Kuna urembo mbalimbali wa macho
kulingana na taste ya mtu na mapendeleo yake . Leo nitazungumzia "smoky
eyes" au macho yaliyapambwa kwa eye liner, mascara na eye shadows zenye rangi nyeusi, grey au za mng'aro.
Jinsi ya kuremba jicho:
-hakikisha uso na ngozi inayozunguka
jicho ni safi kabla ya kuanza urembo wowote usishawishike kupaka
vipodozi juu ya ngozi chafu haitakaa vizuri make up yako. Safisha kwa
kutumia face towel iliyochovywa kwenye maji ya moto(huwa naona ni rahisi
kwangu hasa kama kitambaa nitumiacho ni cheupe ni rahisi kujua kuwa u
msafi au la kwa kuangalia kitambaa) kamwe usioshe uso wako kwa sabuni au
maji ya moto. Ngozi ya uso iko rahisi kudhulika ikipata msukosuko
kidogo. Sabuni huwa na kemikali nyingi na maji ya moto yanapausha uso.
kama utalazimika kutumia sabuni osha uso kwa maji ya baridi kwa muda
kiasi ili kuondoa kemikali zitakazokuwa zimeachwa.
- tayarisha kope/eye lids zako kwa
kupaka wanja mweusi kwa uangalifu au eyeliner ya dark colour kama ni mtu
anayejiamini unaweza tumia rangi yoyote ile sababu si wote wanaweza
paka rangi ya njano au kijani na wakawa confident na muonekano wao.
-Kwa matokeo mazuri uwe na eye shadow za
aina mbili moja ya rangi iliyokolea na nyingine iliyo light. Anza na
rangi iliyo light paka kwa uangalifu kuelekea kona ya nyusi kama picha
hapo chini
endelea kama unapenda ming'ao
machoni(hususani kwa sherehe) unaweza kupaka juu ya kope zako ila
hakikisha hufiki mbali sana karibu na nyusi . Kisha malizia na darker
colour kama picha ya kulia inavyoonyesha anzia kona ya kushoto ya jicho
kwenda kulia kwa kiasi upendacho.
-Linganisha macho yako yote kama yana muonekano sawa kisha unaweza kuongezea mascara kwa juu ya nyusi ikiwa ni mpenzi.
No comments:
Post a Comment