Inawezekana ukawa umesoma sana na ukawa unamiliki vyeti
mbalimbali vya kitaaluma lakini mpaka sasa maisha yako bado unaona hayaendi
sawa sawa kama unavyotaka au inawezekana pia ukawa umebarikiwa akili na maarifa
ya kutambua mengi lakini mpaka sasa huna lolote unaloona ni faida kwako zaidi
ya maisha kuendelea kuwa magumu kwa upande wako na huku wengine wakipanda juu
na kukuacha ukiwashangaa kana kwamba hukuwa nao hapo mwanzo au kana kwamba wao
ndio wenye akili nyingi kukuzidi.
Usikate tamaa wala kujiona huwezi. Kitu cha muhimu hapa ni
kujitambua kwanza na kufahamu nia hasa ya Mwenyezi Mungu kukuleta hapa duniani.
Binadamu ulipoumbwa na Mwenyezi Mungu na ukaletwa hapa duniani hukuletwa kuja
kuteseka au kuja kuwa msindikizaji wa wengine ambao waliumbwa kama wewe
ulivyoumbwa.Uliletwa kwa makusudi maalum na kila dakika unayoishi hapa duniani
kumbuka hairudi tena na ikishaenda imeenda.
Kwa hiyo unapokuwa unataka kukata tamaa kwa kushindwa
kutimiza lengo Fulani kwenye maisha au kwa kufeli shule,kufeli biashara, kufeli
kwenye mahusiano/mapenzi, kufeli maisha, kufeli kupata kazi, kufeli kwenye
kilimo au hata kufeli kiimani, unapaswa kwanza kutambua lengo la Mungu kukuleta
hapa duniani.Hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kuwa umeletwa duniani kuja
kufeli.hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kuwa umeletwa duniani kuja kuangalia
wengine wakisonga mbele na wewe ukirudi nyuma.
Mungu Ni Mwema Siku Zote, Humpa Kila Mtu Sawasawa Na Mapenzi
Yake, Ukishindwa Sehemu Moja Ya Maisha Jaribu Sehemu Nyingine Utaweza Tu,
Hakuna Aliyeumbwa Kukosa, Unaweza Tena Sana, cha kufanya ni kujiamini
tu.Ukijiamini kama unaweza basi hakuna kitakachokuwa kigumu kwako, usijipe moyo
wa kushindwa hata siku moja. Ukikata tamaa tu kila siku utakuwa mtu wa kulia na
kujuta na mafanikio kwako yatakuwa magumu sana kupatikana.
Na Hata hayo Matatizo Uliyonayo
Ni Ya Muda tU, Mwenyezi Mungu Kakuumba Kwa Makusudi Yake, Jipe Moyo Utayashinda,
Yana Mwisho, Unapopata Majaribu Usihuzunike Wala Kukata Tamaa,Mwombe Mungu
Atakusaidia huku ukitafakari njia sahihi za kutatua na kama ukishindwa kupata
utatuzi wewe mwenyewe usione aibu kuomba msaada kwa wengine.
Kuwa Kilema,
Yatima, Mjane, Mfungwa, Mkimbizi, Mgonjwa, Masikini, Na Kadhalika, Kusikufanye
Uishi Kwa Majonzi, Unyanyasike Na Kukata Tamaa, Bado Unavuta Pumzi , Inamaanisha
Bado Unaweza Kubadilisha Huzuni Kuwa Furaha, Mwite Mwenyezi Mungu Akuongoze
Kuanzia Sasa, Hautajuta Wala Kujiona Huwezi. Wangapi ni vilema na wana
mafanikio kuliko wazima?, wangapi waliachiwa familia na wake/waume zao baada ya
kufariki au kwa kukimbia majukumu lakini leo hii wana mafanikio makubwa tu??!
Tunachojifunza hapa ni Kutokata Tamaa na Kujiamini.
Na kitu
kingine cha muhimu kwenye maisha ni uwezo wa kufanya maamuzi bila kuyumba. Unapoamua
Kufanya Maamuzi Na Ukawa Na Uhakika Kama Maamuzi Hayo Ni Sahihi Basi Hutakiwi
Kuogopa, Maisha Ni Yako Na Hutakiwi Kuwa Muoga, Usiogope Majirani Na Wengine Watasema
Nini, Haohao Wanaokusifia Leo Ndio Haohao Watakaokucheka Kesho Ukianguka, Be
Positive With Your Feelingz/Jiamini. Na Usitegemee Sana Nguvu Zao
Kufanikisha Malengo Yako, Wengi Wao Wapo Nawe Mdomoni Tu Lakini Moyoni Wapo
Sehemu Nyingine Kabisa, Pigana Kwa Nguvu Zako Mwenyewe Kama Unataka Mafanikio
Yawe Upande Wako, Usiamini Mtu Isipokuwa Mungu Pekee.
Kitu cha mwisho kukiangalia kwa wewe unayeona maisha
hayakuendei poa kwa sasa ni kuangalia aina ya marafiki ulionao. Ukiona
Umezungukwa Na Marafiki Na Ndugu Wengi Na Wenye Uwezo Wa Kukusaidia Kutoka
Kimaisha Lakini Kila Siku Maisha Yako Yakawa Yanashuka Badala Ya Kupanda…Basi
Huna Budi Kutazama Upande Mwingine, Urafiki Ni Kusaidiana Na Si Kufurahia Pale
Unapoanguka Ili Kila Siku Uwatukuze Wao Tu, Haina Maana Kujuana Na Fulani Halafu Hupati Faida Yoyote.
Kufanikiwa kumewekwa kwa kila mtu hapa duniani bila kujali
umri au dini. Usiangalie una umri gani sasa na usiangalie umetokea familia gani
wala mazingira ya sehemu ulipo wala elimu uliyonayo, unaweza kufanikiwa kama
utaambatana na waliofanikiwa na kuachana na maneno ya waliokata tamaa za
maisha.
No comments:
Post a Comment