Msomaji, nimeona vema nishirikiane nawe
katika hii hoja ya kujiachia kwa miili yetu katika kufanya mapenzi na
wapenzi wetu. Hapa ninaposema kujiachia sina maana kujiachia wakati wa
faragha kufurahia tendo… Bali nazungumzia kujiachia kwa bahati mbaya ama
makusudi na kutojali ama kuzingatia ni idadi ngapi ya watu
unashirikiana nao iwe kwa siku, juma (wiki), mwezi ama hata mwaka.
Suala lililopo hapa (hasa kwa akina
mama/dada) wengi hujiweka katika kundi la kutokujiachia ovyo. Kwako
msomaji naomba tulia na jitafakari ukiwa mkweli kwa nafsi yako kama upo
kundi hili la kujiachia.
Kujiachia kupo tofauti, kuna kujiachia
unakuwa na mpenzi mmoja mmoja lakini hadumu zaidi ya miezi mitatu hivyo
kukufanya uwe umelala na walau watu 4-6 kwa mwaka (hivo kama ulianza huo
mchezo kaika umri wa miaka 17 na upo miaka 25 ina maana umeshawahi lala
na wanaume si chini ya 25). Pia kuna kujiachia kwa kuchanganya wapenzi
ama kutoka nje ya mahusiano ya mpenzi/mwenza wako. Huku kutoka kama ni
kubadilisha kila siku huko nje ndiyo kujiachia kwenyewe na nafuu huwepo
kwa yule ambaye ana-maintain mtu huyo anayetoka naye. Hata hivyo
tuangalie sababu ambazo hutufanya tujiachie ni zipi…
Sababu za Wanawake na Wanaume Kujiachia
Kuwa na Mpenzi asiyemridhisha,
inaweza tokea mtu ana mtu wake anampenda sana na wapo pamoja kama
couple ila hatosheki kabisa wanapokuwa faraghani. Siku za mwanzo
atajitahidi kuvumilia, ila inapotokea tayari starehe ya kutaka
kufikishwa imemvaa, aweza jikuta akajiachia kwingine.
Kuwa na tamaa ya vitu hivyo
kujiachia kwa kuhongwa kama namna ya kupata alicholenga. Hii ilikuwa
sana kwa wanawake, ila tokana na kushuka kwa maadili kasi inaongezeka na
kwa vijana wa kiume pia. Anaweza kuwa na mpenzi wake ama wapenzi wengi
kwa ajili ya kuwa na machimbo tofauti ya kupata pesa ya kujikimu tamaa
zake za vitu. Kwa vijana mara nyingi hutolewa na wamama maarufu kama
Jimama.
Kuwa desperate sana na kutoweza ishi bila Mpenzi, kila
anapoachika mara kishampata mwingine. Kuna kundi la watu hawawezi
kabisa kuweka nafasi (gap) kubwa kati ya mpenzi wake ambaye kaachana
naye na mpenzi mpya. Hii husababisha mhusika kujikuta yupo katika
mahusiano na mtu ambaye hamfai na hivyo kuachika na kutafuta tena.
Mwisho wa siku ndani ya mwaka wapenzi siyo chini ya 6.
Kuwa addicted kwa ngono (Hii
ni wachache kwa wanawake na wengi wa wanaume) Huyu mtu anataka kufanya
ngono mara kwa mara. Inapotokea mtu mpenzi wake hayupo atajitahidi kwa
kila namna atafute mbadala ili kujiridhisha.
Kuwa tu na hulka ya Umalaya/Uhuni. Anakuwa
kishazoea kuwa na wapenzi wengi… Hawezi kuwa na mpenzi mmoja, hawezi
tulia katika mahusiano, kila siku kutafuta sababu za kuwa na mtu zaidi
ya mmoja. Na huona kuwa hiyo ni part ya maisha yake na kuwa afanyalo ni
sawa.
Ushawishi wa makundi… Inaweza kuwa kama mzaha na wengine wakadhani kuwa mtu mzima huwa na akili yake independent katika
maamuzi. Kwa mtazamo wangu, makundi yanachangia sana kwa baadhi ya watu
kujenga tabia ya kujiachia na kuona ni sawa hali awali asingeweza
thubutu.
Ngono kuwa ndicho chanzo cha kipato cha
kila siku, hii ni kwa wale ambao ngono hutumika siyo tu kwa starehe.
Ngono huwa ni chanzo cha kipato… Makundi yametofautiana, kuna wale ambao
ni wa hali ya juu na huchaji kwa bei za juu na pia kuna wale wa viwango
vya chini na viwango vya chini pia wote tegemeana na maeneo
wanayopatikana.
Kutojitambua na hivyo kuwa na huruma sana ya
kumfanya kutoweza kabisa kukataa akiombwa tunda lake. Hii ni kwa
wanawake ambao hawawezi kabisa kusema ‘NO’. Hata kama hamtaki huyo mtu
yeye humuonea huruma na kuona ni kheri tu akamalizane naye akamsaidie
haja zake.
Kuwa na kilevi katika maungo ya watu wawavutiao.
Mfano kuna mwanaume akiona mwanamke mwenye makalio makubwa
anachanganyikiwa kabisa na hujitahidi kwa kila namna ampate huyo
mwanamke. Kama vile baadhi ya wanawake wanavyoweza changanyikiwa kabisa
na kifua, sura ama hata sauti ya mwanaume to the extent atajitahidi kwa kila namna kuweka mazingira ya huyo mwanaume amtongoze ili atimize kiu yake.
Kwa wanaume zinaongezeka;
Kuongeza kujiamini (confidence) na
Ufahari kuwa yeye ni mwanaume kamili na lijali – Cha kusikitisha hapa ni
kuwa siyo wanaume wote ambao wanalala ovyo wana uwezo wa 6/6. Ila
sababu mara nyingi wanawake tumejenga utamaduni wa kujificha hisia za
kweli wakati wa tendo, wengi sababu ni wa kupita tu kwa huyu mwanaume
humezea tu rohoni kwa uwezo wake mbovu katika uwanja huo wa faragha…
Hasa kama ana pesa ndiyo kabisa!
Madhara ya Kujiachia kwa Wanawake na Wanaume pia…
Madhara kwa Ujumla wake – Wanawake
madhara ni makubwa zaidi ya wanaume… It is not fair, ila ndiyo ukweli
wenyewe! Kwa mwanamke kubadilisha wapenzi mara kwa mara, kuwa na wapenzi
zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja na ikajulikana wazi, kutoka nje ya ndoa
kwa kiasi kikubwa sana humbomolea heshima mbele ya jamii na cha ajabu
zaidi kwa wanaume wenyewe! Kitendo kama vile mwanamke kuwa katika kundi
la wanaume ambao zaidi ya mmoja wameshawahi lala naye na inatambulika ni
wazi kuwa maongezi kila ugeuzapo mgongo huwa siyo mazuri juu yako.
Maisha yamebadilika sana na tokana
pengine na mazingira na kukosekana na wanaume ambao wana sifa ya kuwa
wanaume inaweza changia kwa kiasi kikubwa mahusiano kutofanikiwa.
Kimsingi inatakiwa umakini, hekima, subira ya kuweza kupata mtu ambaye
anakufaa kuwa mtu wako kwa muda mrefu. Ni rahisi kusema na ngumu kutenda
lakini inawezekana.
Bahati mbaya saana ni kuwa kuna baadhi ya
wadada huona kama mzaha na kuona kuwa kuna viwango (standards) vipo
sawa katika kumtazama mwanaume ambaye anabadilisha girlfriends mara kwa mara kama vile yeye ambavyo hubadilisha boyfriends mara
kwa mara. Lakini with time hukua na kupevuka akili na kutambua kuwa
hailipi…. Ama huamua kujilipua hadi utu uzima kwa kujua kuwa kama damage
ishafanyika.
Pamoja na kuwa kunaweza kuwa mwanaume na
mwanamke wenye sifa sawa kabisa katika kujiachia katika ngono;
reputation ya hao watu katika jamii ni mbili tofauti. Na hata mwanaume
akilaumiwa kama amekithiri atalaumiwa siyo kwa kuwa na wanawake wengi,
bali kwa kutembea ovyo ovyo hata na wale ambao wanamchafulia tu jina na
sifa zake.
Madhara Mengineyo:-
- Inaweza leta kutokujiamini kwa mhusika hasa kwa wanawake… Kila mara kujichunguza kasoro alizo nazo na kujiona kana kwamba ana nuksi ya kuachwa mara kwa mara. Na kama ni mzuri hili ndiyo humchanganya kabisa na kuweza kujikuta yupo kwa mganga na hali mchawi ni yeye mwenyewe.
- Inaweza leta tafrani kwa wale ambao wamechanganywa watakapo tambua kuwa wamechanganywa. Kuna wengine hupata hasa cha moto, na wengine huponea chupu chupu kudhurika tokana na tabia hizo.
- Kuvunjika kwa ndoa. Hii ni mara nyingi mwanaume anapomfumaniya mkewe. Kwa wanawake wengi husamehe makosa ya kusaliti kwa waume/wapenzi zao kwa sababu zozote zile ambazo hubeba wao. Ni mara chache wake huacha waume zao sababu ya wao kuwa na wapenzi nje.
- Kuchuja kwa uzuri hasa kwa wanawake… Wadada/mama wengi hupungua uzuri wao hasa nuru katika sura zao.
- Kushuka kwa maadili. Wakubwa katika jamii wamekuwa wakichukulia suala la mahusiano kwa wepesi na saa nyingine kutozingatia mazingira na hadhira na kufanya baadhi ya mambo mbele za watoto wadogo wanaokuwa na kuiga tabia za kujihusisha na mapenzi.
- Kushuka kwa heshima ya mhusika kwa jamii iliyo mzunguka tokana na matendo yake hayo.
- Magonjwa hasa ya zinaa na kuzidi kuongezeka kwa kasi kwa HIV/AIDS.
No comments:
Post a Comment