KAMA wewe
ni mwanaume, basi bila shaka unafahamu ile milio na miguno ya wanawake
wakati wa kujamiiana, na kama wewe ni mwanamke pia unafahamu kwamba huwa
unatoa milio na miguno hiyo. Ni nini basi kinachopelekea milio na
miguno hii kutolewa? Je milio na miguno hii ni ya kweli au ni zuga tu,
ili kumfanya mwanaume ajisikie “kijogoo“?
Baadhi ya wataalamu wa masuala ya kujamiiana
na mapenzi walijiuliza pia maswali hayo. Mwaka jana, Gayle Brewer wa
Chuo Kikuu cha Central Lancashire na Colin Hendrie, wa Chuo Kikuu cha
Leeds waliibuka na utafiti wao waliouita “Copulatory Vocalization“ (kwa
tafsiri nyepesi-“Milio/sauti za kujamiiana”). Katika utafiti huo,
waliuliza wanawake 71 ambao wanashiriki tendo hilo mara kwa mara
(sexually active) kati ya umri wa miaka 18 na 48 kwa ajili ya kupata
undani zaidi wa suala hili la kutoa milio wakati wa kujamiiana.
Wataalamu hao waliweza kubaini kwamba wengi
wa wanawake hao walikuwa wanatoa milio, lakini sio tu wakati wanafika
kileleni (orgasm), bali 66% walisema walitoa milio, ili kuharakisha
wanaume zao kufika kileleni, na 87% walisema kwamba walitoa milio, ili
kumfanya wanaume ajisikie “Kijogoo” (boost his self-esteem).
Wataalamu hao waliongeza kusema kwamba
“Wakati mwanamke kwa kawaida hufika kileleni wakati wa kutomasana, mara
nyingi milio ya kujamiiana imeripotiwa kutokea mara kwa mara kabla au
sambamba na wakati ambao mwanaume anafika kileleni“. Walisema pia katika
utafiti wao imebainika kwamba wakati mwingine wanawake walitoa milio na
miguno, ili kukabiliana na kuboheka, uchovu, na maumivu wakati wa tendo
la ndo, kwahiyo basi wanaume inabidi kuwa makini kwani wakati mwengine
kumbe mtoto wa watu ana umia! Au pengine yupo kwenye zile harakati za
kukuzuga, ili ujione “Kijogoo”?
Wataalamu wanaendelea kusema kwamba tatizo
kubwa ni kwamba jamii imefanywa kuamini kwamba milio wakati wa tendo la
kujamiiana huusishwa na mwanamke kufika kileleni au kufurahia tendo
hilo, kiasi kwamba imefikia wanawake kuona ni busara kudanganya (fake)
kwamba wamefika kileleni (wakijua fika kwamba mwanaume tayari ana amini
hivyo) wakati kumbe hawajafika popote.
Wataalamu wanaonya kwamba sio busara kwa
wanawake kudanganya kwamba wamefika kileleni, kwani kufanya hivyo
kunapelekea wanaume kufikiri kwamba wanafanya kila kitu sawa wakati wa
mapigo, wakati kumbe sio. Mwalimu wa elimu ya kujamiiana, Patty Brisben,
anashauri kwamba wanawake watumie miguno/milio kama “njia ya kuonyesha
kwamba wanafurahia tendo, lakini sio njia ya kuficha kama tendo
hawalifurahii.”
Kuficha au kutokuficha, wataalamu wanasema
kwamba suala la kutoa milio/miguno wakati wa tendo la kujamiiana sio
suala la binaadamu peke yao, utafiti kwa wanyama umebaini kwamba hata
manyani jike (baboons) hutoa milio fulani kabla au wakati wa tendo hilo.
Nyani jike hutoa milio fulani kuhashiria kwa nyani dume kwamba yupo
tayari kwa tendo hilo na pia manyani jike huongeza milio wakati
wanajamiiana na nyani dume, ambae ana cheo katika kundi lao
(higher-ranked male baboon). Zaidi ya hayo, nyani jike aina ya “Macaque”
amebainika pia kutoa milio/miguno wakati wa tendo hili nyeti, ili
kumfikisha mwenza wake kileleni haraka!
Mwisho wa yote wataalamu wanamalizia kusema
kwamba suala la kuridhishana kimapenzi (tuite “ukijogoo” wa mwanaume au
vinginevyo), ni suala muhimu kwa pande zote mbili, yaaani mwanaume na
mwanamke. Kwahiyo basi, suala la kutoa milio sio tu suala la mwanamke
kudanganya au kufanya mambo asiyotaka, bali ni suala la kuwepo “hai”
(sexually present) (mara ngani umeshasikia wanaume wa kitanzania
wakilalamika kuhusu wanawake wanaokaa kama “gogo” au “kusoma gazeti”
wakati wa kujamiiana??) wakati wa tendo hilo na kubadilishana mahaba na
mwenza wake.
Mwisho kabisa, wanasema, “wote (wanaume na wanawake) tutoe milio!”
Je unakubaliana na utafiti huu?
Source: CNN Health
No comments:
Post a Comment