Tafiti zinaonyesha kwamba wanawake wameumbiwa ndani yao ujuzi wa asili wa namna gani mahusiano yanatakiwa yawe, namna
gani ndoa inatakiwa iwe na pia familia na malezi yaweje, wao hawahitaji
sana mafunzo na kama mafunzo yanakuwepo basi nikuongezea kile
walichonacho tayari. Wanaume wao huhitaji kusaidiwa kujua namna ya
kuishi kwenye mahusiano, ndoa na hata namna ya malezi. Kusaidiwa au
kufundishwa huku huanzia toka kwa wazazi wa mwanaume huyu na mara
nyingine hata mke wake huwa na maeneo ya kumfundisha na kumsaidia zaidi
pia. Iwapo mwanaume hakupata nafasi ya kujifunza, kufundishwa toka kwa
wazazi la labda hayuko tayari kufundishwa au kuelekezwa na mke wake basi
anaweza kuwa mtu mbovu sana na wenye kuudhi katika mahusiano na mambo
ya familia. Wake zetu, msisite kutufundisha, msidhani tunajua kila kitu,
msipotufundisha na kutuelekeza kiukweli mtatuchukia. Na sisi wanaume
turuhusu kufundishwa, kuelekezwa na kuwa watii katika kujifunza. Wote
wawili ni wadau tulio na hisa sawa katika kuhakikisha tunayafurahia
mahusiano yetu, hakuna bwana wala mtwana – Chris Mauki.
Wednesday, May 17, 2017
Home
/
Unlabelled
/
WEWE MWANAUME, HUO UGUMU NA KUTOTAKA KUELEKEZWA KITU NA MPENZI WAKO KUNATOKA WAPI??
WEWE MWANAUME, HUO UGUMU NA KUTOTAKA KUELEKEZWA KITU NA MPENZI WAKO KUNATOKA WAPI??
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment