Katika
mahusiano yawezekana kabisa vile vitu au kile kilichokuvutia kumkubali
mpenzi wako na kuamua kuwa naye maishani baada ya muda fulani wa maisha
ya pamoja kitu hicho au vitu hivyo vikawa kikwazo cha kukushinikiza
kutamani kutoka nje ya ndoa hiyo, kwa mfano, ulipenda kumwona anavyo
kupenda na kila saa akitaka kujua aliko, unafanya nini, nanani, wewe
ukadhani hayo yalikuwa mapenzi, ukashindwa kujua kuwa huo ulikuwa wivu
wa kawaida tu na sasa wivu huo umezidi, umekomaa, umeota mizizi na
umekufanya unashindwa kustahimili kwa jinsi anavyo kubana pumzi kama
kiranja wa shule ya msingi na unatamani kuachana naye. Mfano wa pili,
pesa nyingi alizokuwa anakupa kabla hamjaoana, ulizifurahia sana na
kuona kuwa umefikia mwisho wa matatizo yako, wewe ulitafsiri kuwa hilo
ndilo penzi na huyo ndiyo mwanaume anayejali, sasa pesa hizo
zimeongezeka, badala ya furaha nayo kuongezeka kwenye mahusiano yenu,
kila siku unakerwa na kiburi chake cha pesa, siku hizi anahonga wanawake
kama alivyokuhonga wewe miaka hiyo. Sasa hapa unaona wazi ya kuwa
ulichokipenda na kikakuvutia kuingia ndani ya penzi sasa kitu kile kile
kinakushinikiza kutoka nje. Jifunze kuwa macho na makini sana katika
vile vinavyokuvutia kuingia kwenye mahusiano ili kupunguza majuto mengi
ya kesho. Usisahau, “what goes around, comes around” – Chris Mauki.
Wednesday, May 17, 2017
VILIVYOKULETA NDANI YA PENZI SASA VINAKUTOA NJE
About Unknown
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment