Kama kichwa cha Habari kinavyojielezea mimi ni binti mrembo
tu Nina kaxi yangu nzuri Namshukuru Mungu, nimepita kwenye mahusiano
kadhaa changamoto hazikosekani Nimekutana na wenye uwezo wanaoweza
kanipa Nitakacho na wenye uwezo wa kawaida tu.
Nilichojifunza ni kwamba Unaweza kuwa kwenye mahusiano na
mtu Anaejiweza akakupa kila utakacho ila hana muda na wewe hamna out
wala muda wa kukaa mkayajenga hata mazungumzo ya kawaida maana mimi ni
mpambanaji
Mkikutana ni show basi siku zinaenda mwaka umekatika hamna
la maana na sio kwamba anamahusiano mengine Hapana ingawa Mwanaume
huwezi msemea ila ni mtu ambaye uko nae huru ila yuko busy muda wote
hawezi kujenga muda kwa ajili yako ila muda wa kufanya mengine kama
kwenda Bar, karaoke nk anao
Pili Mwanaume Ambae hawezi kukuhudumia kwa chochote mnapata
muda wa kuzungumza kushauriana kupanga Mambo ya maendeleo ingawa
hamuwezi kwenda out nk kutokana na kipato ila mapenzi mnayafurahia hata
kwa kukaa ndani tu coz mimi sio mtokaji na haijawahi kunipa chochote
wala sijawahi kumuomba coz namjua Hali yake
Ingawa ana wasiwasi na mimi kutokana na uwezo wake na
urembo wangu ila mimi sina tatizo coz najimudu kwa kila kitu. sasa huyo
mwenye uwezo miezi4 hatuko vizuri na naona nimeshindwa mimi kwa moyo
mweupe coz sijawahi kuenjoy nae hata siku moja nataka kumpokea huyu wa
Hali ya kawaida kwa moyo mmoja tujenge familia maana kule naona utumwa
naombeni Ushauri ndugu zangu
No comments:
Post a Comment