Magonjwa ya ngono ni maambukizi yanayosambazwa kwa njia ya tendo la
ngono au kujamiiana. Magonjwa haya kwa karne nyingi yamejulikana kama
nyororo la maangamizi au bomu la kibaiolojia. Hii ni kutokana na ukweli
kuwa ukiona mgonjwa mmoja mwenye tatizo la ugonjwa wa kuambukiza kwa
njia ya ngono basi ni muhimu kutambua kuwa kuna mtu mwingine nyuma yake
ambaye ana tatizo hilo pia.Kwa kawaida wasichana huwa katika hatari
kubwa zaidi ya kupata magonjwa ya ngono kama watajiingiza katika vitendo
vya kujamiiana. Sababu kubwa zinazowaweka katika hatari ni ile hali ya
kushindwa kuamua namna ya kufanya ngono kwa tahadhari, maumbile ya kike
kama mpokeaji na kutokukomaa kwa shingo ya mji wa mimba nazo ni sababu
zingine zinazoongeza hatari.
Magonjwa mengi ya ngono husababishwa na bakteria, virusi, kuvu (fungus), protozoa na parasaiti. Magonjwa yasababishwayo na bakteri ni kama vile kisonono, mitoki (Granuloma inguinale na Chancroid), kaswende na klamydia. Magonjwa kama vile malengelenge (Herpes simplex), molluscum contageosum, viotea (warts), virusi vya UKIMWI na saratani ya mlango wa kizazi (HPV infection) haya hutokana na virusi. Magonjwa yasababishwayo na kuvu ni kama vile kandidiasisi ambayo huambatana na muwasho sehemu za siri. Magonjwa yaletwayo na protozoa kama vile Trikomoniasisi pia husababisha muwasho sehemu za siri na hutokwa kwa majimaji machafu yenye harufu mbaya hasa kwa wanawake. Upele na chawa wanaokuwa kwenye nywele za kinenani haya pia ni magonjwa ya ngono yanayosababishwa na parasaiti.
Dalili za magonjwa ya ngono hujitokeza kwa njia na dalili nyingi. Wakati mwingine magonjwa haya hayatokezi dalili zozote na pia mgonjwa anaweza kupata maambukizo ya magonjwa mawili au zaidi kwa wakati mmoja anapotenda tendo la ngono. Hatari kubwa zaidi inayoambatana na magonjwa haya ni kutokuwepo kwa dawa zinazotibu baadhi ya magonjwa haya kama vile UKIMWI.

No comments:
Post a Comment