Binti mmoja mwenye umri wa miaka 21 amemfanyia unyama mwanaume aliyekuwa mpenzi wake kwa kumchinja kisha kumnyofoa moyo wake kutokana na wivu wa mapenzi.
Jumanne iliyopita, Mahakama nchini Bangladeshi ilimhukumu kifo mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Fatema Akhter Sonali baada ya kukiri mahakamani hapo kuwa alitekeleza mauaji hayo.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Quazi Shabbir Ahmed aliliambia shirika la habari la AFP kuwa Sonali alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa licha ya mpenzi wake kukataa kumuoa, alikuwa ameendelea kutunza kwenye laptop yake vipande vya video vinavyowaonesha wawili hao wakifanya mapenzi. Lakini pia, aliona video nyingine za mwanaume huyo akifanya mapenzi na wanawake wengine.
“Alikiri Mahakamani kuwa alimuua mpenzi wake, Emdadul Haq Shipon kwa kukataa kumuoa na kwa kutunza video za wawili hao wakiwa wanafanya ngono, kwenye laptop yake [ya marehemu],” alisema Mwendesha mashtaka huyo.
Alisema kuwa ingawa ni nadra sana kwa Mahakama za nchi hiyyo kumhukumu kifo mwanamke, kosa la mwanamke huyo lilikuwa la aina yake hivyo Mahakama ililazimika kumpa hukumu ya kifo.
Akisimulia jinsi alivyoweza kutekeleza unyama huo, Sonali alisema kuwa alimnywesha vinywaji vikali alivyochanganya na vidonge 20 vya usingizi, na baada ya kulala alimfunga mikono na miguu kabla ya kuanza kumchinja na baadae kunnyofoa moyo.
No comments:
Post a Comment