Hadithi ya kusisimua
Mimi ni mwanamke mjane ninaishi mjini Arusha. Huu ni ushuhuda wangu wa maisha yangu.
Miaka 21 iliyopita nilifunga ndoa na mume wangu mpendwa kanisani,
baadaye tukajaliwa kuwa na watoto wa2 mmoja wa kiume Alfred na mwingine
wa kike Minza. Mimi nimesomea mambo ya uuguzi MD, nimefanya kazi muda
mrefu ktk hospitali za wilayani karatu na Arusha mjini mpk
nilipolazimika kuacha kutokana na udhaifu wa mwili na mambo yaliyonipata
katika maisha. Mume wangu alikua ni askari polisi mpk baadaye
alipojiunga na ajira zingine mpaka alipokutwa na mauti kama
nitakavyoeleza baadaye hapo chini.
Tulipooana na mume wangu,maisha yalikua ya furaha sana na tulikua na
mipango mingi mizuri ya kujiendeleza kiuchumi na kihuduma kwani tulikua
tunampenda Mungu na tulikua waimbaji na waombaji kanisani. Baada ya muda
mrefu katika maisha ya ndoa na familia, baadaye maisha yalianza kuwa
magumu kutokana na mishahara yetu kuwa midogo ukilinganisha na mahitaji.
Mume wangu alijisikia vibaya sana zaidi yangu hasa pale alipoona
wengine hasa marafiki zake wanafanikiwa lkn yeye hafanikiwi. Kuna
maaskari walikua wakipandishwa vyeo haraka na kuhamishiwa mijini ikiwemo
Daressalaam na Arusha- hali hiyo ilimpa shida sana akawa anaomba na
kufunga kwa muda mrefu lkn hakuona mafanikio.
Wakati fulani ilitokea akakutana na rafiki yake askari mwenzie,
akamualika nyumbani kwake. Mume wangu aliporudi akaja akiwa mwenye
mawazo makubwa sana, sikujua ni kwanini na hukuniambia hata
nilipomuuliza.
Baada ya siku kadhaa mume wangu akaacha kwenda kanisani wala huduma
hakufurahia tena. Akawa ni mkimya na mwenye mawazo mengi sana. Siku moja
akaniambia atasafiri kikazi kwa muda wa siku tatu. Baada ya siku tatu
akarudi akiwa hoi sana na mgonjwa km mtu mwenye malaria. Nikajaribu
kumshawishi twende hospitali hakukubali kbs akaniambia ni uchuvo tu wa
safari na kazi na atakuwa salama. Kesho yake, kweli akaamka vzr na
kwenda kazini bila kuugua km hapo jana. Ikapita muda mrefu bila kujua
hasa nini kinachoendelea kwa mume wangu kwani hakuniambia chochote hata
nilipomuuliza.
Baada ya muda, mume wangu akapata nafasi ya kwenda masomoni Moshi.
Alipomaliza masomo hayo,haikuchukua muda mrefu tukapata barua ya
uhamisho wa mume wangu kikaz kuelekea Arusha mjini.
Binafsi nilifurahi sana, nikajua Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya
siku nyingi. Kwa hiyo na mimi nikaanza mipango ya uhamisho. Tulipofika
Arusha tukapata makazi mapya na kanisa zuri la kuabudia. Baada ya muda
niligundua mume wangu hakupenda mambo ya Mungu km siku za zamani. Wakati
huu mimi nilikua mjamzito nikijandaa kupata mtoto wa pili.
Tulizungumza sana na mwenzangu lkn sikujua hasa kitu gani kulikua
kinamsumbua. Baada ya muda niligundua mume wangu alikua mlevi wa pombe
na tabia yake ilibadilika sana hasa kuhusu mambo ya kiimani na
kushirikishana mipango. Aligeuka kuwa mtu wa mambo mengi,kuamrisha na
msiri sana- kutokana na aina ya kazi zao nikajua ni kawaida.
Nilipojifungua mtoto wetu wa pili akaniletea zawadi ya gari mark2-mimi
nilikua miongoni mwa wanawake wachache kuendesha mark2 wakati miaka ya90
mwishoni. Tulijisikia vzr sana na mambo ni kama yalikua yananyooka.
Mwaka 2001 mume wangu alipata nafasi ya kwenda tena chuoni kusoma kwa
muda mfupi huko Dar, nikabaki na familia na nikawa naendelea vzr na kazi
zangu. Alipomaliza masomo akarudi na maisha yakaendelea kwa muda km
kawaida. Baada ya miezi km sita kutoka chuo ni, mume wangu akaniambia
anataka kuacha kazi- nilishangaa sana nikamuuliza maswali mengi lkn
hukunijibu vzr. Wiki moja baadaye akaniambia ameacha kazi na ameajiriwa
shirika moja kubwa la UN hapa Arusha.
Kweli akaanza kuvaa sare mpya za kazi hiyo mpya. Kazi hiyo mpya
ilituletea mafanikio makubwa sana ya kifedha na kujieneza kwa mali.
Wakati huo pia mimi nilipata nafasi ya kwenda kusoma chuoni muhimbili
Dar kwa muda wa miaka mitano. Nikaenda Dar nikaiacha familia ikiendelea
vzr kbs.
Nikiwa Dar chuoni nilipata nafasi ya kwenda nje ya nchi kufanya seminar
ya health exhibitions (mafunzo ya maonesho)- nikiwa huko nilipigiwa simu
kuwa mtoto wetu mdogo amefariki dunia. Nilichanganyikiwa nikarudi
nyumbani kwa kuchelewa, nikakuta wameshamzika Alfred mwanangu sikumuona
tena. Ilisemekana alifariki ghafla sana bila kujua hasa ni ugonjwa gani
au alipatwa na nini mwanangu. Niliongea na madaktari, wakanieleza kuwa
mwanangu alitokwa na damu nyingi sana mpk ndani ya jeneza. Uchungu
mkubwa na kuchanganyikiwa vilinipata bila kujua hasa nini cha kufanya.
Niliporudi msibani nilishangaa kumkuta mume wangu akiwa na pete kubwa ya
dhahabu yenye kinakshi cha tanzanite katikati mkono wa kuume.
Nilipomuuliza akaniambia amenunua mjini bei ghali sana na pia ameninulia
na mimi aina km hiyo ya pete. Sikujua chochote nikaipokea ile pete km
zawadi nikawa naivaa. Pia akaniambia kuna kanisa jipya limeanzishwa hapa
mjini ndio tutakua tunasali. Huko tulikutana na watu mbalimbali wa
mataifa mengine na ibada zilikua ni za kiingereza. Tulienda
kutambulishwa na mume wangu kwa mchungaji ambaye nayepia alikua amevaa
pete km ya mume wangu-sikujali sana kwa siku hiyo. Nilijisikia vzr sana
kwani huko nilimuona mume wangu akifurahia na kujitoa km zamani. Pia
tulipata marafiki wengi akiwemo familia moja ya wakameruni waliokua
karibu sana sisi. Tukahamia huko.
Baada ya muda baada ya kuipata ile pete na kurudi chuoni na kujiunga
kanisa jipya huku Arusha, sikupenda tena kwenda kanisani wala
kujishughulisha na mambo ya huduma kama awali. Nilijiona mwenye majukumu
mengi sana na sina muda wa mambo ya kanisani na huduma. Wenzangu
waliponiuliza, niliwajibu kuwa niko bize sana na masomo na shughuli za
kikazi. Nikawa mzembe sana ktk mambo ya imani na huduma.
Lkn siku moja Nikiwa Dar wakati wa fellowship za chuoni, ndugu mmoja
alitutembelea akahubiri kwa nguvu sana akatuambia kuna mtu amezingirwa
na roho mbaya za kichawi zinazotafuta kumuangamiza na familia
yake-sikuelewa hata kidogo wala hakupita mtu yeyote mbele siku hiyo.
Yule muhuburi alilia sana kwa uchungu mpk mwisho wa ibada.
Baada ya kumaliza masomo mwaka 2007 nilirudi Arusha. Nikapata marafiki
wengi na mitandao mbalimbali ya kibiashara ndani na nje ya nchi. Pesa
ilikuwa nyingi mpk nikashangaa kuwa ni baraka za namna gani.
Mwaka 2009 siku moja nilishtuka na kitu kimoja pale mume wangu
aliposahau pete yake (ile nyingine anayovaa mkono wa kuume sio ya ndoa)
nyumbn. Mimi bila kujua nilipoiona niliihifadhi kwenye mkoba wangu
nikaondoka nayo. Kumbe nyuma yangu, mume wangu alirudi nyumbn ghafla na
kuitafuta sana pete akanipigia simu nikamwambia ninayo kwenye mkoba aje
nilipo aichukue. Cha ajabu alipokuja ili nimpe ile pete haikuwepo tena
kwenye mkoba. Nilijikagua na kuwauliza wafanyakzi wenzangu lkn pete
haikuonekana. Mume wangu alichanganyikiwa na kunishambulia kwa makofi na
matusi akiwa mwenye hasira kubwa- sikuwahi kumuona mume wangu akiwa
mwenye hasira na ghadhabu kubwa kiasi kile. Alinidhalilisha hadharani
mbele ya wafanyakazi wenzangu na kuniamrisha twende nyumbn haraka. Ofisi
yao ilikua nikaribu na ofisi kwangu lkn alinipandisha gari yake na
tukaelekea nyumbn bila kupitia ofisini kwao. Kwenye gari tulikua
tunagombezana kwani nilijisikia kudhalilishwa kwa hali ya juu sana.
Tulipofika nyumbani, ugomvi ulikua mkubwa sana na sana mume wangu
alinipiga kweli. Baadaye watu walikuja lkn hawakuweza kuingia ndani
kwani kulikua kumefungwa. Mume wangu alinifungia kwenye chumba kimoja na
nikamsikia akiwapigia simu watu kadhaa huku akilia km mtoto. Sikuelewa
kwa kweli. Mchungaji wa kule kwenye kanisa letu alikuja na mtu mmoja
ambaye alikua ni rafiki wa karibu wa familia yetu lkn foreigner.
Walipofika waliongea na mume wangu kwa muda afu wakaondoka. Mume wangu
akaja akanifungulia mlango akaniambia tuongee- wakati huo alikua mpole
na mkimya asiyelia tena.
Akaniambia kuwa ile pete iliyopotea ilikua ndio pete ya maisha yetu.
Alipewa na huyo mchungaji na ilikua inamasharti makubwa kuwa lazima
aivae yeye tu na isikae muda mrefu nje ya kidole chake. Kwa ufupi pete
hiyo haikuwa ya kawaida na ile pete ilikua ni yule mtoto wetu (Alfred)
aliyekufa miaka kadhaa iliyopita. Nilishtuka kujua hata ile pete
niliopewa mimi haikuwepo mkononi mwangu wakati huo. Ilikua imetoweka,
nikazimia kusikia maneno hayo. Nilipozinduka nilijikuta nyumbn kwa
mchungaji nikiwa nimelazwa kitandani. Kumbe nilipozimia nilipelekwa
hospitali na pia mume wangu akakamatwa na polisi akawekwa lokap lkn
akaachiwa bady kutokana na ushawishi wake pale polisi na alipowaelezea
anavyojua yeye. Alipotoka akaja hospitali wakanichukua mpk nyumbn kwa
mchungaji. Nilipozinduka nikamuona mchungaji na yule rafiki yetu
mkameruni walikua wamevaa pete km ile ya mume wangu iliyopotea.
Hawakunisemesha kitu wala hawa kuomba lkn waliondoka kule chumbani
wakiniacha na mume wangu mara baada ya kupata ufahamu.
Mume wangu alinichukua mpk nyumbn, tulipofika hatukuongea kitu mpk asbh.
Yeye alienda mjini baadaye akarudi akiwa bado mwenye mawazo na wasiwasi
mkubwa. Siku hiyo ikapita na kesho yake. Marafiki zangu walikuja
kunitembelea ili kunipa pole lkn hawakuruhusiwa. Kumbe mume wangu
aliwaambia watu pamoja na ndugu zangu kuwa nimemuibia mali nyingi sana
nimeficha kusikojulikana. Ndugu zangu walipokuja aliwaruhusu kwa
masharti kuwa nisiwaambie ukweli. Akanitisha kuwa nikisema ukweli
tutakufa wote.
Maisha yaliendelea kwa siku kadhaa, nikaendelea na kazi lkn nikiwa
mwenye mawazo makubwa. Nikaomba off kazini kwa muda ili nipate ahueni.
Mume wangu naye akaomba off pia tukawa tunashinda ndani tu. Nyakati za
usiku nikiwa nimelala mara nyingi niliota ndoto kuwa Alfred mwanangu
ananiita yuko barabarani anahangaika akiwa analia. Nikimwambia mume
wangu ananiuliza ni wapi eneo gani hasa, nikimtajia eneo nilipoota
ananiambia hapo ndipo pete ilipo kwa hiyo ataifuata- nakweli mara nyingi
alikua anaamka anaondoka eti kuifuata hilo eneo nilipomuona mtoto wangu
kwenye ndoto.
Pete ile haikuwahi kuonekana na maisha yetu yalianza kuporomoka siku
hadi siku. Mume wangu hakufurahi tena. Alikua ni mtu mwenye majonzi na
wasiwasi sana juu ya maisha yetu siku zijazo. Wakati huo aliwafukuza
wafanyakazi wote wa nyumbn na alininyanganya simu zote na alifungia
ndani nisitoke nje
Siku moja ikitokea mjini katika mizunguko yake alinijia na habari mpya
akidai kuwa ndio suluhisho la tatizo letu. Aliniambia kuwa ili turejee
ktk maisha yetu ya kawaida inabidi tumuue mtoto wetu Minza pia kwa siku
zote za maisha yetu kuanzia siku hiyo itakua ni marufuku kufanya mapenzi
kwa njia ya kawaida ila tu kinyume na maumbile (yaani awe ananiingilia
kinyume na maumbile ya mwanamke). Akaniambia hakuna namna nyingine ya
kurejesha maisha yetu zaidi ya hivyo. Nilishtuka sana nikaogopa mno.
Nilimlaumu sana mume wangu kwanini alijiingiza ktk maisha hayo- ndipo
akanieleza hbr kamili kuwa mafanikio yetu yote yametokana na mfumo huo
wa maisha tangu siku ile aliporudi ile safari tukiwa Karatu. Kumbe siku
ile alikua ametoka kwa mganga aliyepelekwa na yule rafiki yake.
Nilimshauri mume wangu twende kwa mchungaji tukaombewe lkn akasema kuwa
tukisema tu kwa watu tutakufa wote. Pia akasisitiza kuwa sisi wote tuko
katika mtandao huo kwa hiyo sio rahisi kujiokoa tena. Kesho yake mume
wangu alinikumbushia tena akasema ni lazima tufanye hivyo na pia sio kwa
kulazimisha inatakiwa iwe kwa hiari ili tupate faida kwa haraka. Bado
nilikataa, sikuwa tyr kufanya hivyo. Nilimuomba mungu usiku na mchana
atusaidie. Lkn mume wangu Alinitisha sana na kunifinya mwili ili
nikubali kwani alikua mwenye hasira na ghadhabu kubwa. Pia alinifungia
ndani ili nisitoke nje. Pia alisisitiza nisiombe kbs. Maisha yaligeuka
kuwa jehanam.
Siku km mbili zililizofuata tulipigiwa simu kutoka shuleni kwao na mtoto
wetu kuwa Minza ametoweka shuleni hajulikani alipo. Tulikwenda haraka
kujua hatma ya mtoto wetu. Niliogopa zaidi kwani nilijua labda ndio
keshapatikana- japo mume wangu alionekana kuwa si mwenye wasiwasi ht
kidogo. Nilianza kukumbuka kukemea na kuomba Mungu atusaidie lkn mume
wangu alinikataza nisiombe kbs. Akanizabua kibao kikubwa mdomoni tukiwa
kwenye gari mpk damu ikatoka mdomoni. Nikisikia uchungu mkubwa zaidi
kwanini maisha yalikua yanaenda hivyo ghafla au nini faida ya kuishi
basi.
Tulisafiri siku nzima mpk kufika shuleni kwa Minza mwanangu. Kitu cha
ajabu ni kwamba tulimkuta mtoto akiwa hospitali amelzwa haongei wala
hajitambui- na taarifa zinasema alikutwa chumbani(hostel) kwao mchana
huo akiwa anatokwa na damu nyingi.
Siku kadhaa bdye tulipewa mtoto wetu baada ya kupata nafuu tukarudi naye
nyumbn kwa matibabu zaidi. Minza aliendelea kuugua sana bila nafuu na
hakuweza kuzungumza kitu alikua ni mtu wa kulala kitandani na kutazama
tu.
Ilipita miezi kadhaa maisha hayo yakawa yamechukua sura ya familia
yangu. Miradi kadhaa tuliyoifungua mjini ilikua imefungwa, pia kazini
kwangu nilikua nakwenda kwa shida sana. Uwezo wangu wa akili na
kiutendaji ulipooza sana. Nilijiingiza kwenye chama cha ulevi wa pombe
km mume wangu ili kupoteza machungu na kupunguza mawazo. Lkn hai
kusaidia. Lkn kule kanisani tuliendelea kwenda na mume wangu aliendelea
na kazi kule UN.
Siku moja mume wangu aliniambia tunakwenda shambani kwa siku kadhaa
twende wote- tulijiandaa tulikwenda pamoja. Tulipofika huko, tulijumuika
pamoja na mchungaji na yule rafiki yetu mkameruni. Tulifurahi na kunywa
na kula mpk usiku kwa siku hiyo ya kwanza. Kesho yake asubuhi na mapema
niliitwa na mume wangu kuwa kuna kikao- Cha ajabu ni kwamba asbhu hiyo
mchungaji na yule mkameruni walikua wamevalia mavazi ya kitamaduni
kupitiliza kawaida yao. Tulikwenda mpk vichakani zaidi kwani walisema
kuna maongezi muhimu sana.
Tukiwa huko yule mchungaji alitueleza waziwazi kuwa yeye ni mtu mwenye
nguvu nyingi sana na amewasaidia wengi sana. Na pia hata zile mali za
kwanza na kufanikiwa kwetu ni yeye ndiye aliyetusaidia kwa nguvu zake.
Na nguvu hizo ni zilitokana pete yake. Pete yake ndio inayompa nguvu na
kumletea bahati na mvuto kwa watu.
Kwa kuwa tulikua tumeshindwa kutekeleza sharti la kwanza la kumuua Minza
na muda ulikua umepita basi, kuna sharti lingine la mwisho
Kwa hiyo, akasema anao uwezo wa kutupatia pete nyingine lkn ndio kwa
masharti. Na leo hapo yuko tyr kutusaidia tena ili tufanikiwe na tusife-
kwani tulikua tumefanya makosa makubwa sana kupoteza ile pete ya awali.
Akatoa masharti ili tupate pete nyingine inabidi mimi nikubali pale
niingiliwe kimwili nao wote watatu. (yaani nifanye mapenzi na wote
watatu pale kichakani hadharani na mmoja baada ya mwingine akianza mume
wangu). Vinginevyo mume wangu atapoteza maisha pale pale na mimi pia
ningekufa siku zijazo au ningekua kichaa. Nilishtuka nikaogopa sana,
nikaanza kupiga mayowe huku nilikimbia kuelekea kwa mume wangu- nililia
sana kwa uchungu huku nikitaja jina la mume wangu kwa kumlaumu kwanini
alijiingiza kwenye mambo hayo. Mume wangu alinisihi nikubali ili tusife
kwani hakukua na namna nyingine.
Sikukubali. Nilianza kukimbia kuelekea barabarani kuhofia usalama wangu
kwani niligundua mume wangu hakuwa na uwezo tena wa kunisaidia au
kujiokoa. Nilpofika mahala tulipopark magari yetu sikuona gari ht moja.
Nikiwa ktk hali ya kukimbia na kujiokoa huku nikipiga mayowe niliwaona
yule mchungaji na yule mkameruni wamenitokea nyuma na mbele yangu.
Ghafla yule mchungaji aliniwekea mkono kichwani nikaanguka chini
nikapoteza fahamu.
Niliporejea fahamu zangu ni siku nilipojikuta niko katikati ya kundi la
watu walinisimamia na kuniangalia kwaumakini mkubwa sana. Kumbe ilikua
ni kwenye maombezi. Fahamu zangu zilinirejea na kujitambua japo nilikua
nimeharibika mwili na mavazi machakavu pia nikiwa nimefungwa kwa kamba
ngumu sana. Nikifanikiwa kuwatambua baadhi ya ndugu jamaa na marafiki
waliokuwepo pale.
Kwa masaa kadhaa nilijisikia kupumbaa kama mjinga bila kujua nifanye
nini. Alitokea mtu mmoja akaniambia pole. Akaniuliza kama ninajisikiaje
kwa wakati huo. Nikamuelezea. Kisha nikamuhoji kuwa hapo ni wapi-
akaniambia kuwa ni kituo cha maombezi na yeye ndiye mchungaji.
Inasemekana kuwa siku hiyo nilikua nimefunguliwa kutoka katika ukichaa
ulionisumbua kama miaka mitatu na nusu. Katika muda wote huo niliishi
msituni km mnyama. Nilitafutwa na ndugu zangu kwa muda mrefu sana bila
mafanikio. Hakuna mtu alijua mimi au mume wangu tulikua wapi.
Baadaye Nilipouliza kuhusu mwanangu Minza na mume wangu, nijibiwa kuwa
waliokufa miaka mitatu na nusu iliyopita. Ndipo nikakumbuka mambo magumu
ya maisha yaliyonipata. Nilitunga msiba mkubwa upya kabisa. Nililia
sana na kujionea huruma kama yatima asiye na msaada. Sina cha kusema
zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote. Hata uhai nilionao leo ni Mungu tu
amenisaidia.
Sasa hivi nipo tu kwa ndugu zangu tunaishi na maisha yangu mapya ya
kumtumaini Mungu wangu kwa upya kabisa. Bwana Yesu Kristo ndiye msaada
wangu wa karibu. Ninamshukuru Mungu kwa familia yangu mpya ya wana ndugu
ndani ya Kristo Yesu. Mungu awabariki.
AMEN.
UJUMBE HUU UMEKUJA KWAKO KWA MAFUNDISHO YA KIROHO JUU YA IMANI POTOFU
ZIHARIBUZO KUSUDI LA MUNGU JUU YA MWANADAMU NA ULIMWENGU KWA UJUMLA.
MWAMINI YESU UPATE UZIMA WA MILELE
No comments:
Post a Comment