Utafiti uliofanyika na kutolewa miezi kadhaa iliyopita na Vyuo Vikuu Vya
Rice na North Texas, umegundua mambo kadhaa muhimu linapokuja suala la
wanawake kupendelea zaidi kutoka na wanaume warefu. Watafiti hao
walifanya utafiti katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza, waliangalia
vipaumbele vya wanawake na wanaume katika suala zima la kudeti (Dating
Prefences) kwa kutumia matanganzo ya mapenzi 925 (personal dating ads)
yaliyowekwa Yahoo!.
Sehemu ya pili ya utafiti ilihusisha wanaume 54 na wanawake 131 kutoka
chuo fulani Marekani, ambapo majibu yao kwa maswali waliyoulizwa
yalidhibitisha tafiti zilizowahi kufanyika siku za nyuma. Katika majibu
yao, zaidi ya nusu ya wanawake (asilimia 55 ya wanawake) walisema
wanapendelea zaidi kudeti wanaume warefu, wakati asilimia 37 ya wanaume
walisema wanapendelea kudeti wanawake wafupi.
Embu tuchambue kidogo…hii ina maana gani? Ina maana kwamba mambo hayapo
sawia hapa (no balance), kwani wakati asilimia 55 ya wanawake wanataka
wanaume warefu, ni asilimia 37 tu ya wanaume wanaotaka wanawake wafupi,
angalau kwa mujibu wa utafiti huu. Kwa maana hiyo basi wanaume pia
wanapendelea wanawake warefu? Tukumbuke pia idadi ya wanaume (55)
waliolizwa ilikuwa ni ndogo ukilinganisha na wanawake walioulizwa (131).
Poa tuendelee basi, ili tuone utafiti huu ulibaini lipi la ziada…
Kati ya wale watu 925 waliolizwa, 455 walikuwa ni wanaume wenye wastani
wa umri wa miaka 36 na urefu wa futi 5 na inchi 8 (177 cm) na wanawake
walikuwa 470 wenye wastani wa umri wa miaka 35 na urefu wa futi 5 na
inchi 4 (165 cm). Matokeo ni kwamba, wanaume asilimia 14 tu ndio
walisema wanapendelea kudeti wanawake wafupi. Hapa pia wanaume wachache
sana wameonyesha kupendelea wanawake wafupi, na tukumbuke kwamba katika
kundi hili idadi ya waliolizwa ilikuwa inakaribiana sana, yaani wanaume
455 na wanawake 470.
Ilipokuja kwa wanawake wale 470 walioulizwa, karibia nusu au asilimia 49
walisema kwamba wanataka kudeti wanaume warefu kuliko wao tu! Na baadhi
yao walinukuliwa wakisema yafuatayo:
“Kama mwanamke, najisikia na amani zaidi (secure) [anapokuwa na mwanaume
mrefu]. Nahisi kama kuna kitu akipo sawa nikifikiria kumuangalia
mwanaume wangu kwa chini!” alisema mmoja wa washiriki hao. Na mwingine
nae akasema..
“Kuna pia suala zima la kuvaa viatu vya mchuchumio (high heels) na
wakati huohuo bado kuendelea kuwa mfupi mbele ya mwanaume wako. Na pia
nataka kumkumbatia huku mikono yangu ikimzunguka shingoni”. Nafikri
unapata picha jinsi jamaa alivyo mrefu kwake au sio?
Hayo ni baadhi tu ya maoni ya wale walioulizwa kwanini wanapendelea
wanaume warefu, bila shaka unaweza ukafanya utafiti wako mwenyewe kwa
kuuliza wanawake wachache unaowafahamu kwanini wanapendelea wanaume
warefu. Sababu nyingi huwa zinajirudia (kama hii sababu ya kujihisi na
amani a.k.a “secure”), lakini si ajabu unaweza ukajikuta unaibua sababu
nyingine mpya lukuki!
No comments:
Post a Comment