamu kama glycogem.Unaweza
kukabiliana na kuzidi kwa protini zinazoyeyushwa na kuwekwa katika akiba
kwa mfumo huo wa mafuta"
Daktari huyo anasema kuwa, mtu mwenye tatizo hilo ni bora akapangilia
mlo wake kwa siku.
"Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana kama
kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika
hali inayotakiwa.
"Watu wengi wanatumia wanga mwingi wakati wa usiku muda ambao unaenda
kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi ya kujikusanya,
kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa
tumboni" anasema Daktari.
Je Mazoezi husaidia kupunguza uzito wa mwili na manyama uzembe?
Mazoezi ya viungo yamethibitishwa kusaidia kuchoma mafuta ya ziada
katika mwili.
Kutokana na hali ya ulaji unaweza kutengeneza manyama uzembe katika
kifua, mapaja na maeneo fulani ya tumbo ambayo yametengenezwa kupokea
maeneo ya ziada yanayotokana na mafuta yenyewe au sukari iliyobadilishwa
kuwa mafuta. Nishati inayotokana na nafaka ambayop haiwezi kutumika
muda huo hutengenezwa kuwa mafuta na kupelekwa eneo husika. Wanaume huwa
na asilimia 8 hadi 20 ya mafuta katika mwili na ni kawaida wakati kwa
wanawake ni asilinia 13 hadi 25.
Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni kwa wingi katika
mapafu yako na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa
nguvu kwa mwili.
Mafuta yanayounguzwa kwanza ni yale ya kawaida kabla ya kuingia katika
akiba. Kuna umuhimu wa kutambua kuwa mazoezi ni kitu cha bure na kama
ukifanya kwa mpangilio na vizuri hutakuwa na shida ya kutengeneza shepu
yako.
Dk.Martica Heaner,M.A, M.Ed. ambaye hutoa mawaidha ya keep fit ndani ya
MSN anasema ni jambo la heri kama mtu atakula kidogo kabla ya kuanza
mazoezi ili kutoa nishati ya kutosha ya kufanyisha mazoezi.
"Lakini kama unaenda mwendo fulani mdogo tu au unatembea kwa dakika 30
huenda usiwe na haja kabisa ya kula hata hicho kidogo na hasa ikiwa
uliweka kitu kiogo saa tatu zilizopita" anasema.
Tuesday, May 2, 2017
Namna rahisi na salama ya kupunguza tumbo
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment