Mpenzi msomaji wa Maishahalisi leo nimekuandalia elimu inayohusu mambo
ya uzazi hususani kwenye suala la tatizo mimba la kuharibika na
tutagusia baadhi ya dalili ambazo zinaweza kumpata mwanamke anayeweza
kukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba kwa ufupi sana ilikukupa
uelewa wakuchukua hatua mapema unapoona hali hiyo.
DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)
- Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba.
- Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito.
- Dalili nyingine kubwa ni uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo {miscarriage}.
Maumivu makali ya tumbo, wakati mwanamke anapokuwa ni mjamzito lakini
wakati huo huo anapatwa na maumivu makali ya tumbo ya mara kwa mara
yakiambatana na maumivu ya kiuno pamoja na kutokwa na damu nyepesi au
nzito basi ujue ujauzito wako uko kwenye hatari ya kutoka, ni vizuri
ukawasiliana na kituo cha karibu cha afya au ukawasiliana nasi kwa
matibabu zaidi.
VYANZO VYA KUHARIBIKA KWA MIMBA {Miscarriage}
Vyanzo vikubwa vya kuharibika kwa mimba ni kama vifuatavyo;
1.Chromosome abnormalities,
mimba nyingi ambazo huharibika hadi wiki ya ishirini husababishwa na
tatizo hili la chromosomes, na chromosomes huwa zinabeba genes ambazo
huyatambulisha maumbile ya mwanadamu kwa nje, yaani jinsia yake, ngozi
yake itakuaje, macho yake na vitu vingine vingi nisingependa tuingie
ndani sana lakini matatizo haya ya chromosomes huchangia sana kuharibika
kwa mimba.
2.Maambukizi katika mji wa uzazi wa mwanamke {Infections}
kuna kitu kinaitwa Pelvic Inflammatory Diseases {PID} yaani kuvimba kwa
kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi nayo pia huchangia
sana kuharibika kwa mimba kwa mwanamke, lakini pia Candida au fangasi
nazo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba.
3.Chanzo kingine kikubwa ni utoaji wa mimba
Utoaji wa mimba wa mimba za mara kwa mara, wanawakie au wasichana wenye
tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao pia hukutwa na
tatizo hili la kuharibika kwa mimba kwani uingizaji wa vyuma ndani
huweza kuharibu Tazama piaTatizo la maumivu wakati wa tendo la ndoa shingo ya kizazi ya mwanamke na pia kukumbwa na tatizo hili la miscarriage au kuharibika kwa mimba.
4.Chanzo kingine kikubwa ni magonjwa ya zinaa {sexually transmitted diseases}
magonjwa kama gonorrhea, kaswende mara nyingi sana huathili mfumo wa
uzazi wa mwanamke na hasa hasa kwenye mji wa mimba na kuufanya kuwa
legevu na hata ujauzito unapotunga basi huweza kutoka kwa haraka zaidi
na hivyo kusababisha tatizo hili la kutoka kwa mimba {Miscarriage}.
5.Chanzo kingine cha mimba kuharibika ni tatizo la kisukari kwa mwanamke.
Hii nayo huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuharibika kwa mimba na mtu
ambaye hafanyi uangalizi wa karibu wa tatizo la sukari basi husababisha
glucose isitumike kama energy na hivyo kuleta madhara katika kizazi hasa
ujauzito.
6.kuvurugika kwa homoni
Kwa mfano hormone ya progesterone mara nyingi hufanya ile kazi ya
kutunza mimba iendelee kukuwa, na kama kunatokea kwa hormon imbalance au
kuvurugika kwa homoni hii basi mara nyingi tatizo hili la mimba
kuharibika hutokea.
No comments:
Post a Comment