Mitandao ya kijamii imewafanya baadhi ya watu kuwa na ‘uteja’ ambao hupelekea kupata hasara kubwa katika maisha yao ya kila siku, huku wanaoitumia vizuri wakiendelea kufaidika na mapinduzi makubwa ya sayansi ya teknolojia.
Askari mmoja wa kike nchini China amekumbwa na fagio la kutumbuliwa jipu baada ya kupost picha ‘selfie’ kwenye mtandao akiwa amevaa sare za jeshi la polisi nchini humo kwa namna isiyofaa.
Afisa huyo ambaye ni mrembo kweli (jina lilihifadhiwa), alipost picha akiwa na vazi la juu huku chini akiwa amevaa kikaputula kifupi.
Kwa mujibu wa People’s Daily Online kitengo cha Usalama wa Umma cha jimbo la Liaoning, afisa huyo amelishushia heshima jeshi hilo kutokana na post yake hiyo.
Nchini Tanzania, Maafisa wawili wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani waliwahi kufutwa kazi baada ya picha zao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na sare za jeshi hilo wakipigana mabusu.
No comments:
Post a Comment