Jambo hili huwaacha wanawake wakiwa
wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali chungu mzima kama kuna mahali
wamekosea au hawajawavutia wapenzi wao, pale wenzi wao wanapogeukia upande wa pili na kushikwa na usingizi punde tu baada ya kumaliza tendo la kujamiiana.
Lakini utafiti uliofanywa hivi na
wanasayansi unawapa wanaume ahuweni katika kuepuka lawama hizo, kwamba,
kumbe siyo hiyari yao, bali ni maumbile.
Wanasayansi hao wamebaini kwamba, kwa
sababu za kimaumbile ubongo wa wanaume unawalazimisha kulala muda mfupi
baada ya kushiriki tendo la kujamiiana. Katika utafiti wao wanasayansi
hao walibaini kwamba, kwa jinsi ubongo wa mwanaume ulivyotengenezwa,
pale wanapomaliza tendo la kujamiiana na kufika kileleni kuna eneo
linalozimika na kuwafanya kupata usingizi.
Wakati hilo likitokea kwa wanawake hali
ni tofauti, kwani wao hubaki wakikodolea macho dari wakiwa
wamechanganyikiwa na kujiuliza maswali lukuki, wakijihisi kutowaridhisha
wapenzi wao.
Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha
kipimo cha kumulika, maarufu kama scan, ambapo kilitumika kuwamulika
wanaume katika ubongo wao pale wanapofanya tendo la kujamiiana na baada
ya kumaliza kujamiiana na kufika kileleni na kubaini kwamba, eneo
linalojulikana kama cerebral cortex, eneo linalohusika na ‘fikra’
huzimika baada ya mwanaume kufika kileleni.
"Utafiti huu unatupa matokeo ya kile
kinachotokea ndani ya ubongo pale mwanaume anapofika kileleni.” Gazeti
la Mirror lilimnukuu mwanasayansi mmoja wa serikali ya Ufaransa aitwae
Serge Stoleru.
“Lakini kwa wanawake inaonekana ni tofauti kabisa……” Aliongeza kusema mwanasayansi huyo.
Mwanasayansi huyo aliendelea kusema
kwamba, wanawake hushangazwa sana na jambo hilo na ndio sababu hubaki
wakiwashangaa wapenzi wao wanapolala baada ya kumaliza tendo ilo hali
wao wakitaka zaidi….
Kwa hiyo hakuna sababu ya wanawake
kuwalaumu tena wanaume baada ya kumaliza tendo na kulala kwa sababu hivi
sasa wameshajua sababu, watuwache tupumuwe……
No comments:
Post a Comment