Mara
nyingi ni rahisi sana katika mahusiano mkajikuta mnashindwa kuyaongea
na kuyamaliza yale yanayoleta misuguano na ukakasi katika mapenzi yenu.
Yamkini hamyaongei mkayamaliza kwasababu mnaogopa milipuko, yamkini
mnaogopa kupelekea mpasuko au uwezekano wa kuachana, yamkini mmoja
anamuogopa mwenzake kwa namna anavyokuwa mkali au mbishi. Kwa vyovyote
vile, matatizo baina ya wapenzi yasio ongelewa na kumalizwa na kuwafanya
wapenzi kurudi kwenye amani na upendo ni hatari sana. Pale
yanapofunikwa na wapenzi kudhani kwamba wamepooza moto, hatari yake
nikwamba taratibu hupunguza ladha ya penzi, hupunguza mvuto baina ya
wapenzi “intimacy”, kidogo kidogo mnaanza kuchokana, kidogo mnaanza
kuangaliana kama mtu na jirani yake na sio mtu na mpenziwe, na
msipoangalia au kuwa macho kila mmoja anakosa hamu na hamasa na
mwenzake, na hivyo kuweka urahisi wa kutengana. Jifunzeni kuwa na
ujasiri wa kuyaongea, jifunzeni kuwa na ujasiri wa kuyaweka mezani na
kuhakikisha mnafikia ufumbuzi wa yale yanayowatatiza. Furaha ya kwenye
penzi huwekewa mazingira, na haioti tu kama uyoga, au kushuka tu kama
mvua – Dr. Chris Mauki.
Wednesday, May 17, 2017
JIFUNZENI KUYAMALIZA SIO KUYAFUKIA
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment