Unalalamika,
unalaani, unalia na kunung’unika kila wakati na yamkini wala
hujajiuliza tatizo liko wapi? Alikuoa wewe ili apate msaidizi na sio mtu
wa kumfundisha vitu vya kufanya, kama angehitaji hilo basi angemtafuta
mwalimu. Alikuoa akiwa na kiu ya kupata msaidizi na mtu wa kushiriki
naye maisha “a companion” na sio mtu wa kumuongoza kama bosi, yeye
tayari ana bosi wake huko ofisini kwake, hahitaji bosi mwingine wa
nyumbani, labda hakwambii tu anavyosikia vibaya unavyomkalia kooni
katika kila kitu na katika kila maamuzi. Labda hakwambii tu lakini
hahitaji mtu wa kuwa kama mama yake kwenye ndoa wakati tayari ameshawahi
kuwa na mama, wala hahitaji mtu wa kumsimamia kama dada yake, tayari
dada zake walishaifanya kazi hiyo. Utaendelea kuumia na kuteseka sana
kiakili na hata moyoni mwako kama hautofika sehemu ukaitambua nafasi
yako kama mke na pia ukaitambua na kuiheshimu nafasi yake kama mume.
Usikopi na kuigiza jinsi mama yako alivyokuwa anahusiana na baba yako,
yamkini mama yako alikuwa anakosea na kutojua uhalisia, na labda baba
yako aliamua kuwa kimya ilikuepusha shari muda upite, usidhani kwa wao
kuwa pamoja muda mrefu ndio walikuwa wameshibana, fahamu uhalisia na
ukweli huu na ikusaidie kuyatengeneza mahusiano yako na mumeo kwa staili
na mtazamo bora. Kumbukwa kwamba wakubomoa ni wewe, na wakujenga ni
wewe pia. Akili mukichwa – Chris Mauki
Wednesday, May 17, 2017
NI BORA UKAFAHAMU KABLA HAUJATESEKA SANA
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment