WATAALAMU
wamesema kwamba matango ni chakula muhimu sana katika mwili wako
kutokana na kufanhyakazi mbalimbali za kuuweka sawa pamoja na kuupa
maji.
Ni vyema kuhakikisha kwamba kila siku unakula tango kwa afya yako.
Hakika kama upo bize sana kiasi cha
kusahau kuinywa maji ya kutosha, kula tango ambalo asilimia 90 ni maji.
tango litakuongezea maji unayohitaji.
Tango pia linakabiliana na joto nje na
ndani ya mwili. ndio kusema kwa kula tango mwili unapunguza mashambulio
ya kiungulia. Pia kama utajipaka tango utapata nafuu sana dhidi ya miale
ya jua.
Kazi nyingine ya tango ni kupunguza sumu
katika mwili, maji yote yaliyomo ndani ya tango linafanya liwe kama
fagio la kuondoa sumu mbalimbali mwilini na ulaji wa kila mara wa tangu
unasaidia kuondoa mawe katika figo (kidney stones).
Aidha tango linasaidia kukupatia
vitamin.Tango lina vitamin nyingi zinazohitajika katika mwili kwa siku.
Kuna vitamin A,B,C ambazo hupiga busti katika mfumo wako wa kinga kukupa
uangavu na nishati unayoihitaji.
unaweza kufanya jusi ya tango kuwa na
nguvu zaidi kw akuichanganya na karoti na spinachi.Usimenye tango lioshe
na kulila na unaposaga kupata juisi vivyo hivyo kwani ngozi yake
inavitamini C kiasi cha asilimia 123 ya inayohitajika kila siku katika
mwili.
No comments:
Post a Comment