WANAWAKE wengi waliowazuri wa sura huwa
wanapenda kuolewa na wanaume wabaya wa sura. Hii inatokana na ukweli
kwamba wanawake wenye sura nzuri hupenda kuolewa na
wanaume wenye sura mbaya ili kulinda uzuri wao kwani wanaamini kuwa
iwapo ataolewa na mwanaume mwenye sura nzuri, uzuri wake hautaonekana
kwa watu kwani mwanaume pia ataonekana mzuri jambo ambalo litamupunguzia
mwanamke kuonekana mzuri katika jamii. Hii ndio maana wanawake wengi
wenye sura nzuri wanapenda kuolewa na wanaume wenye sura mbaya. Dr.
Linda Mtaalamu wa masuala ya mapenzi na uhusiano anasema " Wanawake
wengi wenye sura nzuri wanatabia ya kutaka waonekane kuwa ni warembo,
jambo ambalo linawapelekea kuolewa na wanaume wenye sura mbaya ili
waendelee kushine katika jamii".
Pia wanaume wenye sura mbaya wanapenda
kuoa wanawake wenye sura nzuri ili kulinda hishima yao kwa kupitia wake
zao. Kwahili ndugu msomaji naomba ujaribu kufanya uchunguzi wa kina kwa
kuangalia wanaume wenye sura mbaya, utagundua kuwa wengi wao wanapenda
kuoa wanawake wazuri na wengi wao tayari wameshaoa wanawake warembo. Je,
kwa upande wa wanawake weusi; je, wanapenda wanaume wa aina gani? Na
kwa upande wa wanaume weusi pia wanapenda wanawake wa aina gani? Pia na
wewe kama unajitabua kuwa uko hivi au vile je, unapenda sweetheart wako
aweje. Sasa tujadili.........................!!!!!
No comments:
Post a Comment