Vijana wengi wa kiume hujikuta katika
wakati mgumu kuchukua maamuzi ya kuishi na mwanamke japo yawezekana
wakawa wanatamani kufanya hivyo kwa muda mrefu kutokana na vikinza
vingi, vingine vikiwa ni vya kimaisha na vingine ni nadharia tu.
Katika bandiko hili, nitagusia sababu kadhaa zinazochangia vijana wengi kujikuta wakisuasua au kuogopa kuingia kwenye ndoa.
Kupanda kwa gharama za maisha
Kigezo hiki huwakumba zaidi wanaume ambao
wanaishi mijini. Gharama za maisha zimepanda sana kiasi kwamba mtu
anaweza kuwa anaishi peke yake na bado kuna mambo ambayo anashindwa
kuyatimiza kwa wakati, kama vile kozi ya nyumba, pesa ya kujikimu na
mengine mengi. Wengi huona ni heri kuwa na mtu tu ambaye ni mpenzi wake
kuliko kudhibiti kabisa kwa kuwa na huyo mtu kwa kuishi naye kwa hofu ya
kushindwa kutimiza wajibu. Ndio maana kwa wale ambao hupata akina dada
ambao wanajiweza kujitegemea na hivyo ni hodari kwa kusaidiana katika
mambo ya kila siku hasa katika masuala ya maendeleo huwa wepesi kuchukua
maamuzi ya kuoa.
Utitiri wa wanawake wanaopatikana kirahisi bila hata kuoa
Ni suala ambalo lipo wazi hasa maeneo ya
mijini akina dada/mama wa kuwa nao katika mahusiano (bila kujalisha ni
wa muda mfupi ama mrefu) wamekuwa wengi, rahisi kuwapata, wa kila aina
mwanaume watakao. Kuna wanaume wamejikita katika hilo kiasi kwamba
mradi tu atake mwanamke atatoka/atatumia namba alizohifadhi kwenye simu
na atafanikisha hiyo azima yake ndani ya siku hiyo hiyo ambayo
amedhamiria bila shida yoyote. Hii inafanya kwa kiasi kuchangia kwa
wanaume kusuasua katika maamuzi ya kuoa. Kwa kimombo hujiambia, “If I
can get it for free, why buy it?”
Maradhi hasa ugonjwa wa UKIMWI
Pamoja na kuhamasishwa kwingi na
wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDs kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza
kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana
kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo,
hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto. Wengi sana hukata tamaa na
huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa. Naomba
izingatiwe kuwa si wote; wengine huwa hodari na huoa/olewa saa nyingine
bila hata kumjulisha mpenzi wake huyo kuwa yeye ana virusi chanya vya
UKIMWI (HIV +ve).
Kufurahia ‘uhuru’
Hawa ni makapera wazoefu (wengine husema
‘bachela sugu’), hakuna mtu ambaye anaweza mshawishi akabadilisha maisha
yake hayo ya kikapela (bachelor). Miaka huzidi kukatika hadi anafika
miaka takribani 40 au zaidi wala hana mpango wa kuoa na wala hajutii
maamuzi yake hayo. Mara nyingi wanaume wa namna hii hupenda sana
wanawake (siyo lazima kuwa atawachanganya kwa kuwa na zaidi ya mmoja);
huwa na uwezo (hata kama sustainable); Hutaka wanawake wadogo (mtu mzima
sana kwake hapana hata kama yeye ni mtu mzima); Ni mtu wa starehe sana,
haoi kamwe na hufurahia uhuru huo kwa hisia kuwa akioa ataupoteza uhuru
wake.
Uhaba wa wanawake wanaofaa kuolewa
Na hii hutokea hasa kwa maeneo ya mijini.
Wadada/mama wengi wamekuwa ni ‘wa mjini’ mno, wajanja, malengo mbele
ikiwa imeambatana na tamaa, wanaoweka pesa mbele utu nyuma, wachanganyi
(kuwa na bwana zaidi ya mmoja). Haya mambo yamekuwa yakifanywa bila
kificho, inamfanya mwanaume anapokuwa katika mahusiano ahisi kuwa hata
mtu wake ana tabia hizo hizo hata kama siyo kweli. Hii inakatisha tamaa
kwa wanaume wengi na kuona wanawake wanaofaa kuoa (tokana na viwango
vyake alivyoweka) ni adimu ama hawapo kabisa!
Kutopata ampendaye kwa dhati
Kuna wanaume vigezo vya mwanamke awe vipi
havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuoa. Yeye kikubwa anataka
ampate mwamake ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na matumaini
kuwa huyo mwanamke atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu mwanaume
anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mkewe
basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanamke akampenda. Kama huyo
mwanamke atakubali kuolewa ama lah; hilo ni suala jingine!
Mahusiano mabovu ya awali
Kuna wanaume huchagua wanawake kwa sifa
ambazo anazijua yeye mwenyewe. Yeye hamuangalii mwanamke kama mtu, bali
anamuangalia kama kitu. Daima vigezo vyake ni nataka mwanamke wa hivi,
tabia za vile, muonekano wa kule na mambo mengine kedekede. Hivyo
unakuta kila siku yuko katika mahusiano na mwanamke ambaye ni kweli
anampenda kimuonekano; ila linapokuja suala la tabia wanashindwana
kabisa. Anaachana nae kisha anatafuta mwingine kwa mtindo uleule –
mwisho wa siku analaumu wanawake wote ni sawa na kukata tamaa ya kuoa
ama kusuasua katika maamuzi ya kutaka kuoa.
Kutoridhika na kipato chake
Kuna mwingine anaweza kuona kutoridhika
na kipato (ni sawa na sababu ya kwanza niliweka ya “Kupanda kwa gharama
za Maisha”) – lakini hii ni tofauti kidogo. Hapa namaanisha pale ambapo
mwanaume ana uwezo kabisa wa kuwa na mke na pia kuweza kukimu mahitaji
yote pamoja na ya familia yake. ILA kwa mipangilio yake anaona yeye
bado; mara nyingi wa hivi anataka ahakikishe ana uwezo wa kutosha ili
aweze kuishi maisha ya kifahari na si ya kujitosheleza tu. Hivyo katika
hali ya kawaida ana uwezo wa kuwa na mke lakini kwa maisha ya mtu wa
kawaida na si wa kitajiri kama malengo yake.
Malezi na Makuzi
Dhana mbovu juu ya ndoa
Dhana ya ndoa inaenda ikibadilika…
Kumekuwa na tabia ya watu kukatisha tamaa kwa kutoa vigezo, sababu,
hadithi juu ya ndoa ambazo ni za kubomoa kuliko kujenga. Sijui hawa watu
hutumia vigezo gani… HATA siku moja usitarajie uishi na mtu miaka nenda
miaka rudi kitanda kimoja, nyumba moja msigombane, kusiwe na madhaifu
na pia kusiwe na wakati ambao wote hadi kiwango cha kukata tamaa. Ndoa
ni zaidi ya starehe na kufurahi… Inahitaji nguvu kubwa, nguvu ya ziada,
hekima, busara, kujituma na pia kuwa committed kwa ndoa kuweza kufanikiwa. Sisemi kuwa lazima zote zitafanikiwa maana kuna mambo ambayo yana mpaka – kuna wakati you just let go.
Ila hakuna haja ya kuibomoa hiyo taasisi kwa makusudi, taasisi ambayo
ni msingi bora wa malezi ya watoto kuliko taasisi yoyote ile inayoweza
lea watoto ambao hasa ndiyo tegemeo la vizazi vijavyo.
Kuzaa ovyo/Kuzaa kabla ya ndoa
Kuna wanaume wanazalisha balaa! Bila
kujalisha hizo mimba ni zao kweli ama wamesingiziwa kinachojalisha na
watoto hao kawakubali na anawalea. Kuna wanaume hadi anafikia umri wa
miaka 30 tayari ana watoto wa wanawake tofauti hata watano na analea.
Kwa kiasi fulani, hii inaweza mvunja morali ya kutaka kuoa, anaona kama
watoto tayari anao na anawalea hivyo hakuna haja ya kuwa na mwanamke
kabisa ndani kama mke. Hii ni mara chache.
Kukua kwa idadi ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa
Maadili mengi ya wanandoa yamezidi
kushuka… Hapo nyuma ilishazoeleka wanaume huwa na tabia ya kutoka nje ya
ndoa na wanawake kwa uchache. Bahati mbaya siku zinavyozidi kwenda
idadi ya wanawake wanaotoka nayo inakuwa kwa kasi, tabia ambayo
inafanywa bila kificho kabisa na imekuwa kana kwamba ni mashindano ya
kutoka. Ni wazi thamani (reputation) ya mwanamke ambaye anatoka na
mwanaume anayetoka ni tofauti. Ni wanaume wachache wana kifua cha kuweza
kuvumilia mkewe/mpenziwe kutoka nje na kuendelea kuwa naye. Kwa wanaume
wengi ambao hawajaoa hili huchangia katika kukata tamaa ya kupata
mwanamke ambae anafaa kuwa mke na asiyeweza kuwa msaliti.
KAMA HUAUTUMII VYAKULA HIVI NGUVU ZA KIUME UTAZISKIA REDION
No comments:
Post a Comment