Leo
kwenye shosti talk nmewaletea topic kutoka kwa Lizz David. .anatuelezea
kuhusu kudumu au kutokudumu kwa ndoa ya wanawake waliolala na wanaume
wengi. .shuka ujisomee na usiache kuchangia mada 8020forums.
Napenda kufikiri kuwa mwanamke ambae
anaweza kudumu katika ndoa ni yule ambae amejitunza, yule ambae ni bikra
, hajawahi kukutana na mwanaume yoyote mpaka siku ya harusi
yake Hata hivyo wachunguzi wameona kuwa
hakuna ubishi katika hilo, hawakai ukweli huu. Wamekuwa wakijiuliza
maswali yenye majibu sahihi.
Kizungumkuti hiki kimekuja baada ya
wachunguzi na watu wanaoshughulikia maswala ya taasisi ya mafunzo ya
ndoa na familia, kuhusu kabla ya ndoa na baada ya ndoa. Wanajiuliza
kama kujamiana kabla ya ndoa inaathiri wanandoa, na kuwa na uwezekano
mkubwa wa talaka.
Jibu lilikuwa nini? Kujamiana kabla ya ndoa inashawishi talaka wakati mwingine,lakini inategemea na sababu zingine.
Lakini naona Talaka inaletwa na
mwenendo, kiwango cha talaka kinashuka kama watu wataoa wanawake bikra
na huenda wakawa sawa na wanawake ambao wamejamiana na wanaume wawili
tu kabla ya ndoa. Lakini wale ambao wamejamiana na wanaume zaidi ya kumi
kabla ya ndoa , kiwango cha talaka ni kikubwa.
Lakini ngoja. Kinachoshangaza ni hiki,
mwanamke ambae amejamiiana na wanaume wawili tu kabla ya ndoa huenda
wakawa na kiwango kikubwa zaidi cha talaka kuliko wale ambao
wamejamiana na wanaume zaidi ya 10.
Kwa kifupi mwanamke anakuwa anafanya kutofautisha mume alie nae na wanaume ambao amejamiana nao kabla ya ndoa.
Wachunguzi wa mambo ya ndoa na familia
wamegundua kuwa kila mwanamke aliepewa talaka alikuwa ameshatembea
na wanaume zaidi ya wawili kabla ya kuingia kwenye ndoa.. Na wamegawa
katika makundi matatu ya wasicana ambao wanatarajia kuingia kwenye
ndoa sasa , hasa kuanzia 2016, 2018, 2020.
Hutashangaa kuwa , wasichana wadogo
wengi wanaoolewa kipindi hiki wanaelewa zaidi , na wana uzoefu mkubwa
wa kujamiana kuliko wale waliopita .
Kwa nini tabia ya kujamiiana imebadilika
sana miaka hii. ? majibu mengi kwenye swali hili ni kwamba ,
wanajihusisha zaidi humo. Wasichana wanafanya mapenzi kwa kuangalia
mwonekano wa nje na kuingia ndani ya mahusiano hivyo. Kuangalia sura,
mazingira ya mtu. Inaonyesha kipindi hiki ni kinachoendelea ni
wachache sana watakuwa kwenye mahusiano ya ndoa kuliko wale waliozaliwa
miaka ya 1970, na wa 1980. Kushuka chini.
Kwa hio imegundulika kuwa mwanamke
akiolewa bikra ni ngumu sana kupata talaka. Wengi wa wanawake wanaolewa
sasa hivi hawafiki miaka mitano wanapata talaka , ukifika huko wewe
ni mmoja wa wale
Bikra au uliwahi kujamiana na wanaume
wawili kabla ya ndoa. Au ni tabia imebadilika kwa neema ya Mungu umepona
kwa hilo.Tukumbuke kuanzia mwaka 2000 talaka zimekuwa ni nyingi mno.
Labda ni ktu kisichotegemewa kufikia
mtu kujamiana na mtu zaidi ya mmoja kupata talaka, kitu kikubwa cha
kushangaza ni kwamba , kinachonekana ni kweli miaka hii. Ijayo, wanawake
ambao wamejamiana na zaidi ya wanaume wawili watakuwa na kiwango
kikubwa cha talaka .
Mwisho. Inaonekana katika mafunzo haya ,
hayaonyeshi dhahiri ukweli wake wa kuwa na talaka kwa watu walio
katika hatari ipi. Ni maamuzi yako , na ni wewe mwenyewe kuamua kama
unataka kujitunza mpaka uolewe au unataka wanza ujamiane na wanaume
wengine kabla ya ndoa kadri unavyotaka .Huwezi kujua yajayo na huwezi
kujidhibiti kwa hilo.
Nani anaejua kitafuata kitu gani
baadae, Ishi maisha yako yalio sahihi, fanya utakacho bila woga
kwamba nitaachika baadae , huwezi kujua hayo. ISHI MAISHA YA USALAMA.
Haya mashosti. .hapa swali kubwa Ni. .Ni
kweli mwanamke aliyelala na wanaume wengi..na nikisema wengi Ni kuanzia
wawili na kuendelea. .basi huyo hatodumu Kwenye ndoa.?
No comments:
Post a Comment